Ninauelewa uwezo wako mkuu 'zitto junior', ndiyo maana natoa heshima kila mara.
Sasa umetoa jibu linalokaribiana na wanachokitaka Zanzibar. Lakini hata katika mfano huo uliouweka hapo, huo ni muungano wa aina nyingine, tofauti kabisa na Muungano wa "Jamhuri ya Tanzania." Kwa hiyo maana yake hapa ni kwamba tutaanza kuunda muundo mpya kabisa wa muungano wetu.
Labda nia iwe ni kwa wao Zanzibar kuondoka kwenye muungano huu na kuingia kama taifa katika Jumuia yetu ya Afrika Mashariki, ambayo lengo lake ni kutupeleka huko kwenye mfano wa Ushirika wa Ulaya.
Lakini, hata hiyo EU, si unaona hata akina Britain wanajiondoa kwa kuona kwamba kuna mambo yao ambayo hawakuwa na "Mamlaka kamili" walipokuwa ndani ya umoja huo?
Kwa hiyo, sehemu inapojitafutia "Mamlaka Kamili", maana yake ni kwamba inataka iwe na uwezo wa kujiamlia juu ya jambo lolote, bila ya kutegemea tena mamlaka nyingine ifanye uamzi kwa niaba ya wanachama wake.