Adam na Hawa walikuwa wawili hapo kale?

Inawezekana wewe una reference zaidi ya Biblia au Quran, please kama una sources zingine ungeziweka hapa ili usiwe umetutega kitendawili, au unataka tukupe mji ili utegue?
Mimi ninachoelewa kupitia "Biblia Takatifu" hakuna kilichofanyika kabla au bila yeye "Mungu", uwe ulimwengu au vilivyomo "wanadamu ama chochote kile
 
Kwa leo tuiite "human Evolution "

kuna phase ya human revolution yeyote ipo in progress huko msituni?
Ushahidi mkuu hata sehemu moja ...isiwe kitandani please
 

pia mungu ndiye aliyemteua adam katika wengi amjue mung lakini angeweza kumchagu hata mtu mwingine mkuu
ukisoma vibaya utatafsiri vingine
 
watu wengi tu walikua wakwanza
Mkuu how can your thinking be like this? Sasa kama wengi walikua wa kwanza inamaana walitokea kwa pamoja? yani kwa kusema hivo unamaanisha mwanzo wa kitu hua hamna, hata simu zilivotengenezwa kulikua na ya kwanza nyingine zikafatia.. hahaha duh ati wengi walikua wa kwanza, hahaha! hii kali. Kwa hiyo kwenu wewe pamoja na wenzako wote mlikua wa kwanza? hata mapacha kuna anayetangulia, hahaha! umetisha mzee
 
Hakuna kitu kama hicho, hakuna summary hio na hakuna contradictions yyoyote katika Biblia,labda kama unasoma Biblia kwa matakwa yako

kulikua na watu sema lengo hapo ni kiroho i mean mtu atakaye mkubali mungu.
Unaijua roho ndugu ?
Kama adam alikuepo kwanini alipuliziwa roho ..
Fikiri
hakuna mtu "binadamu" asiyekuwa wa kiroho, sisi wote ni wa kiroho kwa Mungu huyo huyo aliyemuumba Adamu, hata wewe ni wa kiroho

watu wengi tu walikua wakwanza

please hoja zenu zipo ok, ila tatizo imetumika hoja ya nguvu ila si nguvu ya hoja, jaribuni kuleta reference ili tuamini kuwa kulikuwa na watu wengine kabla ya Adamu tumalize ubishi ila kwa Biblia Takatifu au Quran Takatifu(hiki kitabu sikifahamu sana), bado mtaonekana mnalazimisha hoja yetu kuwa kulikuwa na watu "binadamu" kabla ya Adamu
 
pia mungu ndiye aliyemteua adam katika wengi amjue mung lakini angeweza kumchagu hata mtu mwingine mkuu
ukisoma vibaya utatafsiri vingine

Sasa utachanganyikiwa "Mungu si mwanasiasa huwa hateui ila analeta/ kutoa, Mungu hakumteua Adamu isipokuwa alimuumba,lete reference ya hayo unayosema
 
kuna kitu hapa kinanitatiza.Tunaamini kuwa Mungu hakosei na anajua kabla halijatojea. sasa inawezekanaje Mungu aruhusu kitu halafu baadae akikataze. inamaana tunakiri kakosea? mnaposema zamani ilikuwa ruksa kumlala dada yako halafu then kipindi cha mussa. Mungu huyo akataze? kulitokea nini mpk akataze? so mimi nitarudi tu kwa wanaoamini kuwa duniani kulikuwa na wengi sema adamu alikuwa chaguo lake katii yao km ambavyo alichagua manabii kati yetu. kwasababu Mungu sio bunge la tanzania linalopitisha rushwa"takrima"halafu baadae linakiri lilikosea eti ilikuwa rushwa. MUNGU H AKOSEI.
 
unajua maana ya wote walio hai ? Usitafsiri juu juu mkuu utapotoka bure

Huenda nikawa sijui, ila kwa kadri ya maelezo ya biblia takatifu yanavyosema, Adam anabaki kuwa binadamu wa kwanza.
Kama unamaana nyingine ya wote walio hai si uiweke hapa tukuelewe?

mkuu hayo yapo point ni kuwa kulikuwa na watu wengine pia!

Hiyo point ni kwa mujibu au kwa kurejea wapi? mbona mimi nakuja na mistari ya biblia hata kama hauuamini ukweli wake, nataka na wewe uniambie maana ya wote waliohai na kwamba kulikua na watu wengine kama unavyodai njoo na reference!
 
Sasa utachanganyikiwa "Mungu si mwanasiasa huwa hateui ila analeta/ kutoa, Mungu hakumteua Adamu isipokuwa alimuumba,lete reference ya hayo unayosema

unavyodhani alimuumba kivipi?

