Afariki baada ya kudaiwa kulishwa saruji na askari wa JWTZ

Afariki baada ya kudaiwa kulishwa saruji na askari wa JWTZ

Mkuu unavyoona adhabu aliyopewa inastahili kwa umri wake?
Askari angemchukulia hatua za kisheria ukafanyika na uchunguzi akalipwa mali yake kungekuwa na haja ya haya yote?
Mimi naona kutoa uhai wa mtu kwa makosa hayo kama hakuna ulazima, ni kujitafutia hatia zisizo na ulazima. Bora hata angefanya ujambazi na kuiba vitu vya thamani sawa, lakini kuku anatoa uhai wa mtu?
Haiingii akilini ndugu.
yaan ni aibu kuna kesi nyingine hata wakili huwezi pata maana naye ataonekana hana akili pia
 
Wanajeshi tunawachekea sana. Kuna watu unakuta wanakaa wanasifia hivi vitendo vyao vya kishenzi.
Kuna raia wengi sana kwenye nchi ambao ni sadists na mazombi.
 
[emoji1787][emoji1787]yan hawa jamaa dah sijui hii kitu itaisha lini yan unaweza ukawa huna kosa kabisa ila sasa ukipita hapo kambini kwao utakutwa na kosa tu kama traffic vile akikusimamisha hakosi kosa hata kwenye zile kambi zao za makazi mfano ile ya Kigambon kule nilienda kumchek jamaa yangu yaan bila ya yeye kutokea washaanza kunigeuza nyama
Huu upuuzi utaisha siku raia wengi wakikataa na kusimama imara dhidi ya huo uovu. Tatizo hata uonevu kinyume cha sheria wanaofanyia raia huwa unazungumzwa kwa bashasha sana mitaani na kwenye vyombo vya habari.
 
tusiwafundishe tu ukakamavu na mbinu za kivita hawa wanajeshi wetu huko makambini...

Wanapaswa pia kufundishwa namna ya kuishi na raia huku uraiani...
Sheria zetu zipewe meno makali dhidi ya watu hawa wanapofanya uonevi kwa raia..
Jeshi letu la polisi lipewe meno kwa kushirikiana na MPs yanapotokea mambo kama haya..

Ni hatari sana kuwa na askari wasio na nidhamu kama huyu mpumbavu..
Kuna raia wengi uraini na waandishi kwenye vyombo vya habari huwa wanazungumzia haya matukio kwa bashasha sana.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nilikuwa uko morogoro vijijin, wanajeshi walipanda kwenye treni walikuwa wao tu behewa zima wakachukua mahindi ya kuchemsha kwa mmama wa watu alafu wakamwambia kamdai ela kikwete,

HAKIKA NILIWALAANI SANA WALE WANAJESHI. MMAMA WA WATU AKABAKI ANALIA TU
 
yaan kifupi mtz atakuangalia hivi unakufa mjeda anafanya vile anavyotaka yeye na anaweza kuwa peke yake raia hata 20 raia akijitahid sana atachukua video
Nchi iliyojaa watu waoga wasiojitambua.
 
Kinachowaudhi wanajeshi, ni vile wanateseka Kwa mazoezi usiku na mchana Kwa utayari kukulinda wewe muda wote na roho zao zikiwa mikononi, halafu wewe unayelindwa unawafanyia madharau! Hizo adhabu huwa ni tafsiri ya ujumbe jinsi gani huwafanya adui wa Taifa letu
Hakuna anayelazimishwa kuwa mwanjeshi nchi hii wote wanaokuwa wanajeshi walipenda na waliomba kufanya hiyo kazi kwa hiyari zao.
 
Huu upuuzi utaisha siku raia wengi wakikataa na kusimama imara dhidi ya huo uovu. Tatizo hata uonevu kinyume cha sheria wanaofanyia raia huwa unazungumzwa kwa bashasha sana mitaani na kwenye vyombo vya habari.
kweli kabisaa
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nilikuwa uko morogoro vijijin, wanajeshi walipanda kwenye treni walikuwa wao tu behewa zima wakachukua mahindi ya kuchemsha kwa mmama wa watu alafu wakamwambia kamdai ela kikwete,

HAKIKA NILIWALAANI SANA WALE WANAJESHI. MMAMA WA WATU AKABAKI ANALIA TU
dah dah kama hawana wazazi hapo mama anategemea auze watoto wake wapate kula
 
kabisa yan wala hujakosea huku kwetu kuna mmoja huyo kwanza kabisa huwa hapendi kabisa watu wajue yeye ni nani na sare za Jeshi huwezi mkuta amevaa kitaa halafu anatembea kwa mguu yule jamaa akiwa anaenda kazin akirud ndiyo utabahatika kuona amevaa sare na hapo hadi uchungulie kwenye gari halafu sasa ni mtu wa kujichanganya na raia yaan hana shida ni mtu watu na began ana nyota zake 3 zimetulia
Hawa mbavu mbili tatu na plain begani wengi ni wavuta bange na walevi
 
Nadhani Makosa yanayofanyika ni kule Serikali kuwaruhusu kujenga na kuishi pamoja na raia kitaa! Walipaswa watengewe maeneo yao ya kujenga na kuishi.
Ingawa kusema ukweli siyo wote,wapo wanajeshi wazuri tena wacha Mungu hawana ujinga kama huo.
Mimi nafikiri Serikali ingekuwa inawapeleka Syria,Yemen,Afghanstan,Iraq,Ukraine,Nigeria,Somalia kwenye vita ili wakamalizie hasira zao huko.
 
Mnaishi kizembe sana huko...yani mmeshindwa kuji organize wanakijiji kushughulikia wapumbavu hao kwa kuwapa kichapo heavy cha kiraia tu? Huo unyama mnauvumiliaje wazee??
 
Kinachowaudhi wanajeshi, ni vile wanateseka Kwa mazoezi usiku na mchana Kwa utayari kukulinda wewe muda wote na roho zao zikiwa mikononi, halafu wewe unayelindwa unawafanyia madharau! Hizo adhabu huwa ni tafsiri ya ujumbe jinsi gani huwafanya adui wa Taifa letu
WeWe ni mpumbavu
 
Juzi walikaribia kumtesa mtu mmoja asiyekuwa na hatia pale makongo.
Jamaa alikuwa anatokea mwenge. Alipofika pale Getini VTC lugalo akakaomba msaada askari mmoja mlevi naye akamuita ndani wakaanza kumpiga
Ati wanamuuliza una simu kama hii halafu u makosa nauli?
Pumbavu sana hawa
Ndugu zangu mtu kuwa JWTZ haina maana kwamba yupo juu ya sheria. Walichokifanya wale wanajeshi waliokuwepo pale mbele ya car wash karibu na geti la VTC ni kitendo cha kanyama na cha kipuuzi sana . Najua tukifuatilia kwa pamoja tutawajua. Ili kukomesha tabia hii mbaya na ya kishenzi kabisa. Unaombwa msaada na mtu badala ya kumsaidia unampiga KISA wewe mwanajeshi?
Haya mambo mwamunyange aliyakomesha naona yanarudi tena.
Tuyakatae.
Tukio lilitokea Jumatatu ya tarehe 3. Jan. 2022
 
Back
Top Bottom