Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema Jeshi la Polisi linawashikilia Watu kadhaa kutoka katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo kutokana na kile alichoeleza kuwa walikuwa wakizuia Jeshi hilo kutekeleza majukumu yake.
Wakati tukielekeza nini cha kufanya, kuna baadhi ya Watu walifanya mambo ya kutoelewa, ilibidi tuwachukue na tunaendelea kuzungumza nao kujua kweli walikuwa hawaelewi au walikuwa wanakataa tu ili kusababisha fujo”
“Sisi jukumu letu ni kuona kwamba tunaitekeleza ile sheria na kusimamia kuona kwamba kilichoelekezwa [na Ofisi ya Msajili] basi kinatekelezeka na kutekelezwa kwake ni kutoendelea kufanya zile shughuli zilizokuwa zikifanyika [kanisa la Askofu Gwajima].
“Kama akitaka ziendelee kufanyika basi afuate utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwenye mamlaka za kisheria zilizowekwa. Lakini kwa sasa tunatekeleza kile ambacho ni cha kisheria cha mamlaka iliyowasajili ambayo tayari imesitisha shughuli zao."
CHANZO: Wasafi FM