Uchaguzi 2020 Adam Mchomvu ampiga mtama Emmanuel Mbasha stejini kwenye tamasha la CCM uwanja wa Uhuru

Hiki ndicho kinachotuuma wanaccm. Kwamba aliyepiga hajavaa hata nembo ya CCM na aliyepigwa katupia full CCM.

Mbaya zaidi aliyepiga alikiri hadharani kuwa hakumpigia Rais Magufuli kura mwaka 2015. Inauma sana jamani. Yani tukifungua kila "engo" tunakutana tu na topics za mitama!

Yani tumelipa Tshs milioni 800! Mapato yote yaliyokusanywa kutoka kwa watia nia tumeenda kutupa pale taifa kisha jamaa anachukua points tatu na magoli yote 200! Hapana!

VUTA-NKUVUTE ameanza kutuonya sasa matokeo twayaona.

Any way: CCM hatuhitaji mdahalo kwenye bwalo lisilo na kileo wala mlo. Huo ni Utamaduni wa ndani toka tukiwa jandoni!
 
Alivyorukiwa ule mtama niliona visuti vya kijani vinapepesuka hadi chini.
Yule msela hataki mazoea ya kike.
 
Mchomvu ana wazazi na watu wanaoheshimiana ambao hawaamini kama anavita bangi sasa kumwambia ivyo ni jau hata mimi nakukata.
Mbona huo ni msemo wa kawaida tu anapaniki bure
 
Usisahau pia aliyepiga aliomba msamaha na kusema angekuwa na uwezo angewashawishi wananchi kumchangia Magufuli pesa za vacation.

Akajikalie huko yeye ampigie kampeni tu akija endelee na kazi yake.
 
ccm ni laana hakuna jambo wakafanya na wakamaliza vizuri
 


Nahisi Adam watu walivyomshangilia aliona kama kamaliza hivi kumbe ni tatizo cmg hawawezi kukubali, ccm hatakubali na tcra hawatakubali kifupi nilisema tangu jana Adam itamhalibia big time mwenzake Mbasha kwenye hilo suala hana cha kupoteza ,Nivizuri kuzuia hasira zetu
 
Usisahau pia aliyepiga aliomba msamaha na kusema angekuwa na uwezo angewashawishi wananchi kumchangia Magufuli pesa za vacation.

Akajikalie huko yeye ampigie kampeni tu akija endelee na kazi yake.
Hayo ni maneno tu, ila mtu kulambwa buyu hadharani na mikofia yake ya kijani ni udharilishaji uliotukuka..

Nasikia asubuhi hii kaonekana pale MOI anapelekwa kwenye MRI kuona kama kifundo cha mguu na ugoko kama viko sawa..
 
Mbona mwenyekiti wetu wa chama cha kijani alibariki kipigo cha Mbasha kwa moyo wote.
 
Tuiangalie kwa namna nyingine.

Ingekuwa Chadema kwa ile nyomi tayari wangetangaza wameshashinda uchaguzi.

Na kelele humu zingekuwa nyingi saana.
Hili naloo nyomi ya wasanii Mia mbili. Yani upeleke wasanii 200 uwanjani halafu ujisifie na ile nyomi! Aisee wengi mnastahili mitama
 
Mimi wala sina shida na kujaza. Maana kwa Tanzania tuna watu takribani milioni 60.

Hata ukijaza watu elfu 1000 haina maana ndiyo umeshinda uchaguzi.

Nimeongeza hilo kama moja ya tafakuri kama jana ingekuwa CHADEMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…