Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Uzuri kwenye huu uzi

Kila mmoja anajipambanua kuwa kasoma physics.

Ila kiukweli nusu yao wachangiaji humu hawajasoma physics wanaishia kutaja tu aaa mara physics ngumu mara nini....!!

Kuna watu wanashinda humu mchana kutwa usiku kucha unajiuliza huyu hiyo physics alisoma lini na kama aliisoma???anafanya kazi saa ngapi???.

Jamani tuacheni drama na ku pretend

Ni hayo tu kwa sasa.
wewe bwana kwani unajuaje mtu hajasoma,au kusoma physics unaona kitu cha ajabu sana
 
physics_650x400_51489484821.jpg


5aeb30138efc5bd38c3a8aacd40cc677--projectile-motion-the-motion.jpg


Wakuu japo sijapost kwenye jukwaa hili kwa miezi kadhaa sasa hivyo naomba mnipokee tena mtaalamu Deadbody ,

Wakuu najua JF kuna watu wa kila aina ya masomo humu hivyo leo naomba niwakusanye watu wote waliosoma Advanced Physics tuje tukumbushie namna tulivyokuwa tunashangaa ndani ya chumba cha mtihani .

Ngoja nianze mimi aisee kuleta ushuhuda wangu wa kwanza kabisa:

Story inaanzia pale tu kijana Deadbody niliporipoti Advance school mara ya kwanza aisee ambapo nikapokewa kwa furaha sana na watu niliosoma nao Olevel na Primary.

Walinipokea kwa mbembwe sana maana balaa langu walikuwa wanalijua vizuri kuwa Physics na Maths niliumbiwa mimi(hahaha sipo serious hapa).

Nikapokelewa na kuonyeshwa Block nitakaloishi na maisha ya boarding ndio yakaanza rasmi .

TOPIC YA KWANZA KUFUNDISHWA KWA SOMO LA PHYSICS

Kama ilivyomazoea ya shule za advance kuwa walimu hukimbilia kuanza projectile motion,measurements and error hivyo ikawa hivyo hivyo kwa mwwalimu wetu ambaye alikimbilia kuanza na PROJECTILE MOTION.

ProjectileMotion.jpg


Dah aisee nilishangaa sana kuona topic hiyo ikifundishwa ndani ya siku moja na kuisha yote huku ikiwa na formula nyepesi mno kwa mwanafunzi kilaza kama Jesca kuelewa.

Formulas zilikuwa za Range ,height ambapo kila nikigusa swali kwenye kitabu cha CHAND linaenda natia tiki ,nikaanza kujiuliza kwanini watu wanasema hii topic ngumu mbona nimesolve maswali yote aiseeee..

Dah nikahitimisha tu kwa kujiona mimi ndio mwamba ,mwamba wa mathematics na sikwami kabisa swali la PROJECTILE MOTION .Wakati najitamba hivyo kumbe washikaji wananichora tu kuwa huyu dogo kaja kwa mbwembwe tumtazame kwanza ataishia wapi.

Projectile+motion.jpg


Mwendo ukawa ndio ule ule muhuni nikigusa tu maswali ya examples ya mwalimu napasua tena kwa muda mfupi tu.Na kwa jinsi nilivyokuwa na mbwembwe ilikuwa mtu akiniletea swali la projectile naliweka kwenye calculator lote then nikipiga alama ya sawa sawa kitu imooooo.Wenzangu wakawa wananiambia dogo fanya moja moja kupunguza brackets maana zitakuchanganya,ila kwakuwa nataka kuonyesha mimi ni kichwa sichanganywi nikawabishia na kuweka lote.

Aiseee nilikuwa mpenda sifa hatari enzi hizo kushinda hata BASHITE,nikasema likizo hii watanikoma mchikichini huko ndio nitakuwa nasolvia watu kwenye mabanda ya mihogo wakati wa kusubiri pindi .

