Tatizo moja kubwa la physics unapoanza form 5 iko very interesting na unaiona A ya Necta inakuja. Kimbembe kinaanza kwenye maswali, unakuta umepewa data zisizohusiana na formula yoyote Kumbe ulitakiwa uzidishe area na length upate volume. Halafu hiyo volume uzidishe na density upate mass. Halafu hiyo mass uzidishe na acceleration upate Force ndio ukamilishe data za kufanya swali lako. Yaani hizo mbwembwe zote ila swali bado hujajibu na lina marks 3.
Nilikua na daftari nimeliwekea cover ya derivation ya Benourli principle ili niwe naiona mara kwa mara. Ila Ile biot savart Law ilinishinda kabisa kila nikisoma haipiti wiki nimesahau. Nilikua na topic zangu za ushindi, wave 1, electronics, modern, heat, current. Lakini maswali yalotolewa na NECTA nilikua siyajui kama sikusoma kitu vile. Nikaona ni miujiza tu itafanya nifaulu physics
Vifaa vya lab navyo ni majanga tu. limetre bridge linadeflect upande mmoja, nikianza upya bado linafanya vilevile. Msimamizi anasema endelea tu. Nikasema isiwe tabu nikawa naangalia data za mtu wa mbele na wa nyuma naweka average.
Tuacheni utani wanaopata mabanda ya physics ni kwa sababu wanasoma sana na kusolve sana maswali. Kupata swali la physics ambalo hujawahi kuliona sehemu ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.
Ilinichukua muda kuyaamini matokeo yangu ya form 6 baada ya kupata marks ambazo sikutegemea kabisa kupata kwenye physics. nakumbuka nilihakikisha namba zaidi ya mara tatu ndio nikakubali kweli ni mimi niliyepata lile karai. Niliweka sherehe