Adhabu mbadala wa viboko kwa watoto na wanafunzi wetu

Adhabu mbadala wa viboko kwa watoto na wanafunzi wetu

Kumsimamisha mwanafunzi in a naughty what..??....Hebu kuwa serious eti.....hakuna namna eti wala huo muda wa mwalimu kumvuta pembeni mwanafunzi mmoja mmoja na ku-deal naye na hapo darasani ana wanafunzi zaidi ya 100 na pia ana vipindi madarasa mengine.....short and clear anamaliza mchezo kwa fimbo zake tatu tatu za nguvu...
Mkuu tuna haki ya to disagree, corporal punishment kwangu ni NO
 
Hoja ya kutowacharaza watoto na hata wanafunzi mashuleni sio mpya, lakini je ni upi unaweza kuwa mbadala?!

Nimejaribu kuwashirikisha njia mbadala niliyojifunza mahali fulani.

Adhabu ya viboko ni ya muda mrefu sana duniani, ni ya karne na karne. Ikikita mizizi zaidi katika bara letu la Afrika.

Malezi ya watoto bila kutumia adhabu ni jambo gumu ama lisilowezekana kabisa, hata sisi watu wazima mamlaka zimeweka mbele yetu adhabu mbalimbali tukoseapo kama faini au vifungo gerezani.

Tunaweza kuwaadhibu watoto wetu bila kutumia viboko.

Badala ya kuwatandika watoto viboko, tumia adhabu hizi mbili, ninakupa uhakika kuwa adhabu hizo zitajenga nidhamu kwa watoto/wanafunzi wako si ajabu hata kuliko kuwacharaza.

Wanapokosea wanyime vitu wanavyovipenda kwa mfano wanyime ruhusa ya kwenda nje kucheza na wenzao, ama wanyime kutazama tv, ama wanyime kucheza game n.k

Au walazimishe kufanya wasivyovipenda mfano kufanya kazi fulani za nyumbani labda kusafisha nyumba, ama kuosha vyombo n.k
SIkubaliani na wewe kwenye option yako ya pili..!! Kwamba wape kazi wasizozipenda..!! Ukishampa mtoto kazi ya kufanya kwa maana ya adhabu, ujuwe hiyo kazi ataitazama kwa jicho hilo kwa maisha yake yote yaliyobaki. Hii ni hatari, maana kazi hiyo lazima ifanywe, iwe kama adhabu au hiari
 
Mkuu tuna haki ya to disagree, corporal punishment kwangu ni NO
Kwangu ni big YES na HAITATOKEA IKAISHA....wewe endelea kupiga porojo za vijiwe vya kahawa....wanangu wote wakifanya makosa ya kizembe wanachezea na walimu wao huwa nawaambia mtoto akijichanganya vunja sitaki kufuga vibaka na machangu kwangu....
 
Utatuletea a very violence family ambayo haitakua na upendo, wewe ndio baba unaporudi kazini watoto wako wanakimbilia chini ya uvungu wa vitanda huku wakijikojolea
 
Makosa mengine ya kumuelekeza hivyo ukimtishia utamjengea hofu na utamjengea kukosa kujiamini anapofanya mambo yake. Ukimuelekeza kwa upendo maadamu ni mtoto ataona upendo unaojengeka.

Makosa mengine ni makubwa hayafai kwa kumuelekeza inabidi umpatie adhabu kubwa nayo ni kumtia fimbo na kumwambia kosa alilolifanya!

Utofauti huo utamjengea kuwa kuna masuala mazuri na kuna masuala mabaya ambayo akiyafanya yatamfanya awajibike kwa kutiwa mboko! Kwa kuwa umezungumzia watoto na wanafunzi basi hili jukumu ni la jamii au kwa mzazi na kwa mwalimu kwa maana ya ulezi. Ila wazazi bado wana nafasi kubwa katika hili.

Binafsi, naunga mkono adhabu ya fimbo.
 
Hapo itakuwa kuleta uzungu katika jamii ya mwafrika. Matokeo yake matoto yatakuwa na viburi na utukutu utaongezeka.

Swala la kujua ni kwamba maadili yameshuka sana kutokana na kuharibika kwa misingi ya malezi kama matokeo ya kudhoofika kwa taasisi ya Ndoa ambayo ndio hujenga familia.

Watoto wanapokuwa wanalelewa katika familia dhaifu kama matokeo ya Ndoa dhaifu then watoto wanakuzwa nje ya maadili na hii hupelekea kuongezeka kwa makosa wanapopelekwa taasisi kama shule ambazo husimamia maadili na misingi ya tabia njema, hii hupelekea kupata adhabu za kujirudia mfululizo za viboko na kuwa sugu na matokeo yake jamii huona watoto kama wanateseka na hizi adhabu kumbe ni matokeo ya wao kutoshika maelekezo ya nidhamu na maadili wanayopewa kuyafuata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi utoto na uanafunzi ukiisha, watu huwa na nidhamu? Nahisi kama wezi wa rasilinali za nchi hawashughulikiwi, ila watoto na wanafunzi tu ndio wanaonewa.
 
Mkuu tuna haki ya to disagree, corporal punishment kwangu ni NO
Bible yenyewe imesema usimnyime mtoto viboko, halafu wewe unajifanya kuleta uzungu wako.