Dah maisha yanaenda kasi sana na hatimaye nikapewa habari njema na mwanangu mmoja hivi kuwa kwa mgote jumamosi ni mtihani wa PROJECTILE MOTION hivyo nenda kawaonyeshe aisee kuwa wewe ni mwamba Dar nzima.Nikajawa na sifa kama kawaida yangu na kuwaza mda wote kuwa jumamosi inachelewa aisee nikafanye maajabu mchikichini huko.

SIKU YA MTIHANI WA PROJECTILE MOTION IKAFIKA

projectile_motion_prob_2.png


Kwa kujiamini kabisa nikakaa seat ya mbele kabisa maana nilikuwa sitaki mtu anichungulie tusije tukagongana marks tukawa wote wa kwanza wakati mimi nimetumia nguvu kubwa sana na nimekamia show.

Sitasahau hii siku hasa pale nilipoufungua mtihani wa PROJECTILE MOTION na kukutana na Concepts mpya ambazo sijawahi hata kuhisi kama nazo ni projectile aisee.

Kusoma swali hata halina terminologies ngumu kuelewa ila isipokuwa sina cha kuandika baada ya kulielewa lile swali.Hahahah formulas zangu za RANGE na Maximum height zote hazitumiki na ndio nazitegemea sasa hapo.

Ule mtihani na mimi tulikuwa level tofauti kabisa ambapo ni sawa na mwanafunzi wa darasa la kwanza aliyejifunza hesabu za kujumlisha namba zenye tarakimu moja then umtolee hesabu za magazijuto.

Ule mtihani haukuwa standard yangu japo majirani zangu wanaagiza karatasi za kujibia tu baada ya kujaza za mwanzo.Muhuni natamani nisikusanye niondoke hivyo hivyo ila sasa Mgote anayesimamia mtihani ndio kakaa mbele yangu kiasi kwamba hata nikigeuza jicho tu ananiona ,hhahah noma.

Nikakutana na concepts za kitu kina kuwa projected kutoka kwenye gari linaloenda kwa speed fulani na kitu chenyewe kina speed yake aiseee.Wakati huo air unaambia inaspeed yake then natakiwa kutafuta umbali kitakapotua kutokea umbali ambao gari lilikuwepo wakati wa kurushwa.

material-YTA5u3DP.png


Kila nikiangalia naona nashindwa hata kuchora mstari wa range maana kitu kilirushwa kikiwa kwenye height fulani above the ground.

Kiukweli hilo ndio baadae nikaja kugundua lilikuwa swali rahisi kuliko mengine.Hayo mengine ilikuwa balaaa tupu maana hadi ndege wa angani waliokuwa wanatembea walipishana na hiko kitu walichokiproject tena kwa speed tofauti.

Mfano swali lingine lilikuwa linaanzia mbali kinouma kuwa ,ball imeenza kuserereka kwenye umbo lina shape ya U na kuibuka juu na kuendelea na projectile motion na mara gafla ukagongana na body nyingine huko juu hivyo nitafute velocity waliyogongana nayo halafu unapasuka then kipande kimoja kinaondoka kwa speed yake na kingine kwa speed yake (data zingine ziliwekwa)

Hapo ndio Deadbody nikanza kushtuka kuwa hata ndege na hewa zinaweza kutumika kwenye projectile motion kumbe.

curv_proj_ep2.png


Aisee nilijiona mweupe sana kichwani na hakukuwa na uwezekano wa mimi kupata 1/100 ule mtihani.

Nikasema isiwe shida,maana kukusanya pepa nyeupe ni aibu acha nijitoe ufahamu nitafute range na maximum height ambazo hazijaulizwa nitapate pa kuondokea nyumbani.

Utaratibu ulikuwa simple sana ,yani ukifanya mtihani week hii,majibu yanatoka week ijayo na sikurudi tena huko mpka dk hii napoandika mada hii sijui ule nilipata A au B na sitaki kujua.

NIKAANZA MAISHA MAPYA



Kama principle ilivyokuwa ,ukiona umeshindwa kushinda nao basi ungana nao.Nikaanza kusoma Physics upya mchikichini na nikagundua nilikuwa sijui chochote aisee maana hata circular motion ingeniumbua.
Dah ngoja niishie hapa aisee maana mzuka ukipanda nitaanza kutoa matusi humu kuhusu Newton Rings (Wave 2 ) na madude ya mule..

