Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Magnetism mpka naondoka adv, sija wahi igusa !


Wave , electronic, modern physcics, heat, ndo zilikuwa topic zangu,

Mungu si athumani
Nikapata F ,
Hahahaha aise hii kitu balaa,Mimi nilipiga tuition nikaanza na projectile baada ya wiki nikaanza kukwepa vipindi na topic ilikua ni 20 Amber center.Baada ya kujitathimini nilienda arts hadi leo baadhi ya watu hawaamini kama nilisomaga arts.
 
Umenikumbusha milambo 2010 nikiwa six ticha phys alikuwa mweupe had tukuwa na concept
kwangu physics ilikuwa kitonga kuliko biology
 
Hili somo ni la kiume linaoa watu wa jinsia zote. Physics acha kama ilivo
 
Physics ina makusudi sana na maswali yake kwenye pepa...niliingia pepa necta ilo swali la projectile limetungwa kama visa yani unasoma swali kama story.

Eti Dogo moja yupo ghorofani anataka kumrushia Mpira mwenzake yupo ghorofa ya pili, Bahati mbaya si akakosea Mpira ukagonga ukutani yani haukifika kwenye target...basi mpira mpira ukadunda ukagonga ghorofa la kwanza ukagonga tena ghorofa la pili halafu ukadondoka chini...Hapo inatakiwa utafute umbali Mpira ulipodunda chini kati ya ghorofa ya kwanza na Mpira ulipotua.
 
Haha mnyama phys aisee tulikua tunapoteana sana kwenye mitihani ila kwenye discusion mambo yalikua yanapanda sema sikuwahi kusoma practicals ila theory Nlikua popoa sana

Physics ni kama baskeli tu ukiiweza ata ulaya unaendesha hahaha haka kakauli niliambiwa wakati niko o level

Kipindi hicho anakuja teacher class alafu anasema anaona watu 12 tu watakaoweza mziki wa pcm adv haha
 
Kwakifupi somo gumu kuliko yote duniani ni physics
Inategemea na MTU Mkuu me chemistry ilikua ngumu sana mpaka kesho hata university nilichagua coz ambayo mambo ya chemistry hayatakua mengi sana kama watu Wa chemical and processing Eng

Maana kuna kitu organic hahaha ilikua jiweee la fatuma mkuu mambo ya kuvunja bond dadeki nlipoteana vibaya mno
 
Yaan hata kuitaja tu Phys naogopa sio kwa mziki ule haiwezekan leo napiga maswali yote at nekti wiki sikumbuki hata iyo Rotation cjui Wave na Matzmu...
 
Jaman Advanced Physics kiboko sitasahau maisha yangu yote.
 
mh mi napita Tu wakuu maana phy Ni weka mbali na watoto haiuzwi chin ya umri
 
niliisoma nikaielewa na kuipenda na hata ku tacle maswali kwa asilimia 85..
lakin ilivyonifanya necta, ni sili yangu..
nilifaulu ila sio kwa kiwango nilichokitegemea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha Daaah physics ni balaa Kuna T.O mmoja hivi alimaliza 2006 alikuja Kutufundisha sisi tukiwa form 6 tukajiona Vilaza Wote.. vitabu vya Chand...Roger. vyote tuliona Tumemaliza na Hakuna Swali Gumu.. Jamaa Halafu alikuwa ana dharau balaa na Chuo alifukuzwa Kisa Dharau kwa Maprofesa kwahiyo akabak anapiga Tuition mtaani tu na Sifa Kibao na Kuwaona Watanzania wote hawana Akili ila Yeye peke yake

Ila Nakumbuka Siku ya Mtihani wa Physics Nilipiga msuli Usiku halafu kesho yake Pepa Asubuhi Na Nikasolve Maswali Kama matatu hivi ya Chand kwenye Pepa Yamekuja Vile vile Nikasema Nashukuru Mungu Ndalichako kaniona

Ila Yote tisa nitarudi Shule Zote ila Siyo Advance
[emoji23] [emoji23] [emoji23] mwenyewe shule advance siitamani tena,,,ata wanipe hela hapa...msuli tembo matokeo sisimizi[emoji23] [emoji23] mambo ya tranter,understanding, pure uwiii[emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom