Kuhusu madereva malori hao jamaa hawajali usalama wa bodaboda hata kidogo,Mimi nafanya nao sana kazi maana nipo katika mazingira ambayo nakutana nao Kila siku.
Huwa wanasema wakiwa barabarani hawaoni bodaboda,wanafagia na kupita kama wanakatiza sehemu isiyo na roho za watu. Ukiingia vibaya kwenye tajiri au trailer utajua mwenyewe na hawasimami,wanaona kama kaingia kuku tu chini ya lori.
Mfano hapa kwenye U turn ya bandarini wanavtofanya unagundua jamaa hawathamini roho za bodaboda Wala abiria wake. Umojifanya una haraka ya kuvuka na yeye anakuja hadungi breki Wala kupiga honi. Analeta gari spidi 120 bila kusimama.
Ukipands boda kama unatoka au unaenda ubungo,mkifika buguruni hasa jioni na asubuhi kwenye gombania goli mshike bega boda kisha mwambie tuliza wenge,vinginevyo mtakufa,malori ni noma ile kitaa.
wiki tatu zilizopita tumemzika mfanyakazi mwenzetu ambae alikuwa na pikipiki yake ya kutembelea. Alipitiwa na Lori hapo buguruni na pumzi yake ikakoma hapo.
BUGURUNI+ UHASIBU= DEATH GATE.