Afande Muliro: Jeshi la Polisi limewachukua 'Watu kadhaa' katika Kanisa la Askofu Gwajima

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema Jeshi la Polisi linawashikilia Watu kadhaa kutoka katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo kutokana na kile alichoeleza kuwa walikuwa wakizuia Jeshi hilo kutekeleza majukumu yake.

Wakati tukielekeza nini cha kufanya, kuna baadhi ya Watu walifanya mambo ya kutoelewa, ilibidi tuwachukue na tunaendelea kuzungumza nao kujua kweli walikuwa hawaelewi au walikuwa wanakataa tu ili kusababisha fujo”

“Sisi jukumu letu ni kuona kwamba tunaitekeleza ile sheria na kusimamia kuona kwamba kilichoelekezwa [na Ofisi ya Msajili] basi kinatekelezeka na kutekelezwa kwake ni kutoendelea kufanya zile shughuli zilizokuwa zikifanyika [kanisa la Askofu Gwajima].

“Kama akitaka ziendelee kufanyika basi afuate utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwenye mamlaka za kisheria zilizowekwa. Lakini kwa sasa tunatekeleza kile ambacho ni cha kisheria cha mamlaka iliyowasajili ambayo tayari imesitisha shughuli zao."

CHANZO: Wasafi FM
 
Kama ni kutekeleza ko wakiambiwa waue hadharani wataua!? Au wakiambiwa wale vinyesi watakula!? Yaan hawana hata ile common sense ya vidudu 🤢 🤮
 
Hivi wengine huwa mnawaza kwa kutumia masaburi? Lini kahamasisha vurugu? Leta hapa ushahidi. Kasema watu waache kutekwa. Kwahiyo kusema watu wanatekwa ndiyo vurugu? Anayeuwa na anayekataza kuuwa nani mleta vurugu?
Eti! Kosa hasa la Gwajima ni nini? 😳

20250602_101130.png
 
Back
Top Bottom