Addis Ababa itakuja kuwa kama Dubai miaka 20 ijayo, sio kwa ujenzi huu aisee

Addis Ababa itakuja kuwa kama Dubai miaka 20 ijayo, sio kwa ujenzi huu aisee

Pamoja na Maendeleo makubwa waliyonayo.
Human exposure ni ndogo kulinganisha na nchi kama kenya au Tanzania.

Tanzania kwa exposure hasa kizazi cha vijana kiko juu mno. Wanakosa tu kiongozi wa kuwapush.
Ethiopia wana kází kubwa ya kufanya kwenye human capital
Haa wapi hii hoja yako ya kuhusu exposure ninakukatalia mpaka kesho, hao jamaa wana exposure ya kufa mtu huwezi kabisa kuwalinganisha na nchi yoyote hapa Afrika mashariki.

Baada ya Nigeria nchi ya kiafrika inayofuatia kuwa na diaspora kubwa huko duniani ni Ethiopia.... wale ni global citizens wako mpaka kwenye vinchi vya central Asia kama Azerbaijan na Uzbekistan huko nchi ambazo huwezi kumkuta mbongo au mkenya.

Hili la kutokuwa na umoja nafikiri linaweza kuwa linachangiwa sana na tawala za kitamadunu ambazo zilikaa Ethiopia kwa muda mrefu sana huku kila jamii ikijiona ni bora kuliko wenzake.
 
Asili ya migogoro ya kikabila kwa nchi kama Ethiopia na Nigeria ni zile tawala za kifalme za zamani
Utawala wa Abyssynia ulikuwa wa kabila la Amhara licha ya kuwa na makabila mengine makubwa ilibi yafuate utawala huo na baadaye jeshi lilikua wengi kutoka Tigray
Hii mipaka iliyowekwa na wakoloni na kulazimisha baadhi ya makabila kuwa sehemu ya nchi moja ikasababisha migogoro ya ardhi na rasilimali nyingine
Kuan makabila hayakutaka kuwa chini y utawala wa makabila mengine tangu zamani ila mipaka ya kikoloni hata kama hawakutawaliwa ilibidi waifuate
Makabila makubwa kwa Ethiopia ni Oromo, Amhara na Tigriya. Kuna mengine zaidi ya 80 kama wasomali , Sidama lakini hawana ushawishi wa kisiasa
Hao wote wanapambania rasilimali za nchi kulingana na ukubwa na historia ya uongozi wa nchi kwa ujumla
na ndio wanaendeleza hivyo mpaka leo
Wewe sasa ndio umetoa maelezo sahihi kuhusiana na kiini cha tatizo.. tawala za kijadi zilizokaa kipindi kirefu.

Halafu naskia hao wasomali huko Ethiopia wana jimbo lao kabisa kivipi wanakosaje kuwa na influence sawa na hao wengine kama amhara na oromo?
 
Kwa hiyo ameenda Ethiopia akaprove kuwa hiyo miradi haipo au
Nimeishi Dxb miaka ya 2002-2005, nikarudi tena 2016, 2020 na 2023
Nimeona maendeleo makubwa sana kwa muda mfupi katika nchi bila mfano wa popote kwengine hata hao majirani kama Qatar na pesa yao hawataifikia leo
Mtafute Sheikh Mohammed al Maktoum umsome Vision zake
Addis nimeishi 2015-2018, nikarudi tena 2021, 2024
Nikifanya progress comparison, Dxb ni way ahead ya ADD ambayo level yao kwa sasa ni DXb ya miaka 20 nyuma na Dubai inaendelea kila kukicha
Development ya mwaka kwa DXB ni kubwa mno kiasi kila ukienda baada ya mwaka unakuta wako mbele sana miundombinu na majengo
Kwa hiyo kuifikia kwa pesa ya kukopa na low human capital ni bado sana
Waondokane na state ownership kwa miradi na hii ni ngumu kwa sababu za kihistoria
Ethiopia haivutii wananchi wala wageni kufanya kazi labda wanaotoka majimboni kwenda Addis
Kuna msemo tunasema ukienda duniani usipomkuta muhindi hapo hakuna hela
Tajiri mkubwa hapo ni Msaud
Kiongozi ana progressive mindset lakini wananchi wanamuangusha na nchi yenyewe iko ki mitego
 
Kabila lao sio kubwa kama haya mengine na wanaonekana wakuja
Kuna makabila zaidi ya 80
Kwa kifupi Ethiopia is A highly diverse society which was forged into a state through conquest, governed through centralization, then reorganized around ethnicity without ever building a deeply shared national foundation
 