Kutoka katika vitabu :alimteua kiroho na kumpa ufunuo wa kujua vitu na kumjua mungu
 
Biblia inatakiwa kuitazama kiroho, makosa ya kibinadamu yapo mengi, yaliyofanywa kupunguza ukweli unao kingana na theolojia tulizonazo. Hii imeanza kwa mstari wa kwanza wa biblia neno mbingu "heavens" linabadilishana na "heaven" kuziba pengo la kiimani. Hivyo si ajabu kwa hali hiyo kufanyika kwa mwanzo wa binadamu kulinda imani pia.
 
wakuu mie napingana sana na ukweli huu kwani ni UONGO mtupu kwani hawa jamaa ni watu katika watu!
Je UNAMJUA BINADAMU WA KWANZA HAPA DUNIANI! TAFADHALI FUNGUKA!
Samahani Scatter, Tuanzie hapa kwanza " Yai au kifaranga " kipi cha kwanza?
Halafu usisahau kuna kitu chaitwa Baraka (Blessings).....!
 
mimi hapa "sidhani"

unarudia swali lako lile lile, nilikuambia kuwa usome kitabu cha Mwanzo 1:1-31, wewe umekataa na kukimbilia kujibu hoja bila majibu, tunakuomba utupe reference hautaki, sijui na siye tudhani bila reference!
unavyodhani alimuumba kivipi?

Kutoka katika vitabu :alimteua kiroho na kumpa ufunuo wa kujua vitu na kumjua mungu
 

tuambie unachoamini wewe na kwa nini uaamini hivyo na chanzo cha hicho unachokiamini
 
utaumia bure,scatter hana reference anatumia msuri tu
 
Nakubaliana na wewe kuwa Mungu hakosei na hata kosea hata mara moja, Na Mungu si kigeu geu, na "Mungu si Athumani". Tatizo letu tunataka tumfahamu Mungu kwa hali ya kidunia dunia na ki-ubinadamu
 

mkuu ukisoma vitabu vyote mfano bible mwanzo 2:6 mpaka 2:9 unaelezea philosophy viumbe kuumbwa na ukienda pale mlango wa pili 2:5 unazungumzia mtu wa kwanza kupewa roho ya kumuamini mungu kumbuka tayari keishaumba viumbe ke na me katika nchi
 
tuambie unachoamini wewe na kwa nini uaamini hivyo na chanzo cha hicho unachokiamini

mfano ukisoma bible mwanzo mungu amepambanua kila kitu..
Mwanzo aliumba uhai then akaleta roho
 

natumia kimoja kwa sasa:
rejea bible mlango wa kwanza;
2;5 mungu akaijaza nchi viumbe hai kwa jinsi yake, wanyama wa mwituni na watambao
swali kwako
unajua maana viumbe hai??
Hapo hapo mwanzo
mlango wapili ukisoma tena utakutana mungu anasema akampulizia roho adam ili akaitawale dunia na vilivyomo ukisoma zaidi utaambiwa alipeleka kuishi bustani ya eden
swali
unajua maana ya kupuliziwa roho?



Viumbe hai vilikuepo tangu kale ila roho ya kumjua mungu haikuepo hapo kabla ilikuja baada ya kumteua adam aitangaze
so kulikuwa na watu wengi toka kale na ADAM SIO MTU WA KWANZA DUNIANI ILA NI MIONGONI MWA MAUDONGO YALIYOPEWA ROHO YA KUMJUA MUNGU
 
Da kaaaaaz kwelikweli kama msingi wako ndio huu manake hata nikichukua hii shule sijui nitamwelezea nani anielewe. Adamu aliishi duniani physically na alikula tunda physically na alitolewa nje ya bustani physically na ardhi ililaaniwa physically; tumepokea kifo na laana toka kwake. Sasa jamaa yangu unaposema waliokula tunda ni watu kibaaaao na walioleta kifo ni watu kibaaaao na waliotolewa ubavu kuumba mwanamke ni watu kibaaaao mbona inakuwa shida sana rafiki yangu? mwanamke ana mbavu 18 na mwanaume mbavu 17 mmoja ukiwa umetolewa kumuumba Hawa sasa unaposema waliumbwa kibao tangu mwanzo ni yupi sasa mmoja wao ubavu ulitolewa na hao kibao mbavu yao mojamoja iliyeyuka saa ngapi na kwenda kufanya nini? maandiko yanasema Adam alikuwa peke yake kwa maelfu ya miaka kabla ya kuumbwa mwanamke wewe unakuja na elimu mpya isiyo hata na mizizi mbona hili ni balaa kubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…