Raphael Thedomiri
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 442
- 729
Hoja ya kutowacharaza watoto na hata wanafunzi mashuleni sio mpya, lakini je ni upi unaweza kuwa mbadala?!
Nimejaribu kuwashirikisha njia mbadala niliyojifunza mahali fulani.
Adhabu ya viboko ni ya muda mrefu sana duniani, ni ya karne na karne. Ikikita mizizi zaidi katika bara letu la Afrika.
Malezi ya watoto bila kutumia adhabu ni jambo gumu ama lisilowezekana kabisa, hata sisi watu wazima mamlaka zimeweka mbele yetu adhabu mbalimbali tukoseapo kama faini au vifungo gerezani.
Tunaweza kuwaadhibu watoto wetu bila kutumia viboko.
Badala ya kuwatandika watoto viboko, tumia adhabu hizi mbili, ninakupa uhakika kuwa adhabu hizo zitajenga nidhamu kwa watoto/wanafunzi wako si ajabu hata kuliko kuwacharaza.
Wanapokosea wanyime vitu wanavyovipenda kwa mfano wanyime ruhusa ya kwenda nje kucheza na wenzao, ama wanyime kutazama tv, ama wanyime kucheza game n.k
Au walazimishe kufanya wasivyovipenda mfano kufanya kazi fulani za nyumbani labda kusafisha nyumba, ama kuosha vyombo n.k