Tetesi: Adaiwa kuficha tani tele za sukari Moshi

Tetesi: Adaiwa kuficha tani tele za sukari Moshi

Yaani utamtuhumu na kumkamata mtu kwa kuhifadhi mali yake? unapaswa kumhukumu kama utapata ushahidi kwamba anauza kwa bei ya juu.... Mkiambiwa mnakurupuka msikasirike bure!
Mkuu wewe nahisi haupo kwenye hii biashara ndio utaona kama bla bla,mimi nina duka la jumla na anaye supply bidhaa kwenye duka langu ni mo,zakaria,bakhresa,sayona(matosun group etc na naletewa bidhaa na hao kupitia mobile truck zao mwezi wa pili sasa wanasema sukari hawana,je kama umeangalia clip ya mhe.rais anavyowahutubia wananchi wa katesh unahisi wanaongelewa walioficha sukari kule mbagala na yule aliyelipia sukari kilombelo ila ataki kuuza kwa wananchi? Unahisi wewe na rais nani anajua mwenendo mzima wa hii ishu? Msipende kupinga kila kitu,rais kaongea vitu sisi wengine tulikuwa atuvijui,sasa katufungua masikio na tunajua wanaomhujumu,eti matajiri wengine wanajigamba kwenye majarida ya forbes,hadi tunaambiwa bilionea kijana wa afrika ukiangalia utajiri wao wakimagumashi,wahujumu uchumi,wakwepaji kodi wakubwa,wazajilishaji na wahuzaji vitu fake....
 
Ndugu wana jukwaa nazidi kuiona hii habari ikishamiri hivyo ningependa kujua ukweli wa jambo hili na je mamlaka za juu zinaweza chukua hatua gani stahiki dhidi ya jambo hili hasa ukiangalia MO ni moja kati ya watu wenye ushawishi mno kwenye jamii na hata serikalini
 
Hawa wafanyabiashara wakubwa ni vizuri kuwa nao makin sana, kama kwel kaficha sukari na ikakamatwa na kutolewa bure, anaweza kuleta crisis nyingine.
 
Kwani ni lazima kuuza? Kama ana mpango wa kuiuza nje ya nchi kwa nini alazimishwe? Mbona Bakhresa anasafirisha unga wa ngano nje ya nchi? Huu ni utawala wa kisheria, enzi za Ujamaa na Kujitegemea zilishazikwa na Azimio la Zanzibar, acheni watu wawe huru kuuza na kununua au kuhifadhi kadri wanavyotaka. Si tumeambiwa kuna shehena inakuja, au nahodha amebadili gia katikati ya bahari?
 
Mkuu wewe nahisi haupo kwenye hii biashara ndio utaona kama bla bla,mimi nina duka la jumla na anaye supply bidhaa kwenye duka langu ni mo,zakaria,bakhresa,sayona(matosun group etc na naletewa bidhaa na hao kupitia mobile truck zao mwezi wa pili sasa wanasema sukari hawana,je kama umeangalia clip ya mhe.rais anavyowahutubia wananchi wa katesh unahisi wanaongelewa walioficha sukari kule mbagala na yule aliyelipia sukari kilombelo ila ataki kuuza kwa wananchi? Unahisi wewe na rais nani anajua mwenendo mzima wa hii ishu? Msipende kupinga kila kitu,rais kaongea vitu sisi wengine tulikuwa atuvijui,sasa katufungua masikio na tunajua wanaomhujumu,eti matajiri wengine wanajigamba kwenye majarida ya forbes,hadi tunaambiwa bilionea kijana wa afrika ukiangalia utajiri wao wakimagumashi,wahujumu uchumi,wakwepaji kodi wakubwa,wazajilishaji na wahuzaji vitu fake....

Wanakuuzia bei kubwa kuliko bei elekezi za serikali?? wao kuwa wauzaji wa sukari pekee wakati huu haliwezi kuwa kosa, kama wanafanya hivyo kihahali. Kama wanakuuzia bei ya juu hiyo ndiyo issue tunayotaka kusikia sisi wengine. Hatupo hapa kumtetea mtu yeyote kwani na sisi ni wananchi wa kawaida, lakini pia ni dhambi kuwatuhumu watu bila kuwa na ushahidi wa makosa waliyoyafanya.
 
Haki za huyu mwananchi zizingatiwe katika kuutafuta ukweli, tusije tukamgeuza Mbuzi wa Kafara wakati yeye keshatumia pesa nyingi sana kuumiliki huo mzigo!
Unajua maana ya uhujumu uchumi...!? Unapotengeneze supply ama demand ili kuwaumiza wengine kwenye biashara hiyo ni fraud...mdogo wangu...! Wenzetu wanalikemea sana hilo....!
 
biashara na uongozi ni vitu vi wili tofauti kwa hiyo baadae mtawakamata walio hifadhi mazao kwa ajili ya kuuza kipindi cha masika kuwa wanahujumu Uchumi..Wanao hujumu Uchumi ni Eppa..Escrow..Stanbic bank scandal..rada scandal msitoke katika mada na kukimbia kutafuta viji ishu ambavyo sio..
 
Wanakuuzia bei kubwa kuliko bei elekezi za serikali?? wao kuwa wauzaji wa sukari pekee wakati huu haliwezi kuwa kosa, kama wanafanya hivyo kihahali. Kama wanakuuzia bei ya juu hiyo ndiyo issue tunayotaka kusikia sisi wengine. Hatupo hapa kumtetea mtu yeyote kwani na sisi ni wananchi wa kawaida, lakini pia ni dhambi kuwatuhumu watu bila kuwa na ushahidi wa makosa waliyoyafanya.
Mkuu sio wanauza bei kubwa la hasha,wanasema hawana sukari kabisa mwezi wa pili sasa,wananishushia ngano,mafuta ya kula na bidhaa nyingine,sasa nilivyoona clip ya mhe rais anahutubia uko katesh nimegundua wanahujumu hao wanitwa superdealers,kama ujaangalia clip naomba uhitafute ipo umu umu rais alivyokuwa anaongelea suala la sukari
 
Mwenye mabus ya RATCO nahisi kama anaweza kuisaidia polis kwenye hili ,lakini let time be the judge msije mkanifunga bure
 
tokea hili sakata la uhaba wa sukari litokee, wengi wana jadili kisiasa na sio kitaalamu.

na kama suluhisho likiwa kisiasa halitokidhi kwa wkt wote.
 
MO ni kawaida yake hiyo,haiwezekani mtu awe dealer wa kilombero,tpc halafu huyo huyo ndiye awe anapewa vibali vya kuingiza sukari nchini.Tunajua ccm wakiishiwa huwa ndiye anayeokoa jahazi kwa makubaliano ya sukari
Mtawasingizia sana wafanya biashara badala ya kusema ukweli kuwa viwanda vyetu vya sukari havizalishi sukari ya kukidhi soko la ndani ya nchi. Tuwe wakweli. Pamoja na kuwa na nia nzuri ya kuvulinda vuwanda vyetu, tulikurupuka kuzuia sukari toka nje, serikali makini ingefanya logistic kujua tunazalisha kiasi gani na tunakuwa na upungufu kiasi gani.

Sehemu inayopungua katika hilo, serikali ingetoa vibali kuingiza sukari ili kutosheleza mahitaji.

Hili lingeendelea gradually mpaka pale tutakapokuwa na uwezo wa kulisha sukari kutosha ndani ya nchi ndipo ipige marufuku uingizaji toka nje.
 
tokea hili sakata la uhaba wa sukari litokee, wengi wana jadili kisiasa na sio kitaalamu.

na kama suluhisho likiwa kisiasa halitokidhi kwa wkt wote.
Sana mkuu,na hii mkuu angalia clip ya mhe rais anahutubia wananchi katesh utaona ili suala la shortage ya sukari,lakutengenezwa kabisa
 
Wakati joto la bei ya sukari ikiendelea kuwa juu na wakati kiwanda cha TPC moshi kikiwa kimefungwa km ilivyo utaratibu wake wa kila mwaka kukarabati mitambo yake, inadaiwa tajiri mkubw hapa nchini alifanya kazi ya ziada kukusanya tani za kutosha toka kiwandani hapo na kuzifungia kwenye gowodn zake Moshi.

Hali ya upatikanaji wa sukari imekuwa tata sana na kwa sasa supedealer pekee anayeuza sukari kwa hapa Moshi ni mbunge wa Moshi mjini kupitia Chadema, superdealer wengine akiwepo huyu tajiri aliyesomba tani za kueleweka kazifungia....

Na huyu tajiri ni kada wa ccm na amewahi kuwa mbunge kanda ya kati pale. So mjue tu kuwa Magufuli anahujumiwa kwa speed ya hatari hapa na sisi wananchi tukiona cha moto huku chini....

Si wajua ule usemi kuwa mafahali wakipigana nyasi huumia?

Ndo hayo!

Kazikwetu
Na leo hapa Dar, nimenunua mimi mwenyewe 2400,kutoka ile 2000 tuliyoizoea ya zamani kwa packet
 
Mkuu sio wanauza bei kubwa la hasha,wanasema hawana sukari kabisa mwezi wa pili sasa,wananishushia ngano,mafuta ya kula na bidhaa nyingine,sasa nilivyoona clip ya mhe rais anahutubia uko katesh nimegundua wanahujumu hao wanitwa superdealers,kama ujaangalia clip naomba uhitafute ipo umu umu rais alivyokuwa anaongelea suala la sukari

NImekuelewa Mkuu. Lakini napata shida sana kuamini kwamba mtu anaweza kuwa mhujumu kwa kuweka bidhaa yake kwenye ghala..... ukimpeleka mahakamani utamshitaki kwa kosa gani?
 
Na leo hapa Dar, nimenunua mimi mwenyewe 2400,kutoka ile 2000 tuliyoizoea ya zamani kwa packet

bei elekezi ni tsh. 1800 kwa mujibu wa waziri, labda tusubiri bei elekezi mpya?! aache ukmya.
 
Umeona eee mkuu!!!? Wanatafuta namna ya kumvisha nguo mfalume baada ya kubakia mtupu. Maamuzi mkurupuko yanatia chachu kwenye utendaji uliotibuka wa mfalume.

QUOTE="_Iramba, post: 16105588, member: 359488"]naona mbuzi wa kafara wanatafutwa kwa udi na uvumba hili,kumfichia aibu na kuutua mzigo wa utendaji mbovu wa magufuli kwenda kwa wafanya biashara,ahahaha!
mbuzi wa sadaka wakiisha si mtatoana wenyewe kwa wenyewe nyie watu!
ahahaha[/QUOTE]
 
NImekuelewa Mkuu. Lakini napata shida sana kuamini kwamba mtu anaweza kuwa mhujumu kwa kuweka bidhaa yake kwenye ghala..... ukimpeleka mahakamani utamshitaki kwa kosa gani?
Mkuu kwenye suala la sheria sijui linatekelezeka vipi? nashindwa kujadili kisheria
 
Back
Top Bottom