Adui wa mwanadamu duniani

Adui wa mwanadamu duniani

Mti wa Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2015
Posts
331
Reaction score
99
Dunia hii kuna adui moja tu ambaye ni tishio kwa mwanadamu. Adui huyo hakuna mwanadamu anayeweza kumshinda licha ya kuwa mwanadamu hufanya jitihada za kila namna kumwangamiza lakini jitihada hizo hukwama.

KIFO.
Kifo ndiye adui mbaya na hatari katika maisha ya mwanadamu, kamwe hakuna aliyeshinda kifo kwa uzao wa mwanadamu wala hatotokea atakayeshinda kifo.
Kifo haijaletwa na MWENYEZI MUNGU duniani, MUNGU alituumba tuishi milele lakini uasi ndio imeleta kifo duniani.

Hakuna anayempenda huyo adui lakini hakuna namna ya kumshinda.
 
kulingana na hoja yako we mtu wa chuma .. adui unayemtaja sio kifo umejichanganya ... kwenye maelezo yako ..
 
Ndugu yangu napenda nipingane na wewe,lakini ni kwa hoja na sio kwa ngumi au matusi.
Kwanza adui wa mwanadamu SIO kifo (mauti),bali adui wa mwanadamu ni IBILISI/SHETANI.Ingawa wengi hawatokubali hoja hii na wengine wametamka hadharani kabisa kwamba shetani ndiye Mungu wao,lakini Mwenyezi Mungu ametutahadharisha juu ya huyu shetani kwamba ni ADUI YETU DHAHIRI.Na akasisitiza kwamba atakayemfanya shetani ni rafiki /Mungu/mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu;hakika amepata khasara zilizokua wazi.
Pili,kifo kimeumbwa na Mwenyezi Mungu.Yeye ndiye ANAYEFISHA na KUHUISHA.Na anasema kwamba kila nafsi ITAONJA UMAUTI.Na Mwenyezi Mungu kwa msisitizo kabisa anatuambia kwamba haifi nafsi yoyote ila KWA IDHINI YAKE.Yeye pekee ndiye mwenye kumiliki uhai wa kila kiumbe mbinguni na ardhini.
Tatu,kifo ni HATIMA YA LAZIMA kwa kila kiumbe.Mwanadamu hakuumbwa kuishi milele hapa duniani.Anaishi hapa kwa kipindi maalum kilichowekwa na Muumba.Muda wako wa kuwepo hapa duniani ukikamilika,kifo kinakuondoa hapa kwenda kizuizini.Sasa wale waliodai na wanaodai hakuna Mungu wakifa warudishie uhai kama jeuri wanayo maana ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye MMILIKI wa uhai wa viumbe vyote akiwemo na huyo shetani.
 
The worst tragedy in life is not DEATH but life without a purpose..

Dr. Myles Munroe R.I.P
 
mleta mada wewe mwenyewe umesema "UASI" ndio Unaleta Kifo.

Kwa muktadha huo basi Adui #1 kwa mwanadamu ni "UASI". Wala sio Kifo.
 
Adui mkuu wa Binaadamu ni yule alietangaza vita kwa kinywa chake juu ya binaadamu hebu mtafute mleta mada utamjua tuu
 
Haya ni Maswali yangu Kwa mleta Mada;
kifo Ni Kitu HALISI Mpaka kiwe Adui Yetu?au ni Mbinu tu ya Uandishi?

Pia umesema kuwa Mungu hakuumba kifo,kwanini Hakuumba kifo wakati yeye ndiye Muumbaji wa Kila kitu?
hapa ndipo ulipo utata wa wanaoamini mungu.kwenye kifo
 
Kifo si adui wa mwanadamu, KIFO NI CHAGUO LA MWANADAMU,
Mwanadamu yeyote ambaye amekubali kuzaliwa (KUANZA) pia amekubali kufa (KUMALIZA) kwa msingi wa kanuni ya kila chenye mwanzo kinamiliki mwisho pia.

Hivyo wanadamu tunakufa si kwa sababu ya adhabu au kosa, BINADAMU TUNAKUFA KWA SABABU TULIKUBALI KUWA NA MWANZO YAANI KUZALIWA NA VIVYO HIVYO TUNATAKIWA KUKUBALI KUWA NA MWISHO.

ukihofia kifo hakikisha umewahi kufa, kama hujawahi kufa usihofie kifo kwa kuwa bado hujakiexperience na yawezekana kikawa hakikuhusu (DEATH IS FOR THEM WHO DIED)
 
Mkuu hebu jaribu kuelezea vizuri ... .. .nimeelewa kwa mbalii kdogo
 
Dunia hii kuna adui moja tu ambaye ni tishio kwa mwanadamu. Adui huyo hakuna mwanadamu anayeweza kumshinda licha ya kuwa mwanadamu hufanya jitihada za kila namna kumwangamiza lakini jitihada hizo hukwama.