NAJUA WATU KAMA MIMI WAPO WENGI HUMU,NAOMBA LEO TUJARIBU KUKUMBUSHIA HUYU MNYAMA 'PHYSICS'

KARIBUNI

cart.gif
Hahahaha nomaaa sana huyu mnyamaaa acha kabisa
 
Ile ngoma bana "Physics" , hata mimi niliingia 5 na mbwembwe kama za mtoa mada. Ila ponea yangu ilikua ni Geophysics na heat, I end up with E ya Phyics.

Nikaona ujinga huu kumeza formula za kina Mgote, kwa speed ile ya mwanga, Chuoni nkagonga zangu Accounts mterezo kabisa with ka upper second kangu. Na maisha yanaendelea sasa.
 
Mimi nilisoma PCM. Rafiki wa dingi alikuwa mwalimu wa physics akaniambia ukitaka utoboe advance physics kuwa serious na practical ..niliufuata ushauri wakse na nikatoboa
Kwa wale Pond Boys vijana wa babu Nzoi watakubaliana na mimi kwamba practical ndio zilitutoa. Mimi mpaka kesho naamini kabisa practical ndio ilinipa E, vinginevyo nilikua nataga pale.

Ndo hapo nilipo amua kubadili muelekeo chuoni, mzee wangu mmoja alinishauri niachane na Physics chuo nipige Accounts nikamsikiliza. Sitokaa nijutie ushauri wa mzee huyu mpaka mwisho wangu.
 
Mkuuuu niseme test ya kwanza ya phy nilipata 28 ya 100.

Kusoma PCM PCB PGM ,alafu uliingia bila twiti ,Phy atabaki kua mchawi anaywhitaj dawa madhubuti
====
Ebu fikiria mtu hajasoma Advance(Physics), halafu anaenda mbele huko ,na physics yake ya O-level, anakumbana na Static (course II) baadaye Dynamics(course II) mwishowe anakumbana Thermodynamics(III). Hizi kozi ni application ya hiyo physics yenu ya Advance. Yaani mtu anajichimbia masaa 4 anashindwa kusolve swali ambalo ni mfano kwenye kitabu....Almanusura kichwa 'kipasuke'... Wakuu nadhani mnanielewa.... !
 
====
Ebu fikiria mtu hajasoma Advance(Physics), halafu anaenda mbele huko ,na physics yake ya O-level, anakumbana na Static (course II) baadaye Dynamics(course II) mwishowe anakumbana Thermodynamics(III). Hizi kozi ni application ya hiyo physics yenu ya Advance. Yaani mtu anajichimbia masaa 4 anashindwa kusolve swali ambalo ni mfano kwenye kitabu....Almanusura kichwa 'kipasuke'... Wakuu nadhani mnanielewa.... !
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
====
Ebu fikiria mtu hajasoma Advance(Physics), halafu anaenda mbele huko ,na physics yake ya O-level, anakumbana na Static (course II) baadaye Dynamics(course II) mwishowe anakumbana Thermodynamics(III). Hizi kozi ni application ya hiyo physics yenu ya Advance. Yaani mtu anajichimbia masaa 4 anashindwa kusolve swali ambalo ni mfano kwenye kitabu....Almanusura kichwa 'kipasuke'... Wakuu nadhani mnanielewa.... !
Hapo lazimauzungushe Mkuu
 
Hapo lazimauzungushe Mkuu
Tangu kipindi hicho nilitambua kuwa kumbe Mungu ni kweli uwatendea miujiza watu wanaomuamini. Yaani jamaa alichomoa /alifaulu masomo yale na sasa kabobea kwenye field inayohusisha hizo Applications za Advanced Physics.
 
