Afariki baada ya kuanguka chooni kwa kupigwa stroke

Afariki baada ya kuanguka chooni kwa kupigwa stroke

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Wakati wa JPM alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akasota rumande miaka minne. Mwaka jana akaachiwa kwa NOLE. Aliporejea nyumbani akakuta biashara zake zimekufa. Mke ana mtoto mwingine aliyezaa nje ya ndoa. Mke anadai hakuplan ku-cheat ila changamoto za maisha zilimlazimisha. Baada ya kila kitu kuvurugika na maisha kuwa magumu alimpata "Sponsor" aliyekubali kulea watoto wawili wa jamaa akiwa jela.

Ni "sponsor" huyohuyo aliyelipia gharama za mawakili waliomtetea jamaa hadi kuachiwa huru. Sponsor alitunza familia ya jamaa, akamlipia mawakili, akahakikisha watoto wake wanaendelea kusoma English Medium na hawarudi shule za Kayumba. Akamfungulia mke wa jamaa biashara ya saloon ili aweze kujikimu kwa mahitaji madogo, akamnunulia gari.

Jamaa alipotoka alipata depresion ya maisha, ndoa, uchumi etc. Washkaji zake tulijitahidi kumrudisha sawa lakini it was a locomotive process. Mke alijitetea kwamba yaliyotokea hakukusudia. Aliahidi kukatiza mahusiano na "sponsor" na badala yake watawasiliana kwenye malezi ya mtoto tu. Lakini somo hilo lilikua gumu kwa jamaa.

Jamaa alikua muongeaji sana kabla ya kufungwa. Lakini baada ya kutoka jela akawa mtu mkimya na asiyependa kutoka. Mara zote hujifungia ndani akiwaza na kusoma vitabu. Washkaji zake tuligundua yupo kwenye msongo. Kuporomoka kwa uchumi na kuyumba kwa ndoa yake vilimuumiza sana. Tukaweka utaratibu wa kumtembelea mara kwa mara, kumtia moyo na mara chache kutoka nae out japo kwa kumlazimisha.

Kuhusu mtoto tulimwambia kitanda hakizai haramu. Kuhusu uchumi tulimwambia ajipe moyo atarecorver kwani hayo ni mapito tu. Tulikua tayari kumchangia mtaji kidogo ili aanze kujipanga upya.

Jana nikapata taarifa kuwa ameanguka bafuni. Inadaiwa alipata stroke na mishipa ya kichwa kupasuka. Damu ikavilia kwenye ubongo, akapoteza fahamu. Akakimbizwa hospitali lakini alipofikishwa, madaktari wakasema si yeye bali ni mwili wake tu. Malaika Israel alimtwaa njiani kabla ya kufika hospitali.

Nimeumia sana. Pumzika kamanda. Siku zako nje ya jela zimekua NGUMU SANA kuliko ulipokua jela. Naamini umemsamehe mkeo. Naamini pia umemsamehe JPM aliyevuruga maisha yako na familia yako. Lala salama mwamba. Tutaonana baadae.! 😭😭

Malisa GJ
 
Tumia akili ingekuwa ni msongo wa mawazo angekufa alipokuwa gerezani.Kilicho muua rafiki yako ni mamawzo aliyoyapata baada ya kumkuta Mke wake amemsaliti na ameshindwa kusimamia biashara alizo ziacha.

Mwanamke uliye muhangaikia kwa miaka yote akikusaliti wakati ukiwa kwenye matatizo lazima uchanganyikiwe-hii ilimpata hata Mandela akashindwa hata kumsamehe Winn
 
Mambo mengine akili itumike. Simkubali JPM wala m-CCm yoyote maana hawaaminiki. Ila, tuache uhuni. Malisa namhemshimu kwa harakati zake za kusaidia jamii, lakini kuna wakati anajichomoa betri na kupoteza credibility aliyojijengea kwa kuandika ndombolo.
Watanzania ni watu wa ajabu sana, leo hii hawa akina Mwigulu, na wengineo walafi wa hii nchi, siku ikatokea wakawajibishwa utashangaa akili ya watanzania itakavyobadilika na kuanza kuwatetea na kumsema vibaya aliyewawajibisha. Tutaendelea kutiwa vidole na CCM kwa akili hizi.
 
**Mwanamke uliye muhangaikia kwa miaka yote akikusaliti wakati ukiwa kwenye matatizo lazima uchanganyikiwe-hii ilimpata hata Mandela akashindwa hata kumsamehe Winn
No Mandela alimsamehe Winnie, kilichofanya wakatengana na hadi kutalikiana, ni issue nyingine iliojitokeza baada ya Mandela kuachiwa na sio issues za usaliti akiwa jela.
P
 
Wakati wa JPM alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akasota rumande miaka minne. Mwaka jana akaachiwa kwa NOLE. Aliporejea nyumbani akakuta biashara zake zimekufa. Mke ana mtoto mwingine aliyezaa nje ya ndoa. Mke anadai hakuplan ku-cheat ila changamoto za maisha zilimlazimisha. Baada ya kila kitu kuvurugika na maisha kuwa magumu alimpata "Sponsor" aliyekubali kulea watoto wawili wa jamaa akiwa jela.

Nimeumia sana. Pumzika kamanda. Siku zako nje ya jela zimekua NGUMU SANA kuliko ulipokua jela. Naamini umemsamehe mkeo. Naamini pia umemsamehe JPM aliyevuruga maisha yako na familia yako. Lala salama mwamba. Tutaonana baadae.! 😭😭

Malisa GJ
A very touching story.
JPM hakusiki na hicho kilichotokea ndio maana yuko mbinguni kwa Baba yake Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
 
Back
Top Bottom