Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Afande sele kawashangaza Sana mamilioni ya watanzania ambao wanaendelea kuhoji kuwa Ina maana Afande sele hajaona ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani alivyojenga na kuboresha secta ya Elimu hapa nchini? Watanzania wanahoji kuwa Afande sele amesahau Mara hii namna watanzania walivyokuwa wanahaha kulipa michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Hadi wengine kukimbia Kaya zao?
Wanauliza je, hakuona mh Rais wetu mpendwa akitoa fedha kwa ajiri ya kwenda kujenga vyumba vya madarasa kila shule? hakuona miaka ya nyuma wengine wakienda muhula wa pili kuanza masomo yao kwa kuwa tu hakukuwa na madarasa ya kutosha? Je wangekuwaje sawa na waliolipoti mwezi wa kwanza?
Wanauliza Kwamba huyu msanii hajaona namna uamuzi wa serikali wakufuta Ada ya kidato cha tano na sita ilivyoweza kuwasaidia watoto wa wanyonge kupata Elimu bila shida? Wangapi walikuwa wanashindwa kuripoti shule kwa kukosa Ada? Je haoni Jambo hilo limeleta neema kwa familia masikini? Huyu msanii haoni kuwa hizo Ni faida za Tozo zetu?
Huyu msanii kwamba hajaona namna zahanati na vituo vya Afya vilivyosambazwa kila Kona ya nchi hii ndani ya muda mfupi wa Rais Samia? Kwamba hajaona wananchi walivyopunguziwa adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za Afya? Haoni suala Hilo limesaidia hata wamama wajawazito kujifungulia hospitalini na hivyo kupunguza hatari ya kutokea kwa vifo vya mama na mtoto?
Huyu msanii haoni namna huduma za maji zilivyosogezwa Hadi vijijini na hivyo kupunguza Ile kero ya watu kuamka alfajiri kutafuta maji toka kilometa kadhaa? Anadhani pesa hizo zimetoka wapi? Au alitaka watanzania waendelee kuhenyeka kufuata maji umbali mrefu?
Huyu msanii hajaona juhudi za serikali kuinua maisha ya mkulima kwa uamuzi wake wa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini? Haoni namna ambavyo kwa Sasa mbolea inapatikana kwa Bei nafuu ya elfu 70 kwa DAP ambayo msimu uliopita iliuzwa kwa laki na 40? Haoni Jambo Hilo litachochea uzalishaji kuongezeka msimu ujao! Haoni kuwa uchumi wa mkulima unakwenda kuinuka hasa ukizingatia Ni secta iliyo ajiri kundi kubwa la watanzania na ndio pumzi ya watanzania wengi
Hapana siyo kuwa haoni Bali kaamua tu kujipa upofu na kufanya upotoshaji kwa umma ambao hata hivyo umempuuza tu, watanzania hawamshangai maana bado wanakumbuka kuwa amewahi kuvua nguo jukwaani,kwa hiyo wanaona anatatizo linalohitaji ushauri wa kisaokolojia
Watanzania wanaendelea kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa, maana wameona juhudi zake katika kuijenga nchi yetu na maendeleo yaliyopatikana na namna yalivyogusa maisha ya watanzania kwa kupunguza kero zilizokuwa kidonda ndugu kwao
Watanzania wanasema Tanzania itajengwa na sisi watanzania, hatuwezi tukakaa tu ili wenzetu walipe Kodi na Tozo huko kwao halafu sisi tuletewa huku, Hatutaweza Kuendelea na aibu hiyo, Sasa Tumeamua kuijenga Tanzania yetu na mh Rais wetu mpendwa Samia ameongoza njia hiyo na watanzania tunamuunga mkono
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania walipo