Aeleza walivyokubaliana na mume wake kutafuta watoto nje ya ndoa

Aeleza walivyokubaliana na mume wake kutafuta watoto nje ya ndoa

Ndoa ivunjwe kwa sharti la kutogawana mali.
Hicho ndo Kullaya nafikiri kinampa ugumu wa kusema hayupo tayari kutoa talaka. Ila kwa busara naona huyo mwanamke akubali tu hilo sharti la kuvunjwa ndoa bila kugawana mali ili akafunge ndoa na huyo bwana wake mpya kwani huyo bwana mpya si atafute mali.
 
Yani nijikute tuu tena nakaa nakubaliana kitu na mke wangu,kitu serious

ah weee labda hiyo ndoa tuwe tumeshafikisha 30yrs ila chini ya hapo hii

kichwa yangu itaamua future ya maisha yangu,Hapo mwanamke ana amani tele

kimbembe n kwa huyo bwana mkubwa hapo,atasota sanaaa kukubali matokeo kuwa ndio kashapgwa K.O tena..
 
Yaani kuna watu wanazichezea na kuzinajisi ndoa hadi unashangaa kumbe ambacho hawakujua ni kwamba ndo hazichezewi na sasa ndoa yenyewe imegoma kuchezewa imeamua kujitetea
 
Mnasimulia bongo movie au? hivi unamruhusu vip mkeo akatafute watoto kama bidhaa?
 
Kesi ngumu hii,ila kuna kifungu kinachosema kama wanandoa wameshakaa zaidi ya miaka 3 bila ya kuwa pamoja,ndoa inaweza kuvunjwa,sasa sijajua hapo wanasheria wanadadavua vipi.Ila hapa kuna cha kujifunza kuwa michezo mingine sio ya kujaribu...
Miongoni mwa sababu kuu za kuvunja ndoa ni uzinzi na mwanandoa kubadiki dini. Hapo wote wamezini hata km walikubaliana.
 
Mwanamke ameshanogewa huko aliko na anaona ni mahali salama for her lifetime. mwanaume bado anataman aendelee kuishi nae. Patamu hapo.
 
Kesi ngumu hii,ila kuna kifungu kinachosema kama wanandoa wameshakaa zaidi ya miaka 3 bila ya kuwa pamoja,ndoa inaweza kuvunjwa,sasa sijajua hapo wanasheria wanadadavua vipi.Ila hapa kuna cha kujifunza kuwa michezo mingine sio ya kujaribu...
Mkuu hapo wala hakuna ugumu sheria ipo wazi
Separation more than 6 months tayari
Pia sheria haitambui makubaliano binafsi hapo ni adultery kama ilivyo zingine
 
Wakuu katika pita pita zangu nimekutana na hiki kisa.

Dar es Salaam. Mkazi wa Tabata Liwiti, Magreth Silaeli (37) ameieleza Mahakama ya Mwanzo Buguruni kuwa walikubaliana na mume wake, Raymond Kulaya (44), waachane kwa muda ili kila mtu akatafute watoto “anapopajua” baada ya kuishi miaka mitano bila kupata mtoto.

Magreth sasa anaiomba mahakama itoe hati ya talaka, ili aweze kuolewa na mwanaume anayeishi naye, baada ya kutengana kwa muda na Kulaya.

Alidai mbele ya hakimu Matrona Luanda kuwa yeye na Kulaya walitengana tangu mwaka 2011.

Alidai alifunga ndoa ya Kikristo na Kulaya mwaka 2006 mkoani Kilimanjaro na waliishi pamoja kwa miaka mitano bila kupata watoto.

Magreth alidai wakati anaolewa na Kulaya alimkuta tayari na watoto wawili, lakini katika kipindi chote walichoishi pamoja hawakubahatika kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 mume wake alimueleza kuwa wamekaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na watoto na kumwomba watengane ili kila mtu aende akatafute watoto.Alidai katika kipindi walichoishi pamoja, familia ya ndugu wa mwanaume ilikuwa inawasumbua kuhusiana na watoto na kuwasababishia kukosa raha.

“Mimi nilikuwa naumia sana kwa kuwa nilikuwa sijapata mtoto, angalau mwenzangu nilimkuta na watoto wawili, mwishowe mume wangu aliniambia tutengane kwa muda ili kila mtu aende akatafute watoto anakojua,”alidai Magreth

Aliiambia mahakama kuwa kutokana na kutopata mtoto, Kulaya alimweleza kuwa ni bora kila mtu aende upande mwingine kwani atakapoleta mwanamke mwingine ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja hataweza kumuelewa.

“Mimi nilienda kuishi na mwanamume niliyenaye leo na tumebarikiwa kupata watoto wanne,” alisema.

Magreth alidai yeye na Kulaya walitengana kwa makubaliano hawakuwahi kuwa na ugomvi na sababu kubwa ya kutengana ilikuwa kukaa muda wa miaka mitano bila ya kupata mtoto.

“Kwa kuwa mwanaume ninayeishi naye alinikubali na aliniliwaza wakati nikiwa katika hali ya unyonge na nimezaa naye watoto wanne, naiomba mahakama hii itoe talaka ili mimi niweze kufunga ndoa na mwanaume niliyezaa naye,”alidai Magreth.

Kwa upande wake, Kulaya ameieleza mahakama kuwa aliishi na mke wake Magreth kwa miaka mitano na hawakujaliwa kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 yeye na Magreth walijadiliana na kukubaliana watengane kwa muda ndipo mke wake alipata mwanaume ambaye alizaa naye watoto wanne huku yeye akizaa na mwanamke mwingine watoto watatu.

“Yaani mimi nipo tayari hata leo hii mke wangu nirudiane naye na sina chuki naye na ninawakubali watoto wake nitawapokea, hivyo naiomba mahakama hii itakapotoa maamuzi yake itumie busara kwa hili,”alidai Kulaya. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 17, 2021 kwa ajili ya hukumu.



Watanzania wengi hatuko sawa
 
Nashindwa hataa cha kuandika ila utafute hiyo habari tushacomment
 
Sijaona la ajabu hapo maana sheria inaruhusu kutangana au kuachana mnapoona tatizo kwenye ndoa yenu. Wao walichagua kutengana ili wakisolve tatizo lao warudiane, ubaya uko wapi? Ndoa ni maelewano jamani.
 
Huyu jamaa vipi?,kwanini asimwache huyo mwanamke aolewe?..si yeye ndo alimwambia kila mtu akatafute mtoto kivyake na mwanamke kawapata wanne,,sasa nini cha ziada hadi kulazimisha arudi kuishi naye?
 
Back
Top Bottom