KIFO.
Kifo ndiye adui mbaya na hatari katika maisha ya mwanadamu, kamwe hakuna aliyeshinda kifo kwa uzao wa mwanadamu wala hatotokea atakayeshinda kifo.
Kifo haijaletwa na MWENYEZI MUNGU duniani, MUNGU alituumba tuishi milele lakini uasi ndio imeleta kifo duniani.
Hakuna anayempenda huyo adui lakini hakuna namna ya kumshinda.

Nafikiri kwa watu wa Imani adui Mkubwa wa mwanadamu ni SHETANI. Kwani kifo ni mauti ya mwili, lakini km dini zinavyotufundisha roho haifi, nadhani utakuwa unatambua nini kitatokea siku ya hukumu, km we ni muumini
 
Kifo si adui wa mwanadamu, KIFO NI CHAGUO LA MWANADAMU,
Mwanadamu yeyote ambaye amekubali kuzaliwa (KUANZA) pia amekubali kufa (KUMALIZA) kwa msingi wa kanuni ya kila chenye mwanzo kinamiliki mwisho pia.

Hivyo wanadamu tunakufa si kwa sababu ya adhabu au kosa, BINADAMU TUNAKUFA KWA SABABU TULIKUBALI KUWA NA MWANZO YAANI KUZALIWA NA VIVYO HIVYO TUNATAKIWA KUKUBALI KUWA NA MWISHO.

ukihofia kifo hakikisha umewahi kufa, kama hujawahi kufa usihofie kifo kwa kuwa bado hujakiexperience na yawezekana kikawa hakikuhusu (DEATH IS FOR THEM WHO DIED)

Asante Mkuu Pokofame Kwa kuwafafanuli Hawa watu.
Mimi nina Mshangaa sana Mtu anayeogopa Kifo.Kifo siyo Adhabu Bali ni kati ya Sheria za Asili

Nyota zina Kufa sembuse Mwanadamu?
Every Ordered system Must Go to Disorder Full stop.

Nondo zako ni special for 180 IQ'
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu napenda nipingane na wewe,lakini ni kwa hoja na sio kwa ngumi au matusi.
Kwanza adui wa mwanadamu SIO kifo (mauti),bali adui wa mwanadamu ni IBILISI/SHETANI.Ingawa wengi hawatokubali hoja hii na wengine wametamka hadharani kabisa kwamba shetani ndiye Mungu wao,lakini Mwenyezi Mungu ametutahadharisha juu ya huyu shetani kwamba ni ADUI YETU DHAHIRI.Na akasisitiza kwamba atakayemfanya shetani ni rafiki /Mungu/mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu;hakika amepata khasara zilizokua wazi.
Pili,kifo kimeumbwa na Mwenyezi Mungu.Yeye ndiye ANAYEFISHA na KUHUISHA.Na anasema kwamba kila nafsi ITAONJA UMAUTI.Na Mwenyezi Mungu kwa msisitizo kabisa anatuambia kwamba haifi nafsi yoyote ila KWA IDHINI YAKE.Yeye pekee ndiye mwenye kumiliki uhai wa kila kiumbe mbinguni na ardhini.
Tatu,kifo ni HATIMA YA LAZIMA kwa kila kiumbe.Mwanadamu hakuumbwa kuishi milele hapa duniani.Anaishi hapa kwa kipindi maalum kilichowekwa na Muumba.Muda wako wa kuwepo hapa duniani ukikamilika,kifo kinakuondoa hapa kwenda kizuizini.Sasa wale waliodai na wanaodai hakuna Mungu wakifa warudishie uhai kama jeuri wanayo maana ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye MMILIKI wa uhai wa viumbe vyote akiwemo na huyo shetani.

Tatizo kila siku unatuletea yaliyoujaza moyo wako ambayo ni uoga na kutokujiamini.

Kwani kushindwa kujirudishia uhai kunathibitishaje kwamba mungu yupo?
Jichunguze sana kijana! Usiwe unamuabudu mungu wako kwa vijisababu vidogo kama hivi... Maana ukitumia matatizo yanayoikabili jamii binadamu kama kigezo cha kumwamini na kumwabudu mungu wako, siku hayo matatizo yakipata majibu utapoteza imani.
Na hapa humaanishi kwamba unamuabudu huyo Mungu wako bali unayaabudu matatizo yako.

Na kama mungu wako ndio huyu anaeshindwa na matatizo kama haya tuyaonayo, basi ujue ni msiba mkubwa kwenu.
Maana hakudhihirishi ukuu wake bali kunadhihirisha udhaifu wake 🙂
 
Back
Top Bottom