Afariki kwa kupata ajali Buguruni Dar 27.9.2024, atakayemtambua awajuze ndugu zake

Afariki kwa kupata ajali Buguruni Dar 27.9.2024, atakayemtambua awajuze ndugu zake

Status
Not open for further replies.
Luka 9:59-60
20240928_031303.jpg
 
Amefariki saa mbili asubuhi na amezikwa jioni hii. Masaa kama mawili yaliyopita ndiyo watu wametoka kuzika kwa sababu ya jinsi alivyopondeka kichwa.

Fuso lilimkanysga kichwani hapo buguruni.

R I P.
Reminds me of my late husband. Alipata ajali ya gari akafariki hapohapo.Ni miaka miwili sasa lakini bado maumivu ya sura yake before and after hainitoki akilini.
Eeh Mungu tupe mwisho mwema
Mrembo apumzike kwa amani🙏
 
Ni kweli madereva wa malori na daladala wanashida hiyo, ila kwa asilimia 90 bodaboda huwa wanakitafuta KIFO wenyewe.

Njia nyembamba atalazimisha kupita kati, lori lipo juu, apige hesabu ya tela lake.. na wewe pia akuweke ktk hesabu kwa haraka zako? Ubaya ukikosea ukateleza tuu yeye hana habari wala hajui lolote sana sana ataskia kichwa kimelia.

Pia yale hayana breki za ghafla useme atashika ghafla na kama amebeba mzigo ni hatari kwake yeye mwenyewe. Nimeshuhudia lori baada ya kushika brek ya ghafla mbao zilichomoka na kuponda kichwa cha lori zikitokea nyuma.

Bodaboda wawe makini, pia ktk highway tembea mwendo wa maana, ukijifanyq unanyata wanakufagia. Ni heri uendeshe service road, sio upo highway alaf unatembea na 20.
Aahh kummke aisee kweli tunatembea marehemu mkuu huwezi amini nimekula sana ruti za baiskeli kutoka tabata kwenda town kile kipande cha buguruni mpaka matumbi kuna siku nikaingia high way jamaa mpita njia akasema dogo utakufa huko pita hii service road leo ndio nimemuelewa....kweli ujafa ujaumbika.
 
Kwa kweli kama mtu una uwezo wa kuzikwepa bodaboda na Bajaj,zikimbie kabisa panga ratiba zako vizuri wahi kuamka au hakikisha kila ahadi yako na mtu unaiweka ktk ratiba itakayokufanya usianze kukimbizana barabarani ili utumie public transport utakuwa salama.

Kila mmoja ana ahadi yake lakini hivi vyombo viwili vinauwa kikatili sana tujaribu kujilinda,last month nilipoteza ndugu wawili Mbezi barabara ya Goba ajali ilihusisha Bajaj lorry na coaster ni mtihani sana.
Niliiona hiyo pole sana mkuu imefikia hatua kila nikifika eneo hilo naiwaza hiyo ajali
 
Reminds me of my late husband. Alipata ajali ya gari akafariki hapohapo.Ni miaka miwili sasa lakini bado maumivu ya sura yake before and after hainitoki akilini.
Eeh Mungu tupe mwisho mwema
Mrembo apumzike kwa amani🙏
Ooooh!

Pole sana kipenzi 🙏🏿
 
Huu mwaka vijana wadogo wameondoka wengi sana 😢wakiwa kwenye harakati hizo hizo za kujitafutia riziki, na usafiri ukiwa ni hizo bodaboda 😢😢sijamsahau mdogo wangu kila siku namuwaza, juzi nilitaka kujua kama marehemu baba alikuwa shabiki wa timu gani kati ya simba au yanga, nilikosa wa kumuuliza ila angekuwepo dogo chap ningepata majibu, wapumzike mahali pema marehemu wote, tutaonana badae🕊🕊🕊
 
