ACT wameharibu sana, walichojikifanya ni shortsighted kwa kiwango kikubwa sana. Kiufupi wameuza mechi!
Walichokifanya huko Zanzibar, wamejiondolea power za kisiasa walizokuwa nazo na sasa wamebaki debe tupu.
Kwa sasa ACT huko Zanzibar hawana tena uhalali wa kuhoji uchaguzi wa kule au kusimamia hoja zozote za kutaka tume huru ya uchaguzi Zanzibar au hata bara.
Hawawezi kuweka pressure ya ndani ya kutaka waliohusika kuua, kutesa au kuumiza wananchi kwenye uchaguzi uliopita wafikishwe kwenye mkono wa sheria. Wewe unaweza kuishtaki serikali iliyokuteua uingie serikalini?
In short, ACT wameuza political power in exchange ya vyeo viwili vitatu cermonial
ACT wamemhakikishia Hussein Mwinyi miaka mingine 10 kiulainiiii (akiwa hai). Hakuna Mzanzibar yeyote atakayekuwa serious kuwapigia kura watu wasioweza kudai kwa msimamo usioyumba wanachompa. Wataona huu ni ujinga
Cheo walichopewa ni ceremonial, hawana wawakilishi wa kubadili chochote au kuzuia chochote ndani ya baraza la wawakilishi, Kiufupi wamekwenda kulegitimize uchaguzi ule, kumuondolea pressure Hussein Mwinyi na kumpa ahueni JPM kwenye ishu za huko Zenji.
Kiufupi ACT wameipa ahueni kubwa serikali ya CCM dhidi ya kibinyo na joto la ndani la kisiasa.
Nini itakuwa future ya ACT Tanzania bara? - HAIPO, Chadema wamepata mileage kubwa ya kisiasa huku bara kwa kusimama imara dhidi ya "waasi" 19, while ACT imeonekana kama "appeasers".
Nini future ya Zitto kisiasa? - Anaweza kugombea jimbo lolote litakalokuwa wazi, na safari hii kwa sababu yumo kwenye serikali huko Zanzibar watamuacha ashinde na hivyo upo uwezekano wa Zitto kurudi bungeni kabla ya 2025 iwapo kuna jimbo litakuwa wazi kwa sababu zozote zile
Lakini pia ninaona uwezekano wa JPM kumteua ubunge katika zile nafasi 10, hii inaweza kuwa ni charm offensive na kuwagawa wapinzani zaidi na zaidi
Je Zitto atakuwa credible zaidi katika siasa za 2020-2025, La hasha Watu wa bara hawatakiamini chama chake na pia hawatamuamini hata ajaribu kuwaaminisha vipi kuwa yuko kinyume cha matendo na sera za Magufuli na CCM
Kiufupi, ACT ilikuwa imeanza kukubalika huku bara, na ilikuwa inaenda vizuri sana. Lakini kitendo cha kuflip-flop katika kitu cha wazi na cha msingi kabisa kama kukubali kuibgia katika serikali ambayo wao wenyewe walikusanya ushahidi wa wazi wa uharamu wake ikiwemo (kupiga kura mara nyinginyingi kwa baadhi ya watu, Kura zilizoibiwa, Mauaji, Torture(Mateso) ya wananchi), kisha baada ya hapo wanakwenda kusettle kwa vicheo viwili vitatu visivyo na kichwa wala miguu, Ni dhahiri ACT haiwezi tena kupata heshima ya wananchi.
Je future ya ACT hata huko Zanzibar itaendelea kuwa ileile? - La Hasha
Kwa kitendo cha Maalim kuachana na struggle pana ya manufaa ya Zanzibar in exchange ya kupigiwa saluti na kuwa na motorcade, hakuna chochote cha maana kitakachosaidia wazanzibar katika aspiration yao ya kujichomoa kutoka kwenye makucha ya Tanganyika. kwa move hii, Maalim amesaidia zaidi kuifanya Tanganyika iwe confident kwenye kuikalia zanzibar, maana kumbe Tanganyika inaweza kufanya lolore huko Zanzibar ika go away with it. Ikaua, Ikatesa, Ikapora maamuzi ya Wazanzibar kisha ikawaita mezani watu wachache wa huko wakarushiwa tonge kidogo wakatulia
Pia ninaona kuna uwezekano wa Masheikh wa uamsho kuachiwa ili hii iwe ni kama zawadi kwa maalimu ya kumpa political cover kwa usaliti alioufanya dhidi ya masilahi ya watu Wazanzibar ambao humchagua siku zote. Ili maalimu aonyeshe wazanzibar kuwa ni muhimu awemo kwenye hiyo serikali na kumlindia aibu yake hii, Lazima watawaachia masheikh wa uamsho hivi karibuni.
Poleni Wazanzibar, Mliweka imani yenu kwa Seif, lakini Seif siyo Kamanda wa kumaliza kazi, ni kamanda wa kupoa baada ya joto kuwa kimekuwa kali.
Na kingine ninachokiona, ACT sasa itageuka kama CUF ya Maalim na Lipumba wakati ule bado ni maswahiba, Kwamba Lipumba yupo kwa ajili ya kuifanya CUF iwe kwenye daftari la msajili wa vyama lakini nguvu na effort zote ni Zanzibar. Kwamba Lipumba wewe kaa tu uwe mwenyekiti wa kudumu so long as sisi kwetu Wazanzibar mambo yanaenda basi hakuna Shida. Zitto sasa anakwenda kuwa kijakazi na tarishi wa Kambi ya ACT Zanzibar, maana hatakuwa na mtaji wowote wa kisiasa bara!. Nani ataiamini ACT bara kwa hii flip-flop waliyoifanya?
Mwisho wa kisiasa wa Zitto utakuwa ni kuteuliwa na serikali ya CCM kumuingiza serikalini, hii ndo itakuwa exit stratergy yake katika quagmire hii ya kisiasa, naamini system haitomtupa kabisa, kwa sababu ni kijana mueledi, anajua kujenga hoja na ana kipaji cha uongozi. But kukifanya chama chake kikue kama kilivyoanza kuonyesha dalili, Forget about that. Kambi ya Maalim huko Zanzibar imemuondolea kukubalika na kuaminika zaidi mbele ya population ya wananchi huku bara, na nchi nzima kiujumla !