chaupimbi
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 206
- 60
Ndugu yangu napenda nipingane na wewe,lakini ni kwa hoja na sio kwa ngumi au matusi.
Kwanza adui wa mwanadamu SIO kifo (mauti),bali adui wa mwanadamu ni IBILISI/SHETANI.Ingawa wengi hawatokubali hoja hii na wengine wametamka hadharani kabisa kwamba shetani ndiye Mungu wao,lakini Mwenyezi Mungu ametutahadharisha juu ya huyu shetani kwamba ni ADUI YETU DHAHIRI.Na akasisitiza kwamba atakayemfanya shetani ni rafiki /Mungu/mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu;hakika amepata khasara zilizokua wazi.
Pili,kifo kimeumbwa na Mwenyezi Mungu.Yeye ndiye ANAYEFISHA na KUHUISHA.Na anasema kwamba kila nafsi ITAONJA UMAUTI.Na Mwenyezi Mungu kwa msisitizo kabisa anatuambia kwamba haifi nafsi yoyote ila KWA IDHINI YAKE.Yeye pekee ndiye mwenye kumiliki uhai wa kila kiumbe mbinguni na ardhini.
Tatu,kifo ni HATIMA YA LAZIMA kwa kila kiumbe.Mwanadamu hakuumbwa kuishi milele hapa duniani.Anaishi hapa kwa kipindi maalum kilichowekwa na Muumba.Muda wako wa kuwepo hapa duniani ukikamilika,kifo kinakuondoa hapa kwenda kizuizini.Sasa wale waliodai na wanaodai hakuna Mungu wakifa warudishie uhai kama jeuri wanayo maana ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye MMILIKI wa uhai wa viumbe vyote akiwemo na huyo shetani.
Umeongea vyema.. Imeandikwa ukimfuata yeye hatokutupa nje kamwe na hata ukifa Utaishi... Na kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.... Wanadamu hatujui tulitakiwa tupendane sana ili tumshinde adui yetu shetani.. Lakini sisi wenyewe tunaangamizana kwa kutumika na shetani..