Afande Veronica yupo barabarani kukusanya hela au kufilisi Raia?

Polisi na raia ni ndugu🤔
 
Mtoa mada leseni umeletewa nyumban, sheria ya zebra hujui na hujataka kujifunza sasa we utapigwa mabao mpaka akili ikukae sawa. Kwa wakati wako nakushauri nenda kasome ile sheria then urudi kwandika tena hapa.

Jamno kubwa nlogundua toka kwa mtoa uzi yuko na hasira flan na huyo askari na ni kitu ambacho ni kibaya. Mie nimepata kigugumizi unapotaka elimu , sasa kama askari atakuwa anakuelimisha chuo usingetakiwa uendee. Kama unataka elimu ya namna ya kutumia barabara rudi tena chuo kama umesahau😃 wabongo tuko na uelewa gani.

Acha upigwe faini mpaka ujue sheria hahah haaa ila pole sana mkuuu 😂😂😂
 
Na wanakubali kutoa maana wanamakosa kama mtu umekamilika unato ya nn labda utoe kwa mapenzi yako
 
Ndio michezo yao hyo....ingawa ni ngum kutengenisha Polisi na rushwa
 
M
ujamuelewa. Anacho lalamikia ni kwann kila siku ni naru wale wale wanaochelewa kuvuka/wanaotaka kuvuka gari likitaka kuondoka?
Mwongo huyo kuwa nayeye watu hao hao ndo wanajipitisha kwenye gari lake?
 
Yote majanga mkuu.

Hii ya kuandikiwa usipoitoa kwa wakati inazidi tu kupanda, ni bora ya rushwa ya kumalizana kuliko fine ya kuandikiwa.
Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanakesi ya kujibu
 
Polisi ni ndugu? Unajidanganya sana..
 
sasa gari moja unakuja kupiga kelele hapa!!!ushawahi sikia mwenye dala dala analia lia na traffic??

hela huna road unatembea kiwaki,lazima uliwe kichwa.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Waache wajiongeze tu
Mnataka waishije
Kila mtu ale kutokana na urefu wa kamba yake

Ova
 
Kuna member humu alishawahi leta kisa kama hicho,muda kidogo umepita.

Alikuwa morroco kama sikosei zebra,yupo mbele kabisa akasimama kusubiri watu kuvuka,wakavuka wakaisha akajiridhisha kuondoa gari.
Lkn pembeni kuna kijana alikuwa kasimama anaongea na simu alionekana ni mtu mwenye mambo yake.
Sasa wakati dereva anatoa gari yule jamaa akaanza na yy kutembea kuingia zebra,
Mbele kidogo askari akamwambia awake gari pembeni.
(Wakaanza kubishana)

Sasa kumbe nyuma ya gari yake pale zebra kulikuwa na boss mmoja nae ni askari mkubwa tu.
Aliusoma huo mchezo.

Akamwita yule mpita njia,akamwambia aingie ndani ya gari,wakaenda mpk karibu na pale walipokuwa wanalumbana Yule boss,akamhoji yule kijana hakuonyesha ushirikiano akamlima vibao kazaa pale ,dogo akasema wako pamoja na wale traffic.
Yule boss akamwambia dereva ondoka ,akamwambia yule traffic alopiga mkono na yule kijana wapande kwny gari akaondoka nao.

Sikumbuki jina la hyo thread ila hayo mambo yapo,na hicho kisa kipo humu kishasimuliwa.

Mi nasemaga kati ya watu ambao ambao hawataingia Mbinguni.
Wakwanza ni Polisi,Maafisa TRA na wanasiasa.
 
Acha majungu jomba hao watu hawana kazi ya kufanya mpaka wawekwe na polisi kuvuka zebra.
We kijana ni mtanzania au umetokea Congo?
Hao watu kazi yao ndio hio.
Na wanalipwa hizo pesa za Haramu na hao hao askari.
We unatetea upumbavu?

Kijana tafadhali sana.
Tena sana.
 
haiwezi kuwa sahihi hii
 
Mambo ya kushangaza yamejaa Nchi hii kuna mataa kule Mbezi kwenye Morogoro road taa za kijani zinaruhusu na hapa hapo Pedestrians wanaanza kupita inabidi usubiri wamalizike na Taa Nyekundu inawaka
Solution ni kuwawekea taa zao

Mji wa Bariadi Pedestrian crossing zote zinaongozwa na taa hapa Dar inashindikana nini?
 
Kuna wale walikuwa na mchezo huo pale round about ya kigogo, Yani wanaweka watu kama watatu ukitaka kuvuka tu wanapita na traffic wanakuwa pale mbele wanakusubiri, Kuna mama mmoja mchaga mchaga hivi balaaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…