Addis Ababa itakuja kuwa kama Dubai miaka 20 ijayo, sio kwa ujenzi huu aisee

Haa wapi hii hoja yako ya kuhusu exposure ninakukatalia mpaka kesho, hao jamaa wana exposure ya kufa mtu huwezi kabisa kuwalinganisha na nchi yoyote hapa Afrika mashariki.

Baada ya Nigeria nchi ya kiafrika inayofuatia kuwa na diaspora kubwa huko duniani ni Ethiopia.... wale ni global citizens wako mpaka kwenye vinchi vya central Asia kama Azerbaijan na Uzbekistan huko nchi ambazo huwezi kumkuta mbongo au mkenya.

Hili la kutokuwa na umoja nafikiri linaweza kuwa linachangiwa sana na tawala za kitamadunu ambazo zilikaa Ethiopia kwa muda mrefu sana huku kila jamii ikijiona ni bora kuliko wenzake.
 
Wewe sasa ndio umetoa maelezo sahihi kuhusiana na kiini cha tatizo.. tawala za kijadi zilizokaa kipindi kirefu.

Halafu naskia hao wasomali huko Ethiopia wana jimbo lao kabisa kivipi wanakosaje kuwa na influence sawa na hao wengine kama amhara na oromo?
 
Kwa hiyo ameenda Ethiopia akaprove kuwa hiyo miradi haipo au
Nimeishi Dxb miaka ya 2002-2005, nikarudi tena 2016, 2020 na 2023
Nimeona maendeleo makubwa sana kwa muda mfupi katika nchi bila mfano wa popote kwengine hata hao majirani kama Qatar na pesa yao hawataifikia leo
Mtafute Sheikh Mohammed al Maktoum umsome Vision zake
Addis nimeishi 2015-2018, nikarudi tena 2021, 2024
Nikifanya progress comparison, Dxb ni way ahead ya ADD ambayo level yao kwa sasa ni DXb ya miaka 20 nyuma na Dubai inaendelea kila kukicha
Development ya mwaka kwa DXB ni kubwa mno kiasi kila ukienda baada ya mwaka unakuta wako mbele sana miundombinu na majengo
Kwa hiyo kuifikia kwa pesa ya kukopa na low human capital ni bado sana
Waondokane na state ownership kwa miradi na hii ni ngumu kwa sababu za kihistoria
Ethiopia haivutii wananchi wala wageni kufanya kazi labda wanaotoka majimboni kwenda Addis
Kuna msemo tunasema ukienda duniani usipomkuta muhindi hapo hakuna hela
Tajiri mkubwa hapo ni Msaud
Kiongozi ana progressive mindset lakini wananchi wanamuangusha na nchi yenyewe iko ki mitego
 
Kabila lao sio kubwa kama haya mengine na wanaonekana wakuja
Kuna makabila zaidi ya 80
Kwa kifupi Ethiopia is A highly diverse society which was forged into a state through conquest, governed through centralization, then reorganized around ethnicity without ever building a deeply shared national foundation
 
Nimesema Addis inaweza kuwa kama Dubai kwenye miundombinu in next 20 years
Yani Addis ya mwaka 2045 inaweza kufanana na Dubai ya 2025
 
Nimesema Addis inaweza kuwa kama Dubai kwenye miundombinu in next 20 years
Yani Addis ya mwaka 2045 inaweza kufanana na Dubai ya 2025
Abiy Ahmed anawindwa na mafisi aondoke watu wagawane nchi
Tigray, Oromia wanamlia timing tu
 
Sisi toka watuulie Magufuri wetu tumefulia ile mbaya

Hatuna kipya tena kinachofanyika ndani ya taifa letu ni ufisadi na uuzaji wa rasilimali za taifa na hali ngumu kwa vijana na mbaya zaidi mauaji
Yule bora alikufa
 
Sisi toka watuulie Magufuri wetu tumefulia ile mbaya

Hatuna kipya tena kinachofanyika ndani ya taifa letu ni ufisadi na uuzaji wa rasilimali za taifa na hali ngumu kwa vijana na mbaya zaidi mauaji
Sisi pia tunajenga sana Zanzibar sasa hivi
 
Lakini raia wake wanakamatwa kila siku bongo wakiwa kwenye magari ya mizigo wamekondeana wakikimbilia afrika ya kusini. Maendelea ambayo haya reflect maisha ya watu ni bure kabisa
 
Kwa hiyo ameenda Ethiopia akaprove kuwa hiyo miradi haipo au
Miradi ipo na ni mali ya Serikali, lakini watu ni maskini kupindukia.. Hakuna uhusiano kati ya utajiri wa nchi na hali ya wananchi. Wananchi wanaishi maisha duni sana
 
Miradi ipo na ni mali ya Serikali, lakini watu ni maskini kupindukia.. Hakuna uhusiano kati ya utajiri wa nchi na hali ya wananchi. Wananchi wanaishi maisha duni sana
Ndio watu wa Ethiopia ni masikini
 
kila kitu hatua , leo wanajenga miundo mbinu kesho wawekezaj wakija watavutia vibarua kukimbilia huko kisha mzunguko wa pesa utakuwa vzr

Mzunguko wa pesa hauji kwa kuruhusu pesa ziingie hovyo kweny mzunguko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…