AFCON 2027: Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji

AFCON 2027: Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji

Mbona ni kijana unayeoneka kuwa na akili timamu na unamjua Mungu na Ukuu wake!!??
Inakuwaje kujitoa ufahamu kiasi hiki!!??

Nenda kasome mistari hii na uitafakari.

Yeremia 17:5
BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Zaburi 1:1
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Namtegemea na kumtumainia mwenyezi Mungu na ndio maana nimekuwa mwenye hofu ya Mungu kimatendo na kikauli,.ndio maana huoni nikiwashambulia watu humu kwa lugha za matusi au udhalilishaji wa aina yoyote ile
 
Serikali ya Tanzania imewezesha kwa kuwa imeonyesha mpango kazi wake wa namna ya kufanikisha michuano hiyo kwa kuweka miundombinu yote sawa na kuongeza mingine.ndio maana umeona mh Rais wetu kupitia Twitter ametoa maagizo ya ujenzi na ukamilishaji wa viwanja viwili vya kisasa ambapo kimoja kitakuwa Arusha na kingine Dodoma. lakini pia nafahamu unajuwa namna serikali ilivyowekeza mabilioni ya fedha katika kukarabati uwanja wa Benjamini mkapa ili uwe katika viwango bora kabisa vinavyohitajika. Lakini pia suala la usalama nalo pia serikali imehakikisha kuwa kunakuwepo na kuwahakikishia CAF suala hili wakati wote wa michuano hii. Na mengine mengi tu.
Hujajib maswal yang bali umeongelea infrastructure tu ambayo kwahiyo ipo mataifa mengi tu!! So jibu maswal yangu..
 
Ni Kishindoo ,ni shangwe,ni furaha ,ni nderemo , Ni tabasamu,ni vicheko na Raha tupu kwa Taifa la Tanzania na pongezi nyingi kwa Rais samia mama wa shoka ,chuma cha reli, shujaa wa Afrika na jasiri muongoza njia
😒😒
 
Unajifanya unajua kusifu sio bora hizo sifa ukamsifu mamako alokuzaa au upeleke hizo sifa kanisani kuliko kumpigia mbuzi gitaa ukidhani anaenjoy

huu ni upuuziii wa kiwango cha TBS
Kwani mama yangu alikuwa na nafasi ipi katika kuwezesha michuano hii ya Afrika kufanyika Nchini?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni Kishindoo ,ni shangwe,ni furaha ,ni nderemo , Ni tabasamu,ni vicheko na Raha tupu kwa Taifa la Tanzania na pongezi nyingi kwa Rais samia mama wa shoka ,chuma cha reli, shujaa wa Afrika na jasiri muongoza njia kuwezesha Tanzania kuwa Mwenyeji wa michuano ya Afrika 2027 kwa kushirikiana na nchi za kenya na Uganda. Hii Ni baada ya Tanzania kukidhi vigezo vilivyohitajika hasa kigezo cha usalama na vingine.

Kwa hakika Tanzania ya Rais samia Inaendelea kupata mafanikio kwa kila secta na eneo,kila awekapo mkono Rais Samia ni lazima pafanikiwe,ni lazima pawe na baraka.Rais samia ni ufunguo ufunguao fursa zote na milango yote ya fursa.chini ya uongozi wake tunakwenda kubeba fursa zote zinazopatikana hapa ulimwenguni.kwa kuwa Rais samia ni mtu mwenye mikakati,maono,Dira, ushawishi na malengo.

Ni kiongozi mwenye shabaha ambaye akilenga na kudhamiria jambo ni lazima afanikiwe na kupata ushindi.watanzania na Tanzania tunakwenda kushinda kwa kila kitu na kuibuka washindi kwa kila eneo.huu ni mwanzo tu lakini mazuri yanakuja huko mbele,hii ni rasha rasha tu katika ile mvua kubwa ya mafanikio ijayo mbeleni. Sasa hapa Tutembee kupata mafuriko ya watalii,wawekezaji,kupaa kwa Taifa letu katika anga la michezo, fursa ya kutangaza zaidi vivutio vyetu vya utalii.

Tunakwenda kushuhudia biashara zikifanyika vyema hasa za mahoteli, usafiri,vyakula n.k.Ni fursa ambayo inatupasa kuitumia vyema,ni fursa ambayo wizara hasa za utalii na maliasili. uwekezaji. michezo ,sanaa na utamaduni zinapaswa kuitumia vyema michuano hiyo katika kutengeneza faida za kiuchumi kwa Taifa letu. Kama Taifa tukawe wabunifu sana katika kuitumia vyema michuano hii ambayo inakuwa inafuatiliwa na karibu Dunia nzima.