Halafu uwe unanipa lift kwenye ile Discovery yako nyeusi kutokea huku Mbezi japo mara moja moja jamani. Usafiri shida sana hapa mjini jamani 🙏🏿
Hahahaha mi ni gombania goli tu ndo natafuta mkopo hapa hata nichukue chuma? Ila ile ngoma iliyotokea pale hata ungekuwa kwenye rolls Royce mzinga unakupata wa Lori ndiye alileta balaa
 
Nilijua tu,Buguruni hajafa mtu mara nyingi kama ajali haijahusisha lori

Mandela Road kipande cha kutoka Tabata uelekeo wa Buguruni na Tazara kunakuwaga na madereva fulani vichaa wasiojali utu wa wenye usafiri mdogo kuwashinda
Madereva wengi wanaoendesha malori kutoka ubungo hadi bandarini ni deiwaka,madereva wenyewe huwa wanachukua malori huko mbele ya safari. Hawa utingo deiwaka wengi ni wenye miaka 20s hivi ni wendawazimu kabisa.
 
Kuhusu madereva malori hao jamaa hawajali usalama wa bodaboda hata kidogo,Mimi nafanya nao sana kazi maana nipo katika mazingira ambayo nakutana nao Kila siku.

Huwa wanasema wakiwa barabarani hawaoni bodaboda,wanafagia na kupita kama wanakatiza sehemu isiyo na roho za watu. Ukiingia vibaya kwenye tajiri au trailer utajua mwenyewe na hawasimami,wanaona kama kaingia kuku tu chini ya lori.

Mfano hapa kwenye U turn ya bandarini wanavtofanya unagundua jamaa hawathamini roho za bodaboda Wala abiria wake. Umojifanya una haraka ya kuvuka na yeye anakuja hadungi breki Wala kupiga honi. Analeta gari spidi 120 bila kusimama.

Ukipands boda kama unatoka au unaenda ubungo,mkifika buguruni hasa jioni na asubuhi kwenye gombania goli mshike bega boda kisha mwambie tuliza wenge,vinginevyo mtakufa,malori ni noma ile kitaa.

wiki tatu zilizopita tumemzika mfanyakazi mwenzetu ambae alikuwa na pikipiki yake ya kutembelea. Alipitiwa na Lori hapo buguruni na pumzi yake ikakoma hapo.

BUGURUNI+ UHASIBU= DEATH GATE.
Inaonyesha usafiri wa bodaboda kwa Dar,hasa sehemu hizo,kama ulivyotahadharisha,siyo wakutumia kama mtu hulazimiki.Uwezekano ni mkubwa sana wa kutofika unakokwenda,salama.
R.I.P to young lady,the hustler.
 
Aahh kummke aisee kweli tunatembea marehemu mkuu huwezi amini nimekula sana ruti za baiskeli kutoka tabata kwenda town kile kipande cha buguruni mpaka matumbi kuna siku nikaingia high way jamaa mpita njia akasema dogo utakufa huko pita hii service road leo ndio nimemuelewa....kweli ujafa ujaumbika.
Usijaribu... hata ukiwa na gari pia tembea mwendo mzuri kiasi, kama speed huwez kaa lane ya kushoto at least.
 
Kwa kweli kama mtu una uwezo wa kuzikwepa bodaboda na Bajaj,zikimbie kabisa panga ratiba zako vizuri wahi kuamka au hakikisha kila ahadi yako na mtu unaiweka ktk ratiba itakayokufanya usianze kukimbizana barabarani ili utumie public transport utakuwa salama.

Kila mmoja ana ahadi yake lakini hivi vyombo viwili vinauwa kikatili sana tujaribu kujilinda,last month nilipoteza ndugu wawili Mbezi barabara ya Goba ajali ilihusisha Bajaj lorry na coaster ni mtihani sana.
Kufanya kazi ya bodaboda ni sawa na Askari aliyeko vitani ambaye hajui hatma ya maisha yake,hawa watu ilibidi wawe maofisini, viwandani, mashambani lakini sababu wamegeuzwa mitaji ya wanasiasa hakuna anayejali vifo vyao
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom