Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Mimi nilisoma physics ,nikakutana na Mwalimu mmoja , ni shida aisee ,projectile alivyoifundisha alinishangaza enzi hizo tena mzungu , Alikuja na chungwa Moja

Akafuta ubao , akandika the topic of Today is Projectile Motion

Alichofanya akachukua lile chungwa akalirusha juu likachora Trajectory , lilipotua chini akasema topic imeisha akabeba makabrasha yake akaondoka ,

Siku iliyofuata akasema kama umekuja na A ya kuibia utaondoka na zero

Ha ha ha
Hahahahahaaaaa.

Walimu wengi wa Advance huwa hawajali aisee, wanapiga mapindi uwe umeelewe haujaelewe yeye hajali
 
Tatizo moja kubwa la physics unapoanza form 5 iko very interesting na unaiona A ya Necta inakuja. Kimbembe kinaanza kwenye maswali, unakuta umepewa data zisizohusiana na formula yoyote Kumbe ulitakiwa uzidishe area na length upate volume. Halafu hiyo volume uzidishe na density upate mass. Halafu hiyo mass uzidishe na acceleration upate Force ndio ukamilishe data za kufanya swali lako. Yaani hizo mbwembwe zote ila swali bado hujajibu na lina marks 3.

Nilikua na daftari nimeliwekea cover ya derivation ya Benourli principle ili niwe naiona mara kwa mara. Ila Ile biot savart Law ilinishinda kabisa kila nikisoma haipiti wiki nimesahau. Nilikua na topic zangu za ushindi, wave 1, electronics, modern, heat, current. Lakini maswali yalotolewa na NECTA nilikua siyajui kama sikusoma kitu vile. Nikaona ni miujiza tu itafanya nifaulu physics

Vifaa vya lab navyo ni majanga tu. limetre bridge linadeflect upande mmoja, nikianza upya bado linafanya vilevile. Msimamizi anasema endelea tu. Nikasema isiwe tabu nikawa naangalia data za mtu wa mbele na wa nyuma naweka average.

Tuacheni utani wanaopata mabanda ya physics ni kwa sababu wanasoma sana na kusolve sana maswali. Kupata swali la physics ambalo hujawahi kuliona sehemu ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.

Ilinichukua muda kuyaamini matokeo yangu ya form 6 baada ya kupata marks ambazo sikutegemea kabisa kupata kwenye physics. nakumbuka nilihakikisha namba zaidi ya mara tatu ndio nikakubali kweli ni mimi niliyepata lile karai. Niliweka sherehe
Hahahahahahaaaaaa

Umeelezea vizuri sana hii story
 
Sitasahau necta 2005 vifaa vya umeme viliponigomea Hadi msimamiz kunionea huruma nichukue data kwa jirani niendelee na swali kumbe jirani nae kapata data za uongo
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahaaa advance kazi yangu ilikua ni kukariri page za vitabu na maswali+majibu yake kwenye page husika...
Kwahio mtu akiniletea swali namtajia page alipolitoa halafu namtajia jibu kwa mbwembwe mwisho na swali linanishinda..
[emoji23] [emoji23] [emoji125]
 
Magnetism mpka naondoka adv, sija wahi igusa !


Wave , electronic, modern physcics, heat, ndo zilikuwa topic zangu,

Mungu si athumani
Nikapata F ,
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125]
 
Hahaha Daaah physics ni balaa Kuna T.O mmoja hivi alimaliza 2006 alikuja Kutufundisha sisi tukiwa form 6 tukajiona Vilaza Wote.. vitabu vya Chand...Roger. vyote tuliona Tumemaliza na Hakuna Swali Gumu.. Jamaa Halafu alikuwa ana dharau balaa na Chuo alifukuzwa Kisa Dharau kwa Maprofesa kwahiyo akabak anapiga Tuition mtaani tu na Sifa Kibao na Kuwaona Watanzania wote hawana Akili ila Yeye peke yake

Ila Nakumbuka Siku ya Mtihani wa Physics Nilipiga msuli Usiku halafu kesho yake Pepa Asubuhi Na Nikasolve Maswali Kama matatu hivi ya Chand kwenye Pepa Yamekuja Vile vile Nikasema Nashukuru Mungu Ndalichako kaniona

Ila Yote tisa nitarudi Shule Zote ila Siyo Advance
Jamaa alisomaga Tosamaganga enzi hizo.....alikuwa hatari sana kwenye physics na maths
 
Hahahahah shule yenyew O-level tulkuwa tunagonga Engineering Science badala ya Physics.....so ulikuwa ukichaguliwa Iyunga advance kama ulkotoka ulkuwa unabahatisha hakuna muujiza wa kutoboa.....ukigeuka kushoto unakutana na LE MUTUZ la Chemistry....Mr. SUDI.....***** mzee ana roho mbaya huyo.....kinyama.....

Umenkumbusha mbali sana kwa IYUNGA......
O level utakua umesome secondary ya ufundi wewe
 
Maisha hayapo fair, sitasahau wakati nimeenda kureport advance, siku ya kwanza kuingia class watu wanavunja mechanics muda mimi sijui lolote, na walimu kipindi hicho hamna tukajiorganize kama darasa ikabidi wale waliokwisha kava watupigie pindi...ila mwisho wa siku Mungu si athuman na kutangulia sio kufika necta ikaja tukapiga fresh hata zaid ya waliokuwa wamecover mapema

Nakumbuka kuna kipind mambo yalizid kuwa magumu maswal hayachomoki .... daaaah ikawa nikipata mda nitafuta sehemu najificha nalia weee nikimaliza narud zangu darasan au dom
 
Hahaha mkuu mademu walikuwa wtaturespect sana enzi hizo[/l
SAnaaa .uzur madem walk
ua hawaniulz maswal weng walkua o level...na kwa kuwatsha zaid nikawa nachkua miwani ya macho kwa wahuni af navaa...wee bac ilkua ni kuwaokota kama maembe
 
Aisee staki kukumbuka, nilikuwa nacheza A, B+, B pepa za ndani na nje. NECTA ikaniumbua vibaya yaani nikapata herufi ya kwanza ya jina langu. 'S'
 
kuna ticha wangu wa physics yy alikuwa kila ukimwambia hujaelewa au ukiuliza swali anakujibu"physics is for sure boys not for everyone"
Hahaaa hii kauli nimekutana nayo siku ya pili nafika shuleni... teacher anakwambia PCB is not for everyone. .
 
Back
Top Bottom