Afariki baada ya kuanguka chooni kwa kupigwa stroke

Afariki baada ya kuanguka chooni kwa kupigwa stroke

Mkuu WERRA, kiongozi aliyezungumzwa hapo sio JPM, ni JKN, hata hivyo kuzimu sio motoni, jehanum, kuzimu ni pulgatory, watu walioko kuzimu ni wale wanaadhibiwa kisha wanaingia peponi. Hata JPM, sio lazima kuwa aliingia peponi siku ile ile aliyoondoka, alianzia kuzimu ndipo akaingia peponi!, hata Yesu, alipokufa pale msalabani, alishukia kuzimu, ndipo akafufuka siku ya 3!. Hivi tunavyo zungumza usikute marais wetu wote 3, saa hizi wako peponi, mbinguni kwa Baba!, hao wengine, sikuambiwa ila JPM, nimeambiwa yuko peponi!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
Huwezi toka kuzimu uende peponi ukitoka kuzimu ni jehanamu hasa ukifa bila toba.Ukifa bila dhambi mfano Moses Kulola, Bikira Maria,moja kwa moja mbinguni ukisubiria kwenda peponi au paradiso. Mbinguni ni makazi ya mda ya mfupi ya walio upande wa Mungu na kuzimu ni makao ya mda mfupi ya wafuasi wa shetani. Paradiso ni makao ya milele ya watatifu na kwa wafuasi wa shetani makao ya milele uitwa jehanamu. Hadi SAsa jehanamu na paradiso hazipo hadi baada ya hukumu.
 
Nyie washkaji gani sasa kama mlitelekeza jamaa yenu kwa kila kitu. Kiasi sponsor ndio alitoa hela ya wakili, ada za watoto, kula yao na mtaji kwa shemeji. Then jamaa anapotoka jela ndio mnakajidai ati kuwa nae karibu. Na sasa kafariki umekimbilia kumwandika mitandaoni, aisee sihitaji marafiki.
Umeongea point nzuri sana, huyu Malisa na wenzake wanafiki tuu.
 
Huenda hata aliyefariki humfahamu.

Mambo ya kukopi na kupesti.
 
Tumia akili ingekuwa ni msongo wa mawazo angekufa alipokuwa gerezani.Kilicho muua rafiki yako ni mamawzo aliyoyapata baada ya kumkuta Mke wake amemsaliti na ameshindwa kusimamia biashara alizo ziacha.
**Mwanamke uliye muhangaikia kwa miaka yote akikusaliti wakati ukiwa kwenye matatizo lazima uchanganyikiwe-hii ilimpata hata Mandela akashindwa hata kumsamehe Winn
Mandela alimhangaikia Winnie kivipi na kwa muda gani? Tafuta mfano wa kufanya ulinganisho, Mandela hafanani na haya.
 
Huwezi toka kuzimu uende peponi ukitoka kuzimu ni jehanamu hasa ukifa bila toba.Ukifa bila dhambi mfano Moses Kulola, Bikira Maria,moja kwa moja mbinguni ukisubiria kwenda peponi au paradiso. Mbinguni ni makazi ya mda ya mfupi ya walio upande wa Mungu na kuzimu ni makao ya mda mfupi ya wafuasi wa shetani. Paradiso ni makao ya milele ya watatifu na kwa wafuasi wa shetani makao ya milele uitwa jehanamu. Hadi SAsa jehanamu na paradiso hazipo hadi baada ya hukumu.
Issues za mbinguni, peponi, ahera, paradiso, kuzimu, toharani, jehanum, motoni, kiama etc, ni issues zinazochanganya sana kutokana na dini mbalimbali na mtu akifa nini kinafuatia.

Kwanza Mbinguni ndio peponi, ndio ahera, ndio paradiso ya raha ya milele. Kuzimu ndio toharani, motoni ndio jehanum kwenye moto wa milele.

Mimi ni Mkatoliki, tumefunzwa, unashukia kuzimu kusubiria hukumu ya mwanzo, kama dhambi zako ni chache, utakaa toharani kwa siku kadhaa za mateso, kisha utaingia mbiguni, kama dhambi zako ni nyingi, you just go straight to hell!.

