Afariki kwa kupata ajali Buguruni Dar 27.9.2024, atakayemtambua awajuze ndugu zake

Status
Not open for further replies.
Amefariki saa mbili asubuhi na amezikwa jioni hii. Masaa kama mawili yaliyopita ndiyo watu wametoka kuzika kwa sababu ya jinsi alivyopondeka kichwa.

Fuso lilimkanysga kichwani hapo buguruni.

R I P.
Reminds me of my late husband. Alipata ajali ya gari akafariki hapohapo.Ni miaka miwili sasa lakini bado maumivu ya sura yake before and after hainitoki akilini.
Eeh Mungu tupe mwisho mwema
Mrembo apumzike kwa amani๐Ÿ™
 
Aahh kummke aisee kweli tunatembea marehemu mkuu huwezi amini nimekula sana ruti za baiskeli kutoka tabata kwenda town kile kipande cha buguruni mpaka matumbi kuna siku nikaingia high way jamaa mpita njia akasema dogo utakufa huko pita hii service road leo ndio nimemuelewa....kweli ujafa ujaumbika.
 
Niliiona hiyo pole sana mkuu imefikia hatua kila nikifika eneo hilo naiwaza hiyo ajali
 
Reminds me of my late husband. Alipata ajali ya gari akafariki hapohapo.Ni miaka miwili sasa lakini bado maumivu ya sura yake before and after hainitoki akilini.
Eeh Mungu tupe mwisho mwema
Mrembo apumzike kwa amani๐Ÿ™
Ooooh!

Pole sana kipenzi ๐Ÿ™๐Ÿฟ
 
Huu mwaka vijana wadogo wameondoka wengi sana ๐Ÿ˜ขwakiwa kwenye harakati hizo hizo za kujitafutia riziki, na usafiri ukiwa ni hizo bodaboda ๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ขsijamsahau mdogo wangu kila siku namuwaza, juzi nilitaka kujua kama marehemu baba alikuwa shabiki wa timu gani kati ya simba au yanga, nilikosa wa kumuuliza ila angekuwepo dogo chap ningepata majibu, wapumzike mahali pema marehemu wote, tutaonana badae๐Ÿ•Š๐Ÿ•Š๐Ÿ•Š
 
Halafu uwe unanipa lift kwenye ile Discovery yako nyeusi kutokea huku Mbezi japo mara moja moja jamani. Usafiri shida sana hapa mjini jamani ๐Ÿ™๐Ÿฟ
Hahahaha mi ni gombania goli tu ndo natafuta mkopo hapa hata nichukue chuma? Ila ile ngoma iliyotokea pale hata ungekuwa kwenye rolls Royce mzinga unakupata wa Lori ndiye alileta balaa
 
Kuna uzi mwembamba sana kati ya mauti na uhai
Pumzika kwa amani dada
 
Nilijua tu,Buguruni hajafa mtu mara nyingi kama ajali haijahusisha lori

Mandela Road kipande cha kutoka Tabata uelekeo wa Buguruni na Tazara kunakuwaga na madereva fulani vichaa wasiojali utu wa wenye usafiri mdogo kuwashinda
Madereva wengi wanaoendesha malori kutoka ubungo hadi bandarini ni deiwaka,madereva wenyewe huwa wanachukua malori huko mbele ya safari. Hawa utingo deiwaka wengi ni wenye miaka 20s hivi ni wendawazimu kabisa.
 
Inaonyesha usafiri wa bodaboda kwa Dar,hasa sehemu hizo,kama ulivyotahadharisha,siyo wakutumia kama mtu hulazimiki.Uwezekano ni mkubwa sana wa kutofika unakokwenda,salama.
R.I.P to young lady,the hustler.
 
Usijaribu... hata ukiwa na gari pia tembea mwendo mzuri kiasi, kama speed huwez kaa lane ya kushoto at least.
 
Kufanya kazi ya bodaboda ni sawa na Askari aliyeko vitani ambaye hajui hatma ya maisha yake,hawa watu ilibidi wawe maofisini, viwandani, mashambani lakini sababu wamegeuzwa mitaji ya wanasiasa hakuna anayejali vifo vyao
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