Adam na Hawa walikuwa wawili hapo kale?

Adam na Hawa walikuwa wawili hapo kale?

Kusema kweli bado inanishangaza na itaendelea kunishangaza kama hadi leoo hii tunapozungumza haya mambo ni mwaka 2016, mwezi wa tatu tarehe 6,eti bado kuna waafrika wanaamini hadithi za kwenye biblia kuwa Adamu ndio mtu wa kwanza kuumbwa?kweli hii minyororo ya utumwa iliyofungwa kwenye akili zetu ni mikali aiseee....khaaaa.....hivi waafrika ni lini mtaamka na kufunguka kwa akili zenu??
 
Umesema unapingana na ukweli.
bac sawa,ndelea kupingana nao mpaka ukue unaonyesha bado mtoto
 
Kusema kweli bado inanishangaza na itaendelea kunishangaza kama hadi leoo hii tunapozungumza haya mambo ni mwaka 2016, mwezi wa tatu tarehe 6,eti bado kuna waafrika wanaamini hadithi za kwenye biblia kuwa Adamu ndio mtu wa kwanza kuumbwa?kweli hii minyororo ya utumwa iliyofungwa kwenye akili zetu ni mikali aiseee....khaaaa.....hivi waafrika ni lini mtaamka na kufunguka kwa akili zenu??

Mbona unawatukana waafrika bila sababu? kwani kuamini maandiko matakatifu ni utumwa? mbona waarabu/waislam nao wanaamini kuwa nabii adam ni binadamu wa kwanza? hata hao wazungu waliobobea katika science wanaamini maandiko matakatifu? Heshimu imani za watu
 
Ukiwa mdadisi sana unaweza umiza kichwa, mfano, mwanzo alikuwapo Adam tu kisha akaja Hawa, wakazaa watoto 2 Abel na Cain, Abel akauliwa na Cain! Baada ya hapo Cain nae akapata watoto! Sasa KAMA HAKUMLALA mama yake, maana yake kulikuwa na mwanamke mwingine mbali na Hawa! Hivyo walikuwapo watu kabla ya hapo.
 
Kwa kutumia mfano wa chakula kilichofunikwa kwenye hotpot na kuzaa funza tunapata majibu kuwa ardhi ilizaa viumbe vyote, ndio maana viumbe vyote vikifa vinakuwa mbolea neans vinarudi kwenye asili yao, hata dini inasema kwa kutufumba kuwa tumeumbwa kwa udongo na ndio reality kuwa we come from the land
 
Yes mkuu,Adam na hawa walikua binadamu Wa kwanza lakini biblia inasema walikua na watoto Wa kiume Cain and Abel lakin ukweli ni kwamba walikua pia na daughters..
 
unajua nini watu wananitolea mapovu ila katika kuelimishana adam alikuwa ni mwa watu waliokuwa wakiishi baada ya mungu kuotesha viumbe dunianin

kwa mtazamo wangu jamaa alikuwa mteule katika wale watu wengi waliokuwepo pale katika lile eneo

Mwanzo 4
15. Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.

16. Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.

17. Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe.


Ukisoma hiyo mistari inaonyesha wazi kulikuwa na watu wengine. Maana Adam na Hawa walimzaa Kaini na Abel, Kaini anakamuua Abel. Tunaambiwa kwenye huo mstari wa 15, Mungu anasema mtu yeyote atakaye muua Kaini atalipizwa mara saba na akamtia alama mtu yeyote amuonaye asije kumdhuru. Mtu gani mwingine sasa? Je ni Adam na hawa?

Katika mstari wa 16 tunaambia akaenda na kukaa nchi ya Nodi na mstari wa 17 tunaambiwa akamjua mkewe ikiwa ina maana alipata mke huko, je mke alimtoa wapi?
 
Ukiwa mdadisi sana unaweza umiza kichwa, mfano, mwanzo alikuwapo Adam tu kisha akaja Hawa, wakazaa watoto 2 Abel na Cain, Abel akauliwa na Cain! Baada ya hapo Cain nae akapata watoto! Sasa KAMA HAKUMLALA mama yake, maana yake kulikuwa na mwanamke mwingine mbali na Hawa! Hivyo walikuwapo watu kabla ya hapo.

Taratibu....! Kwani uliambiwa Adamu hakuwa na watoto wengine wa kike? Na unajua ni miaka mingapi ilipita tangu Kaini amuue Habili hadi kupata mtoto?

Issue hizi msizozijua sio za kuingia kichwakichwa bila tafakuri ya kina na kuja na majibu yenu tayari tena ya kitoto.
Unadhani kama lengo lingekuwa kudanganya wangeshindwa kupanga uongo ili watu wapuuzi washindwe
 
walikuwa watt kibao tu sema vibabu mashekhe na mapdri wanatudanganya hawachambui vizuri
Mkuu kama unategemea watu wengine wasome waje wakuchambulie unavyotaka wewe pole sana,vitabu vipo soma mwenyewe.Uzembe wa watu kusoma neno la Mungu umewafanya wadanganywe na wamwache Mungu,kuna vita shetani hajalala.Kama unataka kuiponya nafsi yako jibidiishe kujifunza neno la Mungu,viongozi wapo kukuongoza lakini na wao ni wanadamu wanaweza kukosea sasa kama wewe hujui,hata wakikosea huwezi jua kama wamekosea.
 
Kulikuwa na watu jamii ya majini walio salia awali ktk kuangamizwa hao majn na jamii hiyo ndo aliko elekea kaini na kuchangamana nao then aliowa jamii hiyohiyo na ndo chanzo cha gadhabu ya mungu baada ya kizazi cha thethi mtoto wa 3 kwa adamu kuowa ktk kizazi kile cha majitu yaani uzao wa kaini.
 