Kuna maeneo kama sijakosea 2 kwenye biblia inasisitiza mapigo kwa watoto jinsi yatakavyo wasaidia.

Nafikiri ni vema kuchanganya aina zote za adhabu.
 
Uzungu utatufikisha pabaya sana! Je umetafiti madhara ya viboko against nidhamu ya watoto wa zamani na kuondoa viboko na nidhamu ya sasa?
 
Hoja ya kutowacharaza watoto na hata wanafunzi mashuleni sio mpya, lakini je ni upi unaweza kuwa mbadala?!

Nimejaribu kuwashirikisha njia mbadala niliyojifunza mahali fulani.

Adhabu ya viboko ni ya muda mrefu sana duniani, ni ya karne na karne. Ikikita mizizi zaidi katika bara letu la Afrika.

Malezi ya watoto bila kutumia adhabu ni jambo gumu ama lisilowezekana kabisa, hata sisi watu wazima mamlaka zimeweka mbele yetu adhabu mbalimbali tukoseapo kama faini au vifungo gerezani.

Tunaweza kuwaadhibu watoto wetu bila kutumia viboko.

Badala ya kuwatandika watoto viboko, tumia adhabu hizi mbili, ninakupa uhakika kuwa adhabu hizo zitajenga nidhamu kwa watoto/wanafunzi wako si ajabu hata kuliko kuwacharaza.

Wanapokosea wanyime vitu wanavyovipenda kwa mfano wanyime ruhusa ya kwenda nje kucheza na wenzao, ama wanyime kutazama tv, ama wanyime kucheza game n.k

Au walazimishe kufanya wasivyovipenda mfano kufanya kazi fulani za nyumbani labda kusafisha nyumba, ama kuosha vyombo n.k
Mkuu kama wewe sio mwalimu bora ungakaa kimya tu. Usifundishe watu kufanya kazi. Viboko hufundishwa chuoni na kuna namna ya kumwadhibu mwanafunzi hivo hizi ni taaluma za watu. Huwezi niambia upeleke kufagia wanafunzi umekuta hawajafanya jaribio labda robo ya darasa wakati kuna vipindi vinaendelea.
 
Bible yenyewe imesema usimnyime mtoto viboko, halafu wewe unajifanya kuleta uzungu wako.

Kuna maeneo kama sijakosea 2 kwenye biblia inasisitiza mapigo kwa watoto jinsi yatakavyo wasaidia.

Nafikiri ni vema kuchanganya aina zote za adhabu.
Mimi ji muumini wa dini yangu ya mizimu, hizi dini zimeletwa na merikebu!
 
Kwanz niseme kimaisha hatujafikia Hatua yaakuachana na coplo punishment kutokana na mazingira yetu

Na hii tunaona directly kwa watoto wa kishua kwa asilimia kubwa wamefeli maiasha au wamesaidia maish kwa 100%

Viboko bado Muhimu mazngr bado hajatupa ufanisi mwingne
 
Hao kwa ufup hawaelew mazingira ya malez na kazi za ufundishaji na ujifunzaji , Wanaroppoka tuu

Kiufup mazingira yetu bila viboko bado sana aaaaaaa

Kumsimamisha mwanafunzi in a naughty what..??....Hebu kuwa serious eti.....hakuna namna eti wala huo muda wa mwalimu kumvuta pembeni mwanafunzi mmoja mmoja na ku-deal naye na hapo darasani ana wanafunzi zaidi ya 100 na pia ana vipindi madarasa mengine.....short and clear anamaliza mchezo kwa fimbo zake tatu tatu za nguvu...
 
Fikiria darasa linawanafunzi 25 na wote watatakiwa kuadhibiwa.Je,utajigawa vipi kumfatilia yule na yule ktk adhabu zao.Lakini wote ukiwatoa darasani unabaki na nini.Pia kumnyima asiende mapumziko hiyo hairuhusiwi!

Nyumbani pia ni mtihani kukaa umchunge akamilishe adhabu flani.
Pia kunavijimakosa vidogo vidogo ambavyo mtoto hutakiwa kuzabuliwa on the spot ili akomeshwe haraka then maisha/shughuli ziendelee!

(Wataalam wa akili za watoto wanasema adhabu inatakiwa kutolewa haraka mara tu baada ya kosa kutendeka na wakati wa kumwadhibu mhusika unatakiwa uwepo karibu naye ukiendelea kumuonya na kumwambia kwanini umempa adhabu husika!)
 
No no mkuu huwezi kwa mwalimu aliyeiva kumtoa mwanafunzi nje ya kipindi kama adhabu, kuna adhabu kama za kumsimamisha in a naught corner, pia fanya utafiti mdogo why mwanafunzi ana react kwa tabia Ile,then mwalimu anajua the way forward
Tatizo we hujawahi kuwa mwalimu,hebu kaombe shule ufundishe hata kwa siku tatu alf uwe unatumia hzo adhabu zako uone kama zitaleta mabadiliko.

M nakubaliana na mawazo yako lakin kwa Afrika ili tuweze kutumia hizo adhabu na ziweze kutoa matokeo chanya inahitaji mabadiliko makubwa katika uleaji wa watoto wetu,na hayo mabadiliko yaanzie kwa wazazi kwa kubadili mitazamo ambayo tunayo,na itachukua hata miaka 100 ili kufikia lengo
 
Back
Top Bottom