Aden Rage kumshauri Try Again na Mangungu kudai Tsh. Milioni 100 za bango la Yanga kuifunga Simba 5

Aden Rage kumshauri Try Again na Mangungu kudai Tsh. Milioni 100 za bango la Yanga kuifunga Simba 5

Mwenyekiti wa zamani wa Simba na FAT Adan Rage, amesema wataidai na kuipeleka mahakamani kampuni ya outdoor, Saifi store waliohusika na Kutundika bango lilitumia nembo ya Simba, kwani muendo huo ni wa kibiashara na wamejitangaza kupitia logo ya Simba bila ridhaa ya Simba wenyewe.

Mbobevu huyo wa Sheria amedai ataongea na Try again na Magungu na Viongozi wengine wa Simba kupeleka Madai yao ya kiasi kisichopungua mil 100 Kwa Saifi store ikiwa ni sehemu ya pesa ya kutumika Kwa nembo yao.

Ikumbukwe kuwa club ya yanga iliipa kazi kampuni ya Saifi store kutengeneza na kupandisha bango kubwa linaloonesha ushindi wa bao 5-1 Kwa Yanga dhidi ya Simba.

Kauli hiyo pia imeenda sambamba na pongezi za ushabiki Bora, na pongezi mahsusi kutoka Kwa rais wa fifa kuwa Simba inapiga mpira kuliko Wyada na Mamelod.
Million 100 kidogo sana,brand ya Simba ni kubwa mno,hapo haizidi haipungui Billion 5
 
Ila yanga ni washamba sana kwakweli.. Sikuwahi kudhani kama ile ushindi unaweza kuwa such a big deal kiasi cha kuweka bangi kama lile

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka wanaenda kulishana supu ya vibudu,kweli hawa ni nyani kabisa
FB_IMG_1700028629335.jpg
 
Hiyo kesi Simba hawezi kushinda ..

Kudai fidia kuhusu nembo itakuwa ngumu ..kwakuwa pale kuna NBC premier league ..ambaye ameingia mkataba na Azam TV na bodi ya ligi..

Hiyo picha IPO kwenye page ya Azam TV ...ambao wana haki ya kupiga picha na kuzisambaza popote pale Duniani ...

Na ndio maana hata official page za Yanga kwenye Instagram, Facebook, sijui Twitter/X hizo image (nembo) zipo ila kwa hisani ya Azam Tv..

Azam TV ameruhusiwa kupiga picha na video kisha kurusha kwa MTU yoyote ..ili aweze kuzitumia kama habari au kumbukumbu ..

Azam TV amelipia hizo images ..na haki ya matangazo ..ambapo images hizo zinatumika ..popote pale ..
Kwa hiyo tangazo ni sehemu ya 'popote pale' ? Kwamba CRDB wanaweza kudownload picha ya John Bocco kupitia Azam Tv na kujitangaza kwa kupitia hiyo picha?
 
Kuna mdau alileta mada ya kuuliza Kama ni sahihi kisheria kilichofanywa na yanga kuweka Hilo bango. Kuna waliomtukana lakini inawezekana rage pia ni mdau wa huku kaona hiyo taarifa. Mabango yapo kibiashara na biashara imefanyika lakini bila ridhaa ya mtu mwingine.
Outdoor wamelipwa, tra wamelipwa , tarura au tanroad pia wamelipwa na mabispaa ya kinondoni wamelipwa. Simba watashinda hiyo kesi mapema tu kwa sababu wamewekwa kwenye tangazo bila kuhusishwa.
Je hiyo taarifa kwenye bango ni ya uongo?
 
Huhitaji kibali cha simba kutangaza matokeo ya mechi za Simba, ina maana na magazeti yanailipa simba ?

Simba hapati chochote hapo
 
S
Hiyo kesi Simba hawezi kushinda ..

Kudai fidia kuhusu nembo itakuwa ngumu ..kwakuwa pale kuna NBC premier league ..ambaye ameingia mkataba na Azam TV na bodi ya ligi..

Hiyo picha IPO kwenye page ya Azam TV ...ambao wana haki ya kupiga picha na kuzisambaza popote pale Duniani ...

Na ndio maana hata official page za Yanga kwenye Instagram, Facebook, sijui Twitter/X hizo image (nembo) zipo ila kwa hisani ya Azam Tv..

Azam TV ameruhusiwa kupiga picha na video kisha kurusha kwa MTU yoyote ..ili aweze kuzitumia kama habari au kumbukumbu ..

Azam TV amelipia hizo images ..na haki ya matangazo ..ambapo images hizo zinatumika ..popote pale ..
Subiri uone! Watadaiwa zaidi ya m100! Nembo kutumika bila kibali ni kosa kubwa! Especialy ka,ma umeitumia kwa lengo la kuifedhehesha!! Ujinga ni mzigo mkubwa sana!!
 
Back
Top Bottom