Kiongozi mimi ni muislamu sio tu wakuzaliwa bali ni muislamu ambae nimezaliwa katika uislamu na kujifunza uislamu.Mzee mada hii imekuzidi sana uwezo.Kabla ya kuileta kwanza ulitakiwa utenge muda kujua ni kitu gani unataka ukiwasilishe kwa watu,pia uangalie sana chanzo ambacho unaitoa hii habari.
Kwa uchache ulitkiwa ufahamu yafuatayo,si tu ufahamu juu juu bali ufahamu kielimu.
Ulitakiwa ujue
1.Ni ipi nchi ya kiislamu.
2.Uijue saudia ni nchi ya aina gani
3.Hukmu kwa mujibu wa sheria,yaani kilugha na kiistilahi
4.Ujue ya kuwa kuzungumza jambo ambalo huna elimu ni dhambi
5.Ujue hukumu hazipimwi kwa hisia
Japokuwa sijui imani yako mzee.Ila kuitendea haki misingi ya kielimu nakushauri rudi tena kafanye utafiti au ungekuja kwa mtindo wa kuuliza swali ili ufundishwe lakini si kupotosha umma.
Kaka nina mengi sana ya kusema kuhusu uongo uliomo katika hii makala yako,na hakuna kitu kibaya kama kuwazulia watu uongo.