Afariki baada ya kudaiwa kulishwa saruji na askari wa JWTZ

Utawafanya nini sasa?!!! Omba usiingie anga zao!
Tatizo haujui jinsi ya kuwawajibisha huyo jamaa anakua mdogo sana kuna ngazi za kuripoti huko kambini kwao maana mwanajeshi hatakiwi kumuonea mwananchi kwenye miongozo yao na ukifanya hivyo kazi huna na adhabu juu sema wabongo hatujui kudai haki zetu
 
Hivi kuishi jirani na hawa askari si ni faida na hatari zipo pia? Kwa mfano, jirani yako ni askari anaibiwa, si ataleta timbwili mtaani? Au wakianza vurumai wanawabagua majirani?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
sawa wote wana makosa hata kama umeibiwa unachukuaje sheria mkononi bila kufuata taratibu??

Yeah, wote wana makosa kamanda, lakini kujichukulia sheria mkononi na isitoshe amemuuwa, sio sawa kabisa.
 
Kuku anapoteza uhai wa mtu.

Na ukute chanzo cha kweli wala sio huyo kuku aliyetajwa hapo
 
Hakuna anayelazimishwa kuwa mwanjeshi nchi hii wote wanaokuwa wanajeshi walipenda na waliomba kufanya hiyo kazi kwa hiyari zao.
Tena ukiwakuta hao wanaotaka kua wanajeshi kwenye usahili wanavyoaangaika kila kona hadi kwa Waganga wa kienyeji ili mradi apate kazi ya Ulinzi! Akishapata Sasa utamjua Kama ndiyo yeye, kiburi na ujuwaji unakua juu sana!!
 
Kama kaua na yeye ndo mwisho wake kuanzia sasa ataachishwa kazi na atafikishwa mahakamani,kifungo cha maisha au miaka 30 kinamuhusu.
 
Utawafanya nini sasa?!!! Omba usiingie anga zao!
Na wao huwa wanaingia kwenye anga za kisheria na sheria huwa inawapa wanachostahili.
Mara kadhaa wameshapata hukumu za kunyongwa na vifungo vya maisha.
Hakuna aliye juu ya sheria.
 
🤣🤣🤣Huo ndio ukweli,au nyie Wenyewe mnajionaje?
Unachuki binafsi dhidi ya wanajeshi..
Kazi ya jeshi haimfanyi mtu kuwa mkatili au mkorofi hiyo ni character binafsi ya mtu.. Mbona kuna walimu wengi tu wanapiga hadi wanauwa watoto? Mbona kuna madaktari wengi tu wanawachoma watu sindano za sumu au kuwaambukiza magonjwa kwa makusudi? Na je mbona kuna wanajeshi wengi wako very kind and civilized sema hujakutana nao..
Kila mtu ana tabia yake na hakuna taasisi inayofundisha watu wake kukihuka haki za binadamu..
 
kabisa wakamalizane na wababe wenzao huko wakirud huku wamepoa
 
Dah inasikitisha sana
 
Tatizo haujui jinsi ya kuwawajibisha huyo jamaa anakua mdogo sana kuna ngazi za kuripoti huko kambini kwao maana mwanajeshi hatakiwi kumuonea mwananchi kwenye miongozo yao na ukifanya hivyo kazi huna na adhabu juu sema wabongo hatujui kudai haki zetu
point hatujui haki zetu na kuzidai ni majangaa
 
Uaskari flani wa kijinga na kishenzi
Askari anapaswa kuwa mfano sio mfano kwa ushenzi
 
Tena ukiwakuta hao wanaotaka kua wanajeshi kwenye usahili wanavyoaangaika kila kona hadi kwa Waganga wa kienyeji ili mradi apate kazi ya Ulinzi! Akishapata Sasa utamjua Kama ndiyo yeye, kiburi na ujuwaji unakua juu sana!!
hadi kuhonga mtu ana honga
 
Utawafanya nini sasa?!!! Omba usiingie anga zao!
Hamjui sheria ndugu zangu ndio maana mnawafanyia raia ubabe wa kisengerema mwisho wa siku mnapoteza kazi kijinga tu..
 
Kwa upande mwingine raia bora muendelee kuchapika tu kama hivi maana mna dharua za kifala sana tena wanajeshi huwa mnawaona wema sana kumbe ni wakorofi kuliko hata polisi ambao pia hututesa sometimes.
 
yan kwa hofu waliyo nayo raia kwa hawa watu unaweza kuta mwanajeshi anatembea kabisa na mke wa raia na raia anajua na anatulia tuli kama hajui kinachoendelea vile dah hii hofu cjui itaisha lini huku uraiani
Aisee, utembee na mke wangu halafu nikaushe kabisa. Weee.!

Nitaomba maombi yafike kwa Mungu au la ai hivyo wataalamu si wapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…