UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Ukipitia komenti humu naona watu wanajisahau wanapochukulia waarabu ndiyo uislamu wenyewe...uislamu ni amani na kutenda haki hivyo ata akiwa ni muislamu wakati huo akawa mwarabu pasina kutenda haki na kufata yaliyoamrishwa na dini ya uislamu atahukumiwa yeye kama yeye si uislamu ndiyo uhukumiwe kwa sababu yake japo kwa kiasi kikubwa wasio na uelewa wamekuwa wakiuhukumu uislamu kupitia kwa watu hao maana hauna upungufu (dini iliyokamilika) hivyo wanahukumu kupitia madhaifu ya binadamu ambacho si sawa.
Uislamu ulikuwepo kabla yake (mfalme huyo) na utaendelea kuwepo hivyo waarabu pia ni binadamu hivyo ni chaguo lake kuwa mwema au asiwe mwema ila muislamu anayefata maamrisho mema na kukataza mabaya kamwe huwa mwema na hutenda haki wakati wote.
Sasa chukulia matukio yaliyowahi kutokea hapa nchini kwetu au kwingine halafu ufikiri halafu uendelee kudai uislamu ni ugaidi.
Mf.
1.tukio la mtu kuuawa na mwili wake kuhifadhiwa katika ndoo kubwa ya maji (jaba)
2.mauaji ya albino
3.mtu kuuawa kisha kufungwa katika baiskeli na kudumbukizwa katika maji(kanda ya ziwa)
4....
Je hao pia uislamu uliwatuma kutenda hayo???
Watu wanachuki na Uislamu wenyewe na si hivyo vitendo vya ukatili ambavyo vipo kila mahali na vinafanywa na yeyote,haya yote wanayolalamikia humu ni sababu tu wanatumia kutoa chuki zao.