Ile siku ya kiama ya hukumu ya mwisho ufufuko wa miili na uzima wa milele, ni baada ya Mwama wa Adamu kurudi kwa mara ya pili kwa utukufu, kuwafufua wazima na wafu, na ufalme wake hauna mwisho.

Watakaofufuliwa na kuingia kwenye huo uzima wa milele, ni wale tuu waliokufa wakiwa katika Kiristu Yesu, wengine wote ni to rot in hell!.
P
 
Nimesoma huo ujumbe naona shida iko kwa nyie marafiki zake..mlishindwa kumsaidia huyo shemeji yenu wakati jamaa yuko rumande hadi huyo sponsor akajitokeza.
Hicho mlichokifanya cha kumtafutia mtaji rafiki yenu mngekifanya mapema kwa shemeji yenu wakati rafiki yenu yuko jela..kwa kumsaidia kumpatia mtaji na kumtembelea kujua maendeleo yake lakini nyie mlimuacha na leo mnakuja kulaumu watu.
Poleni sana.
 
Sema huyu Bwana aliyekufa hakuwa na elimu ya kutosha kuhusu saikolojia ya maisha. Maisha ni nini, uhai ni nini, karma ni nini, do and don't do, laws of nature, causes and effects principal nk. Angeyajua hayo angekuwa kiongozi bora sana, hii Dunia sio ya kuikurupukia, wakati mwingine ishi easy way usilazimishe maji yapande mlima. At the end sisi ni wapangaji tu wa dunia zama zinapita na watu wake, mfano kizazi cha SAsa hata akijui Nyerere ni nani na alifanya nini , KILA kizazi kinaishi kwenye wakati wake. Hii Dunia ni kapeti ikanyage polepole.
 
JPM anahusika vipi na mke wake kucheat mpaka kuzaa?
Siku mtashindwa kuwapa unyumba wake zenu mtalaumu JPM.
Pumbavu sana
 
Ndio maana uwa namwomba Mungu siku akiichukua Roho yangu ningependa nifahamu walipo hakina Ben Saanane, Azory, JPM.....
Usisubiri hadi siku unachukuliwa ndio ujue walipo hao, anaweza kujua alipo JPM tuu kwasababu alifariki, Ben na Azory wao walipotea tuu, hivyo wanaweza wakawa huku au kule!. JPM umeishajua yuko wapi, ili uweze kumuona ni lazima ujiandae ili na wewe uende upande aliopo, ukitupwa kule, huwezi kuwaona wa kule kungine!.
P
 
Wakati wa JPM alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akasota rumande miaka minne. Mwaka jana akaachiwa kwa NOLE. Aliporejea nyumbani akakuta biashara zake zimekufa. Mke ana mtoto mwingine aliyezaa nje ya ndoa. Mke anadai hakuplan ku-cheat ila changamoto za maisha zilimlazimisha. Baada ya kila kitu kuvurugika na maisha kuwa magumu alimpata "Sponsor" aliyekubali kulea watoto wawili wa jamaa akiwa jela.

Ni "sponsor" huyohuyo aliyelipia gharama za mawakili waliomtetea jamaa hadi kuachiwa huru. Sponsor alitunza familia ya jamaa, akamlipia mawakili, akahakikisha watoto wake wanaendelea kusoma English Medium na hawarudi shule za Kayumba. Akamfungulia mke wa jamaa biashara ya saloon ili aweze kujikimu kwa mahitaji madogo, akamnunulia gari.

Jamaa alipotoka alipata depresion ya maisha, ndoa, uchumi etc. Washkaji zake tulijitahidi kumrudisha sawa lakini it was a locomotive process. Mke alijitetea kwamba yaliyotokea hakukusudia. Aliahidi kukatiza mahusiano na "sponsor" na badala yake watawasiliana kwenye malezi ya mtoto tu. Lakini somo hilo lilikua gumu kwa jamaa.

Jamaa alikua muongeaji sana kabla ya kufungwa. Lakini baada ya kutoka jela akawa mtu mkimya na asiyependa kutoka. Mara zote hujifungia ndani akiwaza na kusoma vitabu. Washkaji zake tuligundua yupo kwenye msongo. Kuporomoka kwa uchumi na kuyumba kwa ndoa yake vilimuumiza sana. Tukaweka utaratibu wa kumtembelea mara kwa mara, kumtia moyo na mara chache kutoka nae out japo kwa kumlazimisha.