Nikikumbuka physics nakumbuka advance iyunga, RIP mr doppler, maana mbaba siku ya doppler effect anatiririka mpka unasema dah aya bwana, kwakweli adv physics ilinifanya mbaya iyungani sinaga hamu nayo mazee inakufanya ukose muda wa kupambana na mikate ya bios na chems, ukirudi chem wakutana na mr sudi azingua balaa n prac zake dah
Did Mr Doppler died??
Pole kwa familia yake.
Nimesikitika aisee.
 
Physician in nature sisomu kwa mateso nasoma kidogo kwa uelewa kisha nafunika kitaby mtihan unafika nagonga banda tatizo kwa somo la physics kwa walio wengi ni connection kati ya kitu kinachozungumziwa na kitu halisi kwa zamani ilikuwa sawa lakin kwa sasa technolojia kidogo imekuwa hatusumbuki sana na hili somo wajanja tunaelewa
 
Kwa wale Pond Boys vijana wa babu Nzoi watakubaliana na mimi kwamba practical ndio zilitutoa. Mimi mpaka kesho naamini kabisa practical ndio ilinipa E, vinginevyo nilikua nataga pale.

Ndo hapo nilipo amua kubadili muelekeo chuoni, mzee wangu mmoja alinishauri niachane na Physics chuo nipige Accounts nikamsikiliza. Sitokaa nijutie ushauri wa mzee huyu mpaka mwisho wangu.
Wazee wa pond ( Pugu) .....pcm pcb wengi wameishia kwenye accounting
 
Huu uzi umenikumbusha practicals ambapo data zilikua hazileti majibu tarajiwa na kusababisha watu kufanya mapishi ya data.
 
Hahahahah shule yenyew O-level tulkuwa tunagonga Engineering Science badala ya Physics.....so ulikuwa ukichaguliwa Iyunga advance kama ulkotoka ulkuwa unabahatisha hakuna muujiza wa kutoboa.....ukigeuka kushoto unakutana na LE MUTUZ la Chemistry....Mr. SUDI.....***** mzee ana roho mbaya huyo.....kinyama.....

Umenkumbusha mbali sana kwa IYUNGA......
Mr SUDI mzee wa cattle boma. Aisee alikua mzugaji htr ni story za ng'ombe na fomula ya asprin. Kasansa na Doppler walitusogeza knm japo amefika tupo second term. Ila Doppler kaikanyaga sana physics yye notes tu ukiuliza swali anakuambia utaenda kuelewa prepo dah!
 
Wazee wa pond ( Pugu) .....pcm pcb wengi wameishia kwenye accounting
Yaani mkuu kwenye uhasibu ni Dr & Cr deal done. Haina mbwembwe kama za projectile, chamsingi uwe smart kwa monthly reports.
 
Aisee yani hii thread kama inanihusu vile . kipindi Niko o level nlikua naipenda physics acha kabisa mpaka niliapa kabisa kama sita kwenda kusoma advance kama sita chaguliwa combination yenye physics . Basi bwana selection zilivo toka nikawa nimechaguliwa PCB nikaona huo ndo mchongo. Nlipo enda sasa kujiunga a level mzee baba nikawa nasoma physics kwa asilimia 80. Nikawa nawasovia washkaji maswali kinyama masela wangu wakawa wanakaza sana kwenye Chem na bio Mimi ni physics labda na chemistry sanasana ika bio kwaumbali. Nilisolve karibia maswali yote
ya physics kwenye vitabu kadhaa nikajiona Niko fiti kinoma. nikawa nasubili paper tu ilinije nilikamuekamue kiunyama. Heeeeee haki yamungu nilikamua paper 1 nikaja paper 2 nikamalizia na paper 3B ( practical) mwanangu nakwambia nilikua nazijua karibia practical karibia zote za phy Lakini ile sitakuja kuisahau. Ilinigonga mwanzo mwisho nilitika kwenye mtihani nimekua mpoleeeeeee nikawa sins swagga kabisa. Subiria matokeo sasa. Pale ndo niliamin kabisa physics ipo ili iaibishe watu- yaani sikuamin kabisa alicho nifanyia mnyama yule- ndugu zanguni nihatari kabisa
 
Back
Top Bottom