Habarini jamani!
Kwanza nianze kwa kusema kuwa Adam Na hawa hawakuwa watu kama Mimi Na wewe kwa maana ya kuwa Na miili ya nyama.adam humaanisha nguvu ya kiume iliopo kwenye mwili wa binadamu na hawa umaanisha nguvu ya kike iliopo kwenye mwili wa binadamu ambazo hutumika katika uumbaji.nguvu ya kiume hutumika katika kuumba na nguvu ya kike katika kuzalisha.
Naomba niishie hapo.
 
Adam na Hawa walikua wana mwili wenye miguu na mikono kama wewe na Mimi,lakin walikua wana Anna ya mwili usiokufa (immortal body), ambao mwili kifupi ni mwili usio na damu as a life giving substance ndo mana wangeweza kushi milele na milele,mwili ambao hawakua wanasikia maumivu,na nakuunga mkono by then ule mwili( immortal body) ulikua na systems zote za mwili kama mfumo Wa damu,Mbegu za kiume,na mifumo mingine lakini haikua active ila baada ya anguko LA adam na hawa ndipo ile mifumo ndani ya miili yao ikawa activated.
Ndo kusema immortal bodies ya adam na hawa ikabadilika na kua 'mortal now ikawa subjected na pains na physical death.
 
Kingine hapo ni level ya utashi na Akili kwa kipindi cha adam na hawa,walikua in a state of "innocence" hawakujua kipi kizuri sababu hawakujua kipi kibaya.
Walikua kama watoto wadogo kiakili ndo mana walikua uchi lakini hawakujitambua.
Ndo mana walichagua kile kilichokatazwa wakaacha kile kizuri just because by then hawakujua kizuri na kibaya .
Maisha yalikua ya raha ndani ya bustani ya eden.lakini baada ya anguko kutokea ndio wakawa wanajua kizuri na kibaya na hata wakajua kwamba wako uchi na wanahitaji kujifunika miili yao.na hata wakaanza ku-make babies(kuzaa)
So kuna tofauti kubwa ya state of mind ya adam na hawa kabla na baada ya anguko.
 
Aisee! kupitia wachangiaj wa mada hapa naanza kuunganisha vitu kuhusu habari za mwanamke "Lilith".
ambaye nmewahi sikia ni wife of satan pia huwakilishwa na alama ya bundi /owl.
sema nlikua cjui kuwa ndo alikua mke wa Adam before Eva. So it mean if it is real satan exist, kajimilikisha Lilith !!. tena ina maana Lilith hajafa had leo b'cause hakula tunda!?!
emu mwenye chanzo Cha habari za Lilith anipe b'cause Bible Haijaeleza. (sichagui nasoma elimu zote)
Mkuu hats mm hii elimu na itaka sana. Niliwahi kuckia vtabu vya kiyahudi ndo vmemuelezea sana huyu mwanamke mwenye elimu hii atupatia zaid. Nawasilisha
 
Wacha kunisingizia wewe, Mimi sijafikia bado level ya u-mungu
Mkuu usijidharau,ni ii inasababisa setani anatesa watu kwa sababu wanadamu awajui wanauwezo mkubwa kiasi gani.Shetani anachofanya anawapa vitu vinavyoonekana kwa macho ya nyama kama majumba na magari kisa anawaibia vile vya thamani visivyoonekana kwa macho ya nyama.Biblia imesema sisi ni miungu,na kwani mkuu hujui kama Mungu ametuumba kwa mfano wake?
 
Mkuu usijidharau,ni ii inasababisa setani anatesa watu kwa sababu wanadamu awajui wanauwezo mkubwa kiasi gani. Shetani anachofanya anawapa vitu vinavyoonekana kwa macho ya nyama kama majumba na magari kisa anawaibia vile vya thamani visivyoonekana kwa macho ya nyama. Biblia imesema sisi ni miungu, na kwani mkuu hujui kama Mungu ametuumba kwa mfano wake?

Bismillah Rahmaan Rahiiym,
1- Qul Huw-Allahu Ahad
2 - Allah-us-Samad
3 - Lam yalid wl lam yulad
4 - Wa lam yakul lahu kufuwan ahad

In the name of Allah, the Most Beneficent, the Most Merciful.
1 - Say: He is Allah, the One!
2 - Allah, the eternally Besought of all!
3 - He begetteth not nor was begotten.
4 - And there is none comparable unto Him.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehem.
1- Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja tu.
2- Mwenyezi Mungu tu ndiye anayestahiki kukusudiwa.
3- Hakuzaa wala Hakuzaliwa
4- Wala hana anayefanana Naye hata mmoja
 
Mmmh! naona tunaanza kuhoji uumbaji wa Mungu. tunaweza kuhoji baada ya kifo ni wapi. kama hatuamini kuhusu uumbaji, tujiulize huu ulimwengu ulikuwa wapi, kwa nini kuna ulimwengu, kwa nini tunaishi na mambo kadha wa kadha. Nadhani wakati mwingine tunapaswa kuyakubali mapokeo kwa sababu kama ambavyo hatujui imekuwaje ulimwengu ukawepo na baada ya kifo ni nini, basi tukubali kwamba Adam na Hawa ndio watu wa kwanza kuumbwa.

wakuu mie napingana sana na ukweli huu kwani ni UONGO mtupu kwani hawa jamaa ni watu katika watu!
Je UNAMJUA BINADAMU WA KWANZA HAPA DUNIANI! TAFADHALI FUNGUKA!
 
Back
Top Bottom