ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

European Union sio nchi bali ni ushirika wa nchi kama ilivyo EU. England, Wales, Northern Ireland na Scotland hazina mamlaka kamili. Scotland, Wales na Northern Ireland zina mabunge na serikali zao kama ilivyo Zanzibar lakini maamuzi makubwa yanayohusu UK yanafanywa Westminster.
Hatuwezi kuwa tumeungana Kama kila mmoja wetu atakuwa na mamlaka ya kujifanyia anavyotaka. Hata katika ndoa, wanandoa wanakubaliana kila mmoja kupoteza sehemu ya uhuru wake na kuishi katika misingi ambayo wanakubaliana. Tofauti na hivyo sio ndoa.

Amandla...
Naona hujanielewa naposema MAMLAKA KAMILI. Mfano Wales suala la michezo sio la "muungano/shirikisho" hivyo Wana timu za Mpira, rugby zinazoshiriki kimataifa. Ila Zanzibar licha ya kwamba michezo sio jambo la muungano Bado hawawezi peleka timu kushiriki michuano ya kimataifa.

Mamlaka kamili maana yake kujiamulia masuala ambayo sio ya muungano. Masuala ya muungano yaamuliwe Dodoma ila yasiyo ya muungano yaamuliwe na wazanzibar wenyewe.

Same to EU mambo mpaka ya kiuchumi, sheria za kazi, Common market etc Wana share ila Bado Kila nchi Ina mamlaka kamili kwenye masuala nje ya hayo niliyotaja!!
 
Yeye mwenyewe ndani ya chama chake Hana mamlaka kamili

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio Hana maana yeye anaongoza ACT kwenye masuala ya muungano na Tanzania Bara pekee ila ACT upande wa Zanzibar Ina mamlaka kamili maana inajiamulia masuala ya huko bila mTanganyika kuingilia vikao vyao. Wanaiita Kamati ya Mashauriano Zanzibar.

So huwezi kuona Zitto kwenye vikao vya ACT Zanzibar unless agenda ni za muungano.
 
Hawawezi kushiriki katika Olympics au World Cup kwa sababu vyombo hivyo vinatambua nchi zenye mamlaka kamili peke yake ( isipokuwa tu kwa Umoja wa Kifalme kwa sababu msingi wa mpira ulikuwa ni ushindani kati ya England, Scotland na Wales). Njia pekee ya Zanzibar kushiriki kama Zanzibar ni kutoka kwenye Muungano.

Amandla...
Ndio wanachotaka Zanzibar tuwe kma EU au EAC au Senegambia au Ghana-Guinea ila sio nchi imezwe kabisa Bali masuala ya muungano pekee ndio tushirikiane Kila mtu akiwa na nchi yake.
 
Naona hujanielewa naposema MAMLAKA KAMILI. Mfano Wales suala la michezo sio la "muungano/shirikisho" hivyo Wana timu za Mpira, rugby zinazoshiriki kimataifa. Ila Zanzibar licha ya kwamba michezo sio jambo la muungano Bado hawawezi peleka timu kushiriki michuano ya kimataifa.

Mamlaka kamili maana yake kujiamulia masuala ambayo sio ya muungano. Masuala ya muungano yaamuliwe Dodoma ila yasiyo ya muungano yaamuliwe na wazanzibar wenyewe.

Same to EU mambo mpaka ya kiuchumi, sheria za kazi, Common market etc Wana share ila Bado Kila nchi Ina mamlaka kamili kwenye masuala nje ya hayo niliyotaja!!
Mamlaka kamili sio hayo yanayozungumziwa. Zanzibar hawazuiwi na serikali ya Muungano kushiriki katika international sports. Kinachowazuia ni wao kutokuwa "sovereign country" yaani nchi inayotambulika kimataifa. Wales na Scotland zinashiriki kwa sababu za kihistoria na sio kwa sababu wao ni sovereign country. Mfano ni nchi ya Switzerland ambayo cantons zake zina mamlaka sana lakini hata siku moja hautasikia timu ya Geneva ikishiriki kombe la UEFA. Au timu ya Catalonia kutoka Spain.
Mfano wa European Union sio sahihi kwa sababu ile sio nchi bali ni ushirika wa nchi. Kwa sababu hiyo hauwezi kuulinganisha na JMT.
Shida ya Muungano wetu ni utambuzi wa masuala yapi ni ya Muungano na yapi sio. Na logically kama kuna masuala ambayo Zanzibar ina mamlaka kamili juu yake basi isishiriki katika masuala hayo kwa upande wa JMT. Hilo hawataki. Ndio maana watu wanasema msimamo wao ni "changu changu na chako chetu". Ndio maana watu wanajiuliza vitu kama " kwa nini mpemba anaongoza wizara ya ujenzi ? " wanauliza hivi ingawa ni kiongozi mzuri.
Hapo zamani Rais wa Zanzibar alikuwa ndio Makamu wa Kwanza wa Rais na hivyo kuwa mrithi wa kwanza wa Rais wa JMT. Tungekuwa bado na mfumo ule saa hizi Hussein Mwinyi aliyepigiwa kura na wazanzibari peke yao ndio angekuwa Rais wa JMT! Wenye busara wakaona hilo wakabadili mfumo ingawa wenzetu wakaona wamefanyiwa husda.
Kwa kifupi, kama Zanzibar wanataka kuwa na full sovereignty wanapaswa kuchukua hatua za kuvunja Muungano. Kusema vingine ni unafik.