Kuhusu mtoto tulimwambia kitanda hakizai haramu. Kuhusu uchumi tulimwambia ajipe moyo atarecorver kwani hayo ni mapito tu. Tulikua tayari kumchangia mtaji kidogo ili aanze kujipanga upya.

Jana nikapata taarifa kuwa ameanguka bafuni. Inadaiwa alipata stroke na mishipa ya kichwa kupasuka. Damu ikavilia kwenye ubongo, akapoteza fahamu. Akakimbizwa hospitali lakini alipofikishwa, madaktari wakasema si yeye bali ni mwili wake tu. Malaika Israel alimtwaa njiani kabla ya kufika hospitali.

Nimeumia sana. Pumzika kamanda. Siku zako nje ya jela zimekua NGUMU SANA kuliko ulipokua jela. Naamini umemsamehe mkeo. Naamini pia umemsamehe JPM aliyevuruga maisha yako na familia yako. Lala salama mwamba. Tutaonana baadae.! [emoji24][emoji24]

Malisa GJ
Yote hayo sababu ya Magufuli na ameharibu maisha ya watu wengi sana na familia nyingi zinapitia magumu.
 
Kesi nyingi za uhujumu uchumi kipindi cha JPM zilikuwa ni za kubumba ,rejea yule mafnyabiashara arusha aliyebambikiwa "Vipande vya mihogo" na askari wa sabaya wakamlazimisha atoe 100m otherwise watampa kesi ya uhujumu uchumi? Mfanyabiashara wa hotel sabaya alitaka kumbaka Nandi si alisema kwamba alilazimishwa atoe fedha?

Wafanyabiashara wengi kipindi cha JPM waliporwa pesa kwa kisingizio cha uhujumu uchumi ,Mahakama ipi ilihukumu kesi zao? Baada ya kuona hawana ushahidi ndipo JPM na ngosha mwenzake Maganga wakaanzisha plea bargain,kwa ili JIWE anahusika 100% kumfunga huyo jamaa na baada ya kufungwa hapo ndipo biashara zikayumba na baada ya biashara kuyumba kwakuwa mwenyewe yupo ndani ndipo mkewe ikabidi aachie PENZI.

Inamaanisha asingefungwa hayo yote ya biashara kuyumba na kuporwa penzi yasingetokea.
Huyo mwanamke ni malaya tu Kama wale wa barabarani.. kupanda na kushuka ni sehemu ya Maisha. Mwacheni jiwe apumzike... Hana hatia..
 
U
Nyie washkaji gani sasa kama mlitelekeza jamaa yenu kwa kila kitu. Kiasi sponsor ndio alitoa hela ya wakili, ada za watoto, kula yao na mtaji kwa shemeji. Then jamaa anapotoka jela ndio mnakajidai ati kuwa nae karibu. Na sasa kafariki umekimbilia kumwandika mitandaoni, aisee sihitaji marafiki.
Usikute sponsor ni mmoja wa marafiki zakee.. unacheza na Dunia wewe??
 
Hukumtaja Muhusika wala kutaja tuhuma zake sasa kwa nini uituhumu Mamlaka kwa kumtia hatiani?.

Ni vipi na sie tuta balance kuona kama hizo Mamlaka chini ya JPM zilimuonea au kweli alikuwa ana tuhuma?.

Kwa hiyo unataka kutuaminisha wote waliotuhumiwa wakati wa JPM walionewa?, kwamba hakukuwa na Wakosaji kabisa kipindi cha utawala wa JPM?. kama ndivyo na basi wote waliotuhumiwa na kutiwa hatiani kipindi hicho waachiliwe huru.
 
Usisubiri hadi siku unachukuliwa ndio ujue walipo hao, anaweza kujua alipo JPM tuu kwasababu alifariki, Ben na Azory wao walipotea tuu, hivyo wanaweza wakawa huku au kule!. JPM umeishajua yuko wapi, ili uweze kumuona ni lazima ujiandae ili na wewe uende upande aliopo, ukitupwa kule, huwezi kuwaona wa kule kungine!.
P
Tumetofautiana, mimi maisha yangu ya hapa Duniani natenda yaliyo mema.
 
