Afande Sele: Magufuli alikopa na kufanya makubwa, sasa hivi wanakopa na hakuna linaloonekana

Afande Sele: Magufuli alikopa na kufanya makubwa, sasa hivi wanakopa na hakuna linaloonekana

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757

"Unajua kwenye each one teach one hatupingi mikopo, lakini tunapinga aina ya mikopo na kile ambacho kinatumika kupitia hiyo mikopo. Yaani, hiyo mikopo ina impact gani kwa wananchi inayoeleweka. Ni kama vile wewe umeenda kwa bwasheee kukopa unga au mafuta kwa sababu watoto wako wale"

"Sasa wewe unakopa halafu watoto wako bado wanakaa na njaa, sasa wewe umekopa ya nini? Tunasema nchi kubwa zinakopa, Magufuli alikopa, lakini Magu alipokopa tuliona. Miradi ya kimkakati mikubwa alijenga, mipya akaianzisha, ya zamani akaiboresha, ma reli yaliyokufa miaka na miaka yanayoenda huko Arusha kayafufua, reli kigoma inaishia Dodoma kaifufua mpaka Dar es salaam, akajenga na reli mpya, miundombinu ya umeme akaanzisha na mambo mengi mengi alifanya kwa muda mfupi aliotumikia nchi hii."

"Ko tunasema, ok alikopa lakini alifanya hiki. Ila kwenye kukopa kwake pia Magufuli hatukuona tozo zikiongezeka, hatukuona makodi ya ajabu ajabu, yaani tuliona kwamba mambo yanakwenda hata kwenye kipindi cha CORONA, kipindi kigumu dunia nzima imefungiwa ndani yeye bado aliendelea kupambana."

"Hatukuona matozo wala makodi ya ajabu yakiletwa nchi hii"
 
Mkuu kumbuka kuna kurudisha mikopo. JPM alikopa mikopo ya kibiashara ya muda mfupi na riba kubwa. Sasa hiyo mikopo inatakiwa kurejeshwa na miradi yoote mikubwa aliyoanzisha kuanzia ununuzi wa midege, SGR, bwawa la umeme n.k hakuna hata mmoja umeweza kurudisha hata shilingi. Mambo siyo rahisi kama tudhanivyo.
 
Hawa matahira wanashindwa kujua kuwa mikopo aliyokuwa anakopa magufuli Ni ya riba kubwa na ya muda mfupi, yule mzee alichokosea alikuwa sio mkweli,aliwadanganya haya matahira yakahamini kweli miradi Inajengwa kwa fedha za ndani.
 
Back
Top Bottom