mkandu
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 336
- 463
THE BOLDmkandu,
Hongera kwa kunijibu kwa hoja walau sasa unadhihirisha wewe in great thinker... Maana great thinkers tunajadili kwa hoja namna hii sio kebehi...
Nirudi kwenye hoja zako...
Umeandika mambo ya maana sana ambayo naamini yana maana kubwa lakini bahati mbaya umetoka nje ya mada ninayoizungumza hapa...
Hoja zako zimejikita katika kutetea uhalali wa watu kuchinjwa hadharani, kwamba hoja zako unajaribu kuonyesha kwanini suala kuchinja watu hadharani ni halali... Nadhani hoja zako hazipingani na nilichoandika bali zinaunga mkono andishi langu...
Kwanini?
Katika makala hii kitu kikuu nilichojaribu kuonyesha ni kwamba "kuna nchi duniani bado wanachinja watu hadharani"... That's it! Sijajaribu kutetea wala kupinga... Nilichokifanya ni kuonyesha tu hiyo fact kwamba " kuna watu wanachinjana hadharani"!
Kama unapingana na mimi, nilitegemea uje hapa ulete ushahidi kwamba watu hawachinjwi... Yaani mimi kusema Saudi Arabia wanachinja watu nimedanganya... Utuonyeshe kuwa hawachinji raia wao au labda utuambie Al-Beshi sio mchinjaji...
Lakini kuja na hoja za kutetea uhalali wa watu kuchinjwa sioni ni namna gani unapingana nami sana sana umeniunga mkono fact yangu kwamba "Saudi Arabia wanachinja raia hadharani"!
Niseme kwamba, makala yangu imejaribu kuonyesha ukweli kwamba "Saudi Arabia bado wanachinja watu!" Suala la uhalali au uharamu wa hilo nakuachia wewe msomaji uamue kwa ufahamu wako...
Mfano wewe mkuu kwa ufahamu wako umetetea kwamba ni sawa kabisa watu kuchinjwa hadharani na umetoa sababu zako.... Naam hivyo ndivyo nataka!! Wewe ufanye maamuzi hayo kwa sababu zako... Wewe binafsi uunge mkono au upinge...
Pia wako wengine kadiri nilivyozisoma comments wamepinga vikali suala hili... Swadakta, nao wana haki ya kupinga kwa sababu zao...
Kwa ufupi ni kwamba kama unakubali Saudia Arabia wanachinja watu basi unaniunga mkono nilichoandika... That's the point na kiini cha makala hii... The fact that Saudi Arabia is still conducting public beheadings to its convicted citizens... Hiyo ni fact na kama unapingana nayo basi tueleze kuwa Saudi Arabia haichinji watu na utupe ushahidi...
Shukrani!
....Ahsante kwa kuelewa vile ambavyo ulivinukuu ambavyo vilikuwa na makosa ndani take.
Labda niseme tu lengo langu halikuwa kukupinga kuwa eti watu hawachinjwi laa.
Ni sawa na kukataa kuwa Tanzania watu hawanyongwi ila nilichokuwa naweka sawa ni zile sehemu nilizoziona zina makosa au hazina ukweli ndani yake.
Ijapokuwa nimetaja kwa uchache na kingine nilichopinga ni kupotosha lengo la kuchinja mbele ya hadhara.
Ni sawa umkute mkristo kaweka sanamu ya yesu ndani ya nyumba ww ukaita kapamba nyumba kumbe yy kamuweka kwa ajili ya ibada inakuwa unapotosha maana kwa kujitia kujua kwako.
Ikumbukwe ktk kujadili jambo au kuliandika jambo huwa na malengo makuu matatu..
(1) Kuelimisha
(2)kufurahisha
(3)Kuasa
Na hii mada imeegemea kwenye kuasa jamii ila ss ktk kuasa kwako unapotoka katika ukweli ukaingiza uongo tutaita propaganda.
Leo hii tutajisikiaje watanzania tutakapozushiwa kuwa tumeweka hukumu ya kunyonga kwa ajili kuwaasiri wapinzani .?
Na ndicho kinachosambazwa kwa wasaudia kuwa wanaochinjwa wanaonewa jibu likiwa ndio tutajiuliza tena je wanaonewa kwa mlengo UPI au minajili ya nani..?
Katk huu ulimwengu zipo minzani za kupima mambo kimitazamo tofauti kwa mfano jamii zetu za kiafrika mwanamke kuoa tutamtazama kwa jicho la tatu na India ukimchinja ng'ombe unaonekana umefanya kufuru na imekubalika kwenye serikali zao.
Kipi kinachoonesha km cha ajabu had kizue mjadala ktk hukumu za kiislam ikiwa tunakubaliana kuwa kila jamii IPO na mambo au itikadi zinazoaminiwa sehemu husika iweje patokee watu wajione wao ndo miongozo ya wengine na wengine hatuko sahihi.
......MKUU THE BOLD
Katika ulimwengu wa fitna tunapaswa kukwepa na kukaa mbali nazo harakati wafanyazo watu Fulani hii binafsi nimeona INA mlengo wa kuasa jamii ili tuseme no kwa kinachofanywa na Saudia ila kiukweli hii itakuwa inaharifu imani za sisi wengine ambao tunaamini na kile kinachofanywa na nchi km saudia km vile Yemen, Brunei ,Pakistan n.k
Nawasilishaaaaa
....Mkandu....
Chalileeee
