Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Status
Not open for further replies.
Ni kwanini basi wawe wakazi wengi wa motoni kisa zaka tu? na hayo maelezo mengine kwanini unayakataa hayaendani na hukumu tajwa??
 
Kijana unachanganya changanya mambo ili mradi mtu asikufatilize sio.
Jaribu kuleta jambo moja baada ya lengine kisha omba maelezo. Sasa hapa umechanganya habar ya boko haram, sjui Sudan n.k
Mi nakujibu nukta moja baada ya nyingine.
Kwanza Boko haramu ni moja ya kakundi ya kikhawaarij(yametoka katika utii wa mtawala wa haki). Kundi ambalo linamadhara sana kwa waislam na wengine kwa ujumla. Kwa kuzingatia mafunzi ya dini kundi hili na harakati zake zote wanazofanya hazipo katika mafundisho ya dini yetu. Na ikiwa wanalo wanalolifanya ukadhani limefunzwa na uislam liletee ref.

Case ya Sudan sijawahi kuiskia pamoja na hilo sijui kuwepo kwa hukmu ya mwanamke kuuwa ikiwa ameolewa na asie muislam. Japo ninalojua tu ni kua uislam umekataza mwanamke muislam kuolewa na asie muislam. Kama una ref ya hayo yaliyofanywa yamefunzwa na dini tuoneshe.

Kuhusu majini kua wa kwanza kuamini huu ni uzushi wa ajabu uliouleta maandiko uliyoleta hayasemi hivyo. Kama nilivyosema awali unalazimisha yale unayowaza kuhusu uislam yawe ndio lakin nafasi hiyo haipo.
Nakueleza kilichopo kwenye hiyo hadithi uliyoleta.
Quran 67.5 inasema

"Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa, na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto uwakao kwa nguvu." katika kazi za nyota alizozipa Allah miongoni mwazo ni kuwapigia mashetani wanaotaka kuvuka kuelekea mahala ambapo hawaruhisiwi kufika. Hivyo kila wanapikaribia ukingo huo wanatandikwa.

Habari ya hao majini waliosikia quran na kuiamini ni haqi hilo halina shaka. Sijajua utata wako uko wapi hapo!

Katika vitu navyo vishangaa kwenu ni kusema mungu wenu huyo mnaemuabudu haja umba kila kiumbe. Yani kuna viumbe si vyake. Huoni kama anamapungufu? Yani kayika ulimwengu kuna viumbe havijaumbwa na unae muabudu!!!

Basi mimi ninaemuabudu ameumba vyote wakiwemo majini katika hili sijaona tusi bali umempa sifa anayostaki yeye ndie Mungu wa majini na watu na kila kiitwacho kiumbe. Pia ametakasika kua na mke na mtoto. Hizo sifa za viumbe wake si yeye
 
Ni kwanini basi wawe wakazi wengi wa motoni kisa zaka tu? na hayo maelezo mengine kwanini unayakataa hayaendani na hukumu tajwa??
Laa unatatizo la kunukuu ndugu yangu hamna mahala palipotajwa zaka mi nimeona hivi
"You curse frequently and are ungrateful to your husbands."
Kutoa sadaka imekuja ili kuwasafisha na hayo madhambi yaliyotajwa na mengine na mwishi wa siku waingie peponi.

Maelezo ninayoyakataa yapi?
 
Kijana acha kuruka kuruka kwa kutoa nukuu bila kuzielewa.Kwanza kabisa Boko Haramu hawahukumu kwa sheria za Kiislamu.Sababu hakuna dola katika dola nyingine.Uislamu ni elimu mzee.Uislamu yaani Qur'an na Sunnah kwanza hutafsiriwa kwa zenyewe kisha Qur'an kwa hutafsiriwa kwa sunnah,kauli za maswahaba na maimamu pia.

Halafu unaposema ya kuwa majini ndio wa mwanzo kuiamini Qur'an kwa aya gani inayoonyesha hivyo.Mzee nilitamani nikujibu kwa ufupi sana sababu ndio jibu muafaka ulilotakiwa kupewa.

Unapozungumzia tukio la majini kuiamini Qur'an baada ya kuisikia inabidi ujiulize tukio hilo lilitokea kipindi gani na mwaka gani na mtume wetu amani za Allah ziwe juu yake alijiuje ya kuwa majini wameisikia na kuiamini Qur'an.

Sasa kama nyinyi mmezoea kubeba beba maandiko bila kujua tafsiri zake na sababu za kushukua maandiko hayo ni nyie sio huku kwetu.

Kwa ufupi Uislamu huujui mzee.Bora uulize uelekezwe...
 
Mama ake Yesu alikuwa na mume ? Mbona alizaa ? Usiwe na ufahamu finyu kiasi hicho ? Unafikiri kila kilichozaliwa kilikuwa na wazazi wawili ? au kilichokuwepo kilitokana na uwili ?

Mzee huwezi kumjadili Mola wa ulimwengu kwa mihemko namna hiyo mpaka ukasahau ya kuwa mnaemuita Yesu na kumuabudu alipatikana bila ya baba kwa uwezo wake Allah.Hii ni elimu na huwa nayo wanaume wenye vifua vya kuhifadhi elimu.

