Kwani hujasikia Kuwa uchunguzi unaendelea?

Uchunguzi kuenddelea sio sababu ya kuzuia maandamano. Maandamano ni haki ya kikatiba na sababu ya maandamano sio lazima iwe ya msingi kwa wengine! Polisi hawapewi hata sababu kisheria ni kupewa taarifa tu.

Pili uchunguzi wao haunaga kikomo mpaka leo waliompiga risasi Lissu eti uchunguzi unaendelea. Usije kujidanganya na kufikiri unasaidia nchi kwa kushabikia kila kitu hili ni swala la kitaifa tunaenda pabaya na wazee wote wamesema hivyo juzi naona vijana kila kitu ni masihara
 
Akili ni nywele kila mtu ana zake nadhami mdio msemo wanaotumia polisi wetu.

Ilitokea naandamano ya wananchi wengi kila mkoa kweli wataweza kudhibiti!

Mifano ni kwenye nchi za kiarab yaliyopelekea Serikali zilizokuwepo kuondolewa.
 
Baki kwako ugongane na mumeo.
 
Sioni shida kusoma maoni yako maana hata mpumbavu naye ana haki ya kusikilizwa
 
Wakati anatoka kwao Musoma kuja mjini sisi ndio tulimpokea, asiote Mapembe kwa vyeo vya kuteuliwa, ajiulize wale walioteuliwa na Jiwe leo wako wapi?
 
Hakuna demokrasia isiyo na mipaka
Demokrasia bunayoitaja haitekelezeki sehemu nyingi Duniani.
Ni njia tu ya kulinda maslahi fulani ya waliowahi kuona mbali huko Duniani.
Afrika na Tanzania Kwa upekee Ina mfumo wake wa kiutawaka na siyo huo unaoitwa Demokrasia.
 
Safi sana Mbowe watu watatekwa na kuuawa mpaka lini. Nitaandamana nifie kwenye maandamano ili nizikwe kwa heshima kuliko Soka na wenzake ambao hata maiti zao hazijulikani zilipo
 
Hii nchi ingekuwa ina amani watekaji wangeshikwa au kuuwawa ndani ya Lisaa lomoja pindi wafanyapo unyama wao
Kwahiyo asitokee mbuzi yeyote kujifanya mlinda amani huku akiwa sirini anaiharibu
 
Lucas Mwashambwa Kamanda Murilo kwenye eneo lake la usalama 'DSM' mtu anatekwa mchana mweupe na siku ya tatu anakutwa kauwawa, leo tunaingia wiki ya pili hakuna mshukiwa hata moja aliyekamatwa. Chukulia Lucas Mwashambwa kama marehemu Mzee Kibao angekuwa ni mzazi wako? Mambo mengine yasikie tu kwa wenzako. Kifo cha ghafla kinauma sana tofauti na kile umeuguza kwa ugonjwa mpaka imeshindikana. Na wewe Lucas Mwashambwa unapenda sana kumtajataja Mungu sijui huwa unamaanisha au laa.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…