Nimeishi Dxb miaka ya 2002-2005, nikarudi tena 2016, 2020 na 2023
Nimeona maendeleo makubwa sana kwa muda mfupi katika nchi bila mfano wa popote kwengine hata hao majirani kama Qatar na pesa yao hawataifikia leo
Mtafute Sheikh Mohammed al Maktoum umsome Vision zake
Addis nimeishi 2015-2018, nikarudi tena 2021, 2024
Nikifanya progress comparison, Dxb ni way ahead ya ADD ambayo level yao kwa sasa ni DXb ya miaka 20 nyuma na Dubai inaendelea kila kukicha
Development ya mwaka kwa DXB ni kubwa mno kiasi kila ukienda baada ya mwaka unakuta wako mbele sana miundombinu na majengo
Kwa hiyo kuifikia kwa pesa ya kukopa na low human capital ni bado sana
Waondokane na state ownership kwa miradi na hii ni ngumu kwa sababu za kihistoria
Ethiopia haivutii wananchi wala wageni kufanya kazi labda wanaotoka majimboni kwenda Addis
Kuna msemo tunasema ukienda duniani usipomkuta muhindi hapo hakuna hela
Tajiri mkubwa hapo ni Msaud
Kiongozi ana progressive mindset lakini wananchi wanamuangusha na nchi yenyewe iko ki mitego
Nimesema Addis inaweza kuwa kama Dubai kwenye miundombinu in next 20 years
Yani Addis ya mwaka 2045 inaweza kufanana na Dubai ya 2025
 
Nimesema Addis inaweza kuwa kama Dubai kwenye miundombinu in next 20 years
Yani Addis ya mwaka 2045 inaweza kufanana na Dubai ya 2025
Abiy Ahmed anawindwa na mafisi aondoke watu wagawane nchi
Tigray, Oromia wanamlia timing tu
 
Sisi toka watuulie Magufuri wetu tumefulia ile mbaya

Hatuna kipya tena kinachofanyika ndani ya taifa letu ni ufisadi na uuzaji wa rasilimali za taifa na hali ngumu kwa vijana na mbaya zaidi mauaji
Yule bora alikufa
 
Huyu Rais wa Ethiopia sio poa aisee. Leo nilikuwa naangalia hii video inaonesha jinsi Addis Ababa inavyokua kwa kasi in just short time

Watu wanahamishwa uswazi wanapelekwa kwenye makazi bora, wanaongeza viwanda na uwekezaji kila kona, wanapanda miti everywhere, maghorofa yanajengwa kila kukicha, wana treni ya umeme ya ndani ya mji, yani jiji linakua kwa kasi, kila kona ni ujenzi tu

Angalia hii video uone jinsi Addis Ababa inavyobadilika siku hadi siku

View: https://youtu.be/TRC243t3jkc?si=Ol1iiWwO9joejrod

Sisi toka watuulie Magufuri wetu tumefulia ile mbaya

Hatuna kipya tena kinachofanyika ndani ya taifa letu ni ufisadi na uuzaji wa rasilimali za taifa na hali ngumu kwa vijana na mbaya zaidi mauaji
Sisi pia tunajenga sana Zanzibar sasa hivi
 
Lakini raia wake wanakamatwa kila siku bongo wakiwa kwenye magari ya mizigo wamekondeana wakikimbilia afrika ya kusini. Maendelea ambayo haya reflect maisha ya watu ni bure kabisa
 
Kwa hiyo ameenda Ethiopia akaprove kuwa hiyo miradi haipo au
Miradi ipo na ni mali ya Serikali, lakini watu ni maskini kupindukia.. Hakuna uhusiano kati ya utajiri wa nchi na hali ya wananchi. Wananchi wanaishi maisha duni sana
 
Miradi ipo na ni mali ya Serikali, lakini watu ni maskini kupindukia.. Hakuna uhusiano kati ya utajiri wa nchi na hali ya wananchi. Wananchi wanaishi maisha duni sana
Ndio watu wa Ethiopia ni masikini
 
wananchi wanataka ajira, huduma za kijamii kama elimu bora na affordable, huduma za afya
wakipata ajira na mzunguko wa fedha ukiongezeka kutokana na biashara watakuwa na makazi bora na hata kuweza kutumia hiyo miundo mbinu km treni za umeme, ndege na barabara za kisasa za kulipia kuwahi kufanya shughuli za kiuchumi
Tatizo kwa nchi kama Ethiopia, ajira hakuna, ukiipata mshahara kiduchu, mzunguko wa fedha mdogo sana , biashara zimeshikwa na ma don na wageni mwisho wa siku hata treni za mjini hawapandi wanatembea sana ila hali ya hewa inasaidia tu
Ukiwawezesha wananchi hata hiyo miundo mbinu watajenga wenyewe kwa PPP
kila kitu hatua , leo wanajenga miundo mbinu kesho wawekezaj wakija watavutia vibarua kukimbilia huko kisha mzunguko wa pesa utakuwa vzr

Mzunguko wa pesa hauji kwa kuruhusu pesa ziingie hovyo kweny mzunguko
 
Back
Top Bottom