Uchaguzi 2020 Adam Mchomvu ampiga mtama Emmanuel Mbasha stejini kwenye tamasha la CCM uwanja wa Uhuru

Uchaguzi 2020 Adam Mchomvu ampiga mtama Emmanuel Mbasha stejini kwenye tamasha la CCM uwanja wa Uhuru

Chama cha mapinduzi kupitia katibu wake wa uenezi, Ndugu H. Pole pole wameandaa tukio lililowakutanisha wadau mbalimbali wa burudani wakiwemo wasanii wa maigizo, muziki n.k. Waliloliita #UhuruKunaJambo linalofanyika katika uwanja wa uhuru.

Katika tukio hilo kuna tukio lingine limetokea, ambapo mtangazaji wa Clouds Fm pamoja na msanii Mbasha wamevutana mashati.

Tukio lilianza baada ya Mbasha kutumbuiza na kuwauliza mashabiki kuwa aendelee ama ashuke? Mashabiki wakasikika wakisisitiza kuwa ashuke lakini Mbasha akamwambia Adam kuwa wanasema aendelee. Kisha akaongezea kwa kusema "tatizo wewe Adamu bangi sana" maneno yale yalionyesha moja kwa moja hayakumpendeza Adamu maana hata Mbasha alivyokuwa anataka kumkumbatia, alimkwepa na kumputa mikono.

Adam akawa amesogea kwa pembeni kiasi, Mbasha akawa bado anang'ang'ania kubaki kwenye stage ndipo Adam akamkata ngwara na Mbasha kudondoka.

Wengi wamelitazama katika namna tofauti tukio hili. Wengine wakisema Mbasha amemkosea Adam kwa kusema kuwa Adam anavuta bangi tena mbele ya hadhira. Ni kumkosea, na anaweza kumfanya Adam kuwekwa chini na kuchunguzwa maana vyombo vya ulinzi na usalama vipo pale.

Baadhi wanamlaumu Adam kwa kumdhalilisha mwenzie mbele ya umati kwa kumkata ngwara, wanasema angesubiri wayazungumze wakiwa nyuma ya stage.

Wewe unalionaje hili?
Mchovu yupo right maana Mbasha alijiona kwenye hamna .
 
Mi naona wenye makosa ni walioanza kampeni kabla ya wakati... (lakini nikiwaza naona kwamba huenda hawa jamaa kampeni hazikuwahi kuisha wamekuwa wakifanya kwa miaka mitano)
 
Huyo Mbasha!!!! Alikuwa amekunywa au kavuta nini kabla!!.. duh!!!

Anataja Bangi.. kwa mkusanyiko kama huo.. akitaka waongelee bangi anayoijua yeye na matumizi yake au?

Shame on him
Adam amemvumilia sana mbasha. Mbasha hajielewi, nadhani ndio maana flora aliondoka. Nimekwazika sana mbasha kung'ang'ania mic na kulazimisha aimbe wimbo hata haueleweki. Harafu kumkumbatia mwanaume mwenzie jukwaani.
 
Hata me ninge mpaisha "Adam tatizo wew bangi sana" 😡 mbele ya umati and on-air
 
Nimecheeka saana. Sijui mchomvu kawaza nini kumsambua ngwala Mbasha mbele ya Magufuli. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nasikia tatizo lilianzia pale mbasha alipotaka kumfanyia mchomvu matendo yanayolandana na jina lake ndipo mchomvu akaona aikijilegeza bwana mbasha atatimiza adhma yake kuilaini.Mtama aliokula bwana mbasha nasikia hata mapepo yaliyokuwa ndani yake yalitimkia kusikojulikana
 
Huyo mbasha kawaida yake kuropoka ropoka ninge kuwa hapo ninge muongezea
 
@Mshana Jr wewe mtu akisema “tatizo wewe mchawi sana” utachukua hatua gani?!
 
Huyu mbasha alimuambia adamu unajua wewe ni bangi Sana
 
Izi mada zinngine tuwaachie vijana wa lumumba .sisi atu waingilii kwenye Mambo yenu
Hili halina upande mzee. Na mimi wala sijaleta nikasema nimesimama katika upande. Kazi yangu ni kukupa taarifa na kuzichakata kwa pamoja. Tusifanye vitu kwa ushabiki.
 
Back
Top Bottom