Afande Veronica yupo barabarani kukusanya hela au kufilisi Raia?

Afande Veronica yupo barabarani kukusanya hela au kufilisi Raia?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Polisi wana mbinu nyingi za kutengeneza mazingira ya Rushwa na kukupiga faini. Huwezi pona kwenye 18 zao, watatafuta kosa hadi walipate.

Sitaki kusema Chuo cha Polisi Moshi (CCP) hawafundishi ila nadhani wanatakiwa kubadili Mitaala yao. Kuna vitu wanavifanya Polisi wetu hadi unajiuliza huko CCP walienda kusoma Ujinga? Polisi wanatakiwa watoe huduma sababu ni Watumishi wa Umma.

Rais Samia kaongeza Mshahara ili mfanye kazi kwa Tabasamu, sasa hasira za nini?

Mfano: Kuna askari pale Stesheni (maeneo ya Central/TRA (kwenye Zebra)) ana watu wake wa kukatiza zile zebra ili apige watu fine. Anaitwa WP 4548 CPL Veronica, ayafanyayo anakosea na kudhalilisha Jeshi letu.

Unaweza kuwapisha watu, utakaa hadi waishe, ukianza kuondoka ghafla utaona anaibuka mtu na kutaka kukatiza zebra. Anafanya timing, Ukianza kuondoka anapita anakimbia na Vero anakupiga Mkono. Anakuwa na wenzake wawili. Unaulizwa Kwanini huheshimu watumiaji wengine wa barabara? Anakupiga fine.

Mimi ninahofu, wale jamaa wanatengenezwa? Kwanini wao tu ndo wakatize kwa kuchelewa siku zote?

Pili: Polisi wanatakiwa Wasimamishe Magari ili watu wavuke na wakishaisha wawaruhusu muondoke. Lakini wao wanasimama pembeni pale, Nyie madereva Mtajisimamisha wenyewe watu wavuke na wakishavuka mnajiruhusu wenyewe. Hapo ndipo kwenye mtego wa kuliwa hela.

Polisi tunaomba msaada wenu, mtusaidie muwapo kazini. Sababu Polisi kazi sio kupiga fine tu bali hata kutoa elimu ya barabarani kwa watumiaji wa barabara.

Polisi na Raia ni Ndugu, tushirikiane. Tusiishi kama paka na panya.
 
Wanachukua ya kubrashia mokasi wewe wape tu ndio chanzo chao cha mapato binafsi
 
majungu tu unaleta hapa.

kubeba jina zima la mtu anayekuhudumia eti una malalamiko naye ni uzwazwa.

watu watajuaje kama huna visa naye!!!
Hapo ulipo unaweza kuwa hata pa kulala hauna. Ukitaka kujua adha ya polisi trafiki miliki gari Dar ndio utawajua hawana hata chembe ya utu. Wao ni rushwa tu. Hiki kinachosemwa ni ukweli mtupu.
 
Acha majungu jomba hao watu hawana kazi ya kufanya mpaka wawekwe na polisi kuvuka zebra.
najua utaanza kusema tushajua una gari
basi nikuambie mie dereva tu nawaandesha WAHINDI mshahara 250000/=

haya turudi kwenye MADA kama sio dereva huwezi kujua adha ya TRAFFIC anachosema ndio kipo na hiyo MICHEZO sio hapo tu ipo sehemu nyingi.

Usione watu wajinga walipofurahia yule TRAFICC morocco aitel kuporomoshewa MITUSI ya nguoni na dreva daladala.

Hao jamaa ni wapuuzi AKILI zao zimejaa pesa zaidi kuliko kuongoza magari
 
Iyo pesa una pewa risiti au mna yamaliza kimya kimya tuanzie apo kwanza
 
Hapo ulipo unaweza kuwa hata pa kulala hauna. Ukitaka kujua adha ya polisi trafiki miliki gari Dar ndio utawajua hawana hata chembe ya utu. Wao ni rushwa tu. Hiki kinachosemwa ni ukweli mtupu.
sasa gari moja unakuja kupiga kelele hapa!!!ushawahi sikia mwenye dala dala analia lia na traffic??

hela huna road unatembea kiwaki,lazima uliwe kichwa.
 
Kwenye zebra unatakiwa usimame bila kusimamishwa hata kama hamna mtu anaetaka kuvuka ukijiridhisha hamna mtu karibu ndo unaendelea na safari Kama hulijui hilo iko siku utapigwa faini kwa kupita kwenye zebra bila kusimama hata Kama hamna mtu ndo utashangaaa zaidi
 
Back
Top Bottom