Allah wetu aliyejuu,ndio alimuumba mnaemuita Yesu na kumuabudu kwa ujinga.Tabia za wakiristo hazibadiliki sababu ndio mlivyo,wakiristo walipotea sababu ya kufata vitu vichwa mchungwa na mayahudi walipotea sababu ya kukithirisha kwao kuuliza uliza hata vile vitu ambavyo wanajua majibu yao.

Ndio maana sikushangaa nilipoona uliposema ya kuwa "Mungu wa majini hakuzaa sababu hakuwa na mke",ujinga uliopea kabisa.

Ukija na hoja nyingine nitakueleza nini tofauti ya tafsiri na tarjama.Kisha nitakupa maana ya hizo aya tukufu ulizozinukuu.

Mola wetu hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hana mfano wa kitu chochote....
 
Una hoja dhaifu kuliko nyumba za bui bui....Hiyo sura inaitwa surat al jinn,sura hiyo inazungumzia majini na jinsi walivyoiamini Qur'an na kuisifia,wakasema "Hakika hali wa shani sisi tumeisikia Qur'an ya ajabu..."
 
Taratibu taratibu kaka.
Tuwe layyin
Mana hapa twanfunza asiejua.
 
Hoyaaa mnao bishana juu ya dini sio powa kama vipi anzisheni thread ya kufunzana huko muuache huu uzi upumue..haukuanzishwa kwaajili yane.
 
The bold na mimi pia ni mdau mkubwa kwahyo nitag ili niendelee kufaidi uhondo wa stori zako
 
Kwahiyo unakubali Uislam ulizaliwa na Shetani/Lucifer?
Hakuna maana nyingine ya aya hii ya majini, unless unambie unakuja na new version yako na si ya Mudy.
ikiwa mola wako hakuzaa na hakuzaliwa, ila akitaka kuzaa anaweza sawa?

Kwenye Nyekundu hapo mbona unatofautiana na quran ya Muhammad aloshushiwa na allah?
 
Una hoja dhaifu kuliko nyumba za bui bui....Hiyo sura inaitwa surat al jinn,sura hiyo inazungumzia majini na jinsi walivyoiamini Qur'an na kuisifia,wakasema "Hakika hali wa shani sisi tumeisikia Qur'an ya ajabu..."
Wacha hizo! Majini ni Makenge yasiyo onekana, kazi yao kujambajamba misikitini na kukojolea wale waislamu wanaosinzia wakati wa sala.Kuna kitu gani cha kusifia ndani ya quran mpaka majini yasifie? Tuambie japo aya moja yakusifiwa na majini katika Qur'an.
 
The Bold teremsha vitu. wanapewa ref. za kusapoti mada yako na kuonyesha jinsi unyama unavyotendeka kwa kisingizio cha Allah na udini wanabishia tu.
 
Leta aya inayokwenda na kinyume na niliyo yasema mzee.Sio unaandika kisa una vidole vya kuandika.Jibu hoja kwa hoja sio "...mbona...".

Ulitakiwa kuelewa nilichokiandika sio uishie kusoma tu hoja zangu.Uislamu haujaanzishwa na SHETANI.Na mpaka naingia kaburini sio wewe tu hata wakubwa wenu katika dini mnaowafata kichwa mchunga hamuwezi kuleta ushahidi ya kuwa uislamu umeanzishwa na SHETANI.

Pili,rudi kajifunze kwa kina juu ya neno SHETANI,ukirudi na maana ya shetani nitakupa ufahamu sahihi juu ya hilo tamko la SHETANI...
 
Sasa uislamu uliletwa na nani? Unaweza kutudhitishie kwa maandiko kama aliyeleta uislamu siyo shetani Allah aka moon god?

Kwanza hamna ushaidi wowote kwamba uislamu uliletwa na Mungu wa Abraham, Yakobo, Isaiah au Waisrael. Kwa wayahudi neno Allah halikuwai kutumika. Hakukuwepo unabii wowote juu ya bedui Muddy au ushahidi wa yeye kupewa utume kwa dini inayopinga biblia na ukristo. Tupe ushahidi juu ya unabii wa Muddy na uungu wa Allah.
 
Unaandika maneno yasiyo na msingi lengo lako huenda likawa kukwaza imani mtu. Kwa mafunzo yangu mimi sitatukana wala kumtukana unaemuabudu. Ili ikiwa una nia ya kuuliza ili uelezwe tumia lugha ya kistarabu tu utaeleweka.
Tuanze somo sasa.
Umeomba kuthibitishiwa kuwa Mungu aliyemtuma Ibrahim, yakub na Musa ndo huyo aliemtuma Muhammad?
Jabu fupi kabisa ndiyo kwa ushahidi ufuatao
Quran 42.13
"Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye."
Naye Ibrahim aliomba kwa Mola wake atumwe kutokana na kizaz cha Ismail
2.127-128
"Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema."

Maneno yako ya kuzua umeyatoa wapi?
Lipe lengine unataka ufunzwe
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…