Mambo mengine akili itumike. Simkubali JPM wala m-CCm yoyote maana hawaaminiki. Ila, tuache uhuni. Malisa namhemshimu kwa harakati zake za kusaidia jamii, lakini kuna wakati anajichomoa betri na kupoteza credibility aliyojijengea kwa kuandika ndombolo.
Watanzania ni watu wa ajabu sana, leo hii hawa akina Mwigulu, na wengineo walafi wa hii nchi, siku ikatokea wakawajibishwa utashangaa akili ya watanzania itakavyobadilika na kuanza kuwatetea na kumsema vibaya aliyewawajibisha. Tutaendelea kutiwa vidole na CCM kwa akili hizi.