Tukahakikishe Tunaibuka vinara wa kubeba fursa kupitia michuano hii,. wafanyabishara changamkieni fursa hii na jiandaeni kubeba fursa kwa kushirikiana na serikali yetu,.Kuweni karibu na serikali ili kupata taarifa na msaada mtakapoona mnahitaji msaada wa serikali yenu.

Ni lazima pia kama Taifa tumzawadie Rais samia muhula wa pili wa uongozi ili michuano hii ifaane na kupendeza sana na kufaidika na matunda ya juhudi zake za kuifanya Tanzania kuwa Mwenyeji wa michuano hii mikubwa kabisa barani Afrika.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Wewe una pepo au jini la unafiki, kwann kusifia hadi kupitiliza? Rais Samia amewezeshaje afcon? Ni kwasababu ya ile fedha ya kununua magoli au kajenga viwanja vipya? Unaemsifia nae anakushangaa.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Tunazidi kupoteana!
F6xfq_lXcAAF1vV.jpeg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni Kishindoo ,ni shangwe,ni furaha ,ni nderemo , Ni tabasamu,ni vicheko na Raha tupu kwa Taifa la Tanzania na pongezi nyingi kwa Rais samia mama wa shoka ,chuma cha reli, shujaa wa Afrika na jasiri muongoza njia kuwezesha Tanzania kuwa Mwenyeji wa michuano ya Afrika 2027 kwa kushirikiana na nchi za kenya na Uganda. Hii Ni baada ya Tanzania kukidhi vigezo vilivyohitajika hasa kigezo cha usalama na vingine.

Kwa hakika Tanzania ya Rais samia Inaendelea kupata mafanikio kwa kila secta na eneo,kila awekapo mkono Rais Samia ni lazima pafanikiwe,ni lazima pawe na baraka.Rais samia ni ufunguo ufunguao fursa zote na milango yote ya fursa.chini ya uongozi wake tunakwenda kubeba fursa zote zinazopatikana hapa ulimwenguni.kwa kuwa Rais samia ni mtu mwenye mikakati,maono,Dira, ushawishi na malengo.

Ni kiongozi mwenye shabaha ambaye akilenga na kudhamiria jambo ni lazima afanikiwe na kupata ushindi.watanzania na Tanzania tunakwenda kushinda kwa kila kitu na kuibuka washindi kwa kila eneo.huu ni mwanzo tu lakini mazuri yanakuja huko mbele,hii ni rasha rasha tu katika ile mvua kubwa ya mafanikio ijayo mbeleni. Sasa hapa Tutegemee kupata mafuriko ya watalii,wawekezaji,kupaa kwa Taifa letu katika anga la michezo, fursa ya kutangaza zaidi vivutio vyetu vya utalii.

Tunakwenda kushuhudia biashara zikifanyika vyema hasa za mahoteli, usafiri,vyakula n.k.Ni fursa ambayo inatupasa kuitumia vyema,ni fursa ambayo wizara hasa za utalii na maliasili. uwekezaji. michezo ,sanaa na utamaduni zinapaswa kuitumia vyema michuano hiyo katika kutengeneza faida za kiuchumi kwa Taifa letu. Kama Taifa tukawe wabunifu sana katika kuitumia vyema michuano hii ambayo inakuwa inafuatiliwa na karibu Dunia nzima.

Tukahakikishe Tunaibuka vinara wa kubeba fursa kupitia michuano hii,. wafanyabishara changamkieni fursa hii na jiandaeni kubeba fursa kwa kushirikiana na serikali yetu,.Kuweni karibu na serikali ili kupata taarifa na msaada mtakapoona mnahitaji msaada wa serikali yenu.

Ni lazima pia kama Taifa tumzawadie Rais samia muhula wa pili wa uongozi ili michuano hii ifaane na kupendeza sana na kufaidika na matunda ya juhudi zake za kuifanya Tanzania kuwa Mwenyeji wa michuano hii mikubwa kabisa barani Afrika.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
642786eaf89cd766b3c46b68b12fb506.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe una pepo au jini la unafiki, kwann kusifia hadi kupitiliza? Rais Samia amewezeshaje afcon? Ni kwasababu ya ile fedha ya kununua magoli au kajenga viwanja vipya? Unaemsifia nae anakushangaa.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
Ni serikali ya Rais samia imetoa mabilioni ya pesa kukarabati uwanja wa Benjamini mkapa,Ni serikali ya Rais samia inakwenda kujenga viwanja viwili vya kisasa Arusha na Dodoma,Ni serikali ya Rais samia kwa kutunza na kuendeleza amani nchini imepelekea