Amandla ...
 
Ndio wanachotaka Zanzibar tuwe kma EU au EAC au Senegambia au Ghana-Guinea ila sio nchi imezwe kabisa Bali masuala ya muungano pekee ndio tushirikiane Kila mtu akiwa na nchi yake.
Kama wanataka tuwe na mahusiano kama EAC basi wachukue hatua wawe kama Kenya na wengine. Hawawezi kuwa hivyo ndani ya JMT. EU, EAC, Senegambia na Ghana Guinea sio nchi kama ilivyo JMT. Kiukweli ni kuwa Zanzibar ina autonomy kuliko nchi nyingi zilizoungana. Nchi kama Scotland, Catalonia n.k. hazina mamlaka ambayo Zanzibar inayo. Wakitaka zaidi ya hayo waliyokuwa nayo watoke katika Muungano. Hiyo sio dhambi. Mbona Czechoslovakia walipeana talaka? Mbona USSR walipeana talaka? Au Yugoslavia? Waseme na kama sote tutaona kuwa tumefika mwisho wa safari tutengane kwa amani. Hapo tutaweza kuwa na uhusiano ndani ya EAC na sio kama nchi moja.

Amandla...
 
Ulisema kwamba Zanzibar haiwezi kuwa na muungano kisa Ina watu wachache. Ndio nkasema nchi kuwa na watu wachache sio issue hata The Gambia ni nchi ndogo kispace na population ila iliwahi kuwa na muungano na Senegal huko nyuma licha ya disparity hiyo.

Na nmesema hata UN The Gambia Ina kura 1 kama ambayo India yenye raia billion 1 Ina kura Moja pekee.
Bila shaka mkuu hapa haukunielewa, nililenga kuwa ikiwa Zanzibar inaidadi ndogo namna ile hatuwezi kwenda kwenye shirikisho lenye equal responsibility na rights kwa member states halafu wakamudu kuendesha serikali lazima wataleta hoja ya wao ni wachache hivyo responsibilities ziwe proportional na idadi yao na mapato yao.


Hii moja kwa moja itavunja hata hayo mahusiano kidogo yatakayokuwepo kipindi hicho.

Kuna mdau pale juu amehoji kama ACT wanaipigania Zanzibar iwe na mamlaka kamili wakati inayo mamlaka kwenye mambo yasiyo ya Muungano mbona hawaipiganii Tanganyika ambayo haina hayo mamlaka hata kidogo waliyonayo Zanzibar ?

Bado narudia hoja yangu ACT wanafanya siasa hadaa au wanapigania kitu wasichokijua mwisho wake.
 
  1. Kushindwa kuboresha Muundo wa Muungano wetu na hatimae ule wa Afrika.
    • Walipounganisha Tanganyika na Zanzibar walidai lengo nikuunganisha AFRIKA.
    • Ukitazama katiba haioneshi ruhusa ya kuongeza nchi nyingine kwenye muungano huu.
    • Wanapo vutana kuhusu Mfumo wa Muungano kurekebishwa ,wanafukuzana kwenye chama.
    • Aboud jumbe kafukzwa,
    • Maalim Seif kafukuzwa,Mzee Hassan Nassor Moyo kafukuzwa
    • Mansour Yusuf Himid Mtoto wa Mwana Mapnduzi kafukuzwa
    • Chupuchupu Amani Karume kufukzwa.
    • Sasa unajiuliza Huu muungani ni kwa maslahi ya Nanai, Mbona Hauendelezwi, Kwa nini Uwe unalindwa Kwa mitutu ya Bunduki na Kulishana Viapo vya Kuulinda?
    • Kulikoni?
    • Au ndio Vile tena aina ya Ukoloni.?
    • LET US BE HONEST