Wakati wa JPM alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akasota rumande miaka minne. Mwaka jana akaachiwa kwa NOLE. Aliporejea nyumbani akakuta biashara zake zimekufa. Mke ana mtoto mwingine aliyezaa nje ya ndoa. Mke anadai hakuplan ku-cheat ila changamoto za maisha zilimlazimisha. Baada ya kila kitu kuvurugika na maisha kuwa magumu alimpata "Sponsor" aliyekubali kulea watoto wawili wa jamaa akiwa jela.

Ni "sponsor" huyohuyo aliyelipia gharama za mawakili waliomtetea jamaa hadi kuachiwa huru. Sponsor alitunza familia ya jamaa, akamlipia mawakili, akahakikisha watoto wake wanaendelea kusoma English Medium na hawarudi shule za Kayumba. Akamfungulia mke wa jamaa biashara ya saloon ili aweze kujikimu kwa mahitaji madogo, akamnunulia gari.

Jamaa alipotoka alipata depresion ya maisha, ndoa, uchumi etc. Washkaji zake tulijitahidi kumrudisha sawa lakini it was a locomotive process. Mke alijitetea kwamba yaliyotokea hakukusudia. Aliahidi kukatiza mahusiano na "sponsor" na badala yake watawasiliana kwenye malezi ya mtoto tu. Lakini somo hilo lilikua gumu kwa jamaa.

Jamaa alikua muongeaji sana kabla ya kufungwa. Lakini baada ya kutoka jela akawa mtu mkimya na asiyependa kutoka. Mara zote hujifungia ndani akiwaza na kusoma vitabu. Washkaji zake tuligundua yupo kwenye msongo. Kuporomoka kwa uchumi na kuyumba kwa ndoa yake vilimuumiza sana. Tukaweka utaratibu wa kumtembelea mara kwa mara, kumtia moyo na mara chache kutoka nae out japo kwa kumlazimisha.

Kuhusu mtoto tulimwambia kitanda hakizai haramu. Kuhusu uchumi tulimwambia ajipe moyo atarecorver kwani hayo ni mapito tu. Tulikua tayari kumchangia mtaji kidogo ili aanze kujipanga upya.

Jana nikapata taarifa kuwa ameanguka bafuni. Inadaiwa alipata stroke na mishipa ya kichwa kupasuka. Damu ikavilia kwenye ubongo, akapoteza fahamu. Akakimbizwa hospitali lakini alipofikishwa, madaktari wakasema si yeye bali ni mwili wake tu. Malaika Israel alimtwaa njiani kabla ya kufika hospitali.

Nimeumia sana. Pumzika kamanda. Siku zako nje ya jela zimekua NGUMU SANA kuliko ulipokua jela. Naamini umemsamehe mkeo. Naamini pia umemsamehe JPM aliyevuruga maisha yako na familia yako. Lala salama mwamba. Tutaonana baadae.! 😭😭

Malisa GJ
Nadhani sasa ni wakati mzuri wa kuachana na taarifa zemye uzushi au fabrications.

JamiiForums tunaomba majibu ya usahihi wa taarifa hii kupitia #JamiiFactsCheck

Taarifa ya kifo au msiba huwa haifichwi namna hii ili kutengeneza motion kwenye jamii
 
Hukumtaja Muhusika wala kutaja tuhuma zake sasa kwa nini uituhumu Mamlaka kwa kumtia hatiani?.

Ni vipi na sie tuta balance kuona kama hizo Mamlaka chini ya JPM zilimuonea au kweli alikuwa ana tuhuma?.

Kwa hiyo unataka kutuaminisha wote waliotuhumiwa wakati wa JPM walionewa?, kwamba hakukuwa na Wakosaji kabisa kipindi cha utawala wa JPM?. kama ndivyo na basi wote waliotuhumiwa na kutiwa hatiani kipindi hicho waachiliwe huru.
Ninachokiona hapa ni sense ya Moderator aliyefanya editing ya heading hakujipa muda wa kuisoma na kuielewa mada kisha angeihamishia ChitChat maana seems mtoa mada alikuwa amedhamiria kupiga soga na siyo kujenga hoja
 
Back
Top Bottom