Kuna kaukoloni kwenye huu muungano,ccm kila siku ni muungano wa serikali mbili kuelekea serikali 1,miaka 60 sasa hakuna progress kuelekea serikali moja zaidi tunaona zenji wanajiondoa taratibu,kimasingi suala la muungano hata ccm nao ni underdog tu.
 
ACT Wazalendo , wanazungumzia matakwa ya wazanzibari. Hi kauli mbiu ya Mamlaka kamili ilisha watilisha wengi ndani kwa kuonekana wanahatarisha Muungano.
Lakini ujuwe kuwa Chama cha siasa kina Maono yake na Mtazamo wake wa jinsi ya kuendesha nchi na siasa.
Huu Muungano usiokuwa na DIRA ni wa CCM si wa Chadema wala ACT.
Hata Mfumo wa Uendeshaji nchi wa mikoa ni wa CCM , chadema wao ni Majimbo. na Serikali 3
CCM sera yao ya msingi ni serikali 2 kuelekea 1. LakiniCCM Zanzibar hawaitaki hiyo. hapo ndio utaona kuwa kuna KIJAMBO kimejificha chini ya MUUNGANO.
ndio maana wenye maono tofauti wanataka shirikisho ambalo linaweza likaziunganisha nchi nyingine nyingi tuu.

Ccm no wanazi,wasio taka kubadilika na kuutambua ukweli kwamba huu muungano ni wakihuni.
 
Hivi suala la serkali moja kwanini wengi hawalipigii chapuo! Kwangu naona zanzibar iwe tu mikoa. Serkali moja. Bunge 1. Mahakama 1.
Haiwezekan tumeshafikia maono ya Africa Mashariki kuelekea sarafu 1.
Africa 1.
Alafu bado Tanzania tunajikata vipandepande

Wapemba hawataki hata kusikia serikali moja hapo inabidi mitutu iwalazimishe tu,ccm wanaogopa watapoteza ushawishi ambao kimsingi haupo.
 
Ebu acha vituko , Karume aliposema koti la muungano linambana , unafikiri nani alikuwa na uwezo wa kumuua? Mastermind hapa ni Tanzania bara ndio maana walikuwa tayari kuua nchi yao ya Tanganyika kwa ajili ya muungano

Hakuna nchi ya tanzania bara,kuna tanganyika,kuhusu koti la muungano kubana hata tanganyika wameanza kuuchoka huu uhuni wa muungano.
 
CCM wameufanya huu Muungano kama ndoa ya kikatoliki (kikiristo )mke mmoja, hakuana kuachana.
sasa kweli mfumo umezeeka mno, na wao wenyewe hawezi kuuhimili.
Leo Raisi Mzanzibari Kashika Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Tanganyika Imo ndani,
Watanganyika hawaridhiki ,lakini wanagugumia kichichini.
Wengi wanaona kuwa mambo yanakwenda sivyo kabisa.
Kama Vile Wanaona Zanzibar Inapendelewa sanaa, Kule Zenji wanatawala wenyewe pekeyao,
Kisha huku bara wanachangia na wenzao, ilhali wao wako wengi kuliko zenji.
HII SHIDA KWELI
FUNGUKENI ILI MUELEZE MACHUNGU MUNAYOKABILIANA NAYO
MFUMO HUU SI MWEMA KATU

Kwangu mimi huu ni mfumo wa kihuni
 
Marais tunawachagulia huku Dodoma,
Sheria tunawatungia huku Dodoma,
Hiyo haiwatoshi? Waambie wakae kwa kutulia.
Rais wa Zanzibar hachaguliwi Dodoma. Anaechaguliwa ni mgombea urais kwa upande wa CCM ambao Makao yake Makuu yapo Dodoma. Wanachama wa CCM kutoka Zanzibar wanashiriki kikamilifu katika uteuzi huo. Raia wa Zanzibar ndio wanamchagua Rais wao. Na wanafanya hivyo wakiwa Zanzibar na sio Dodoma.

Amandla....
 
Back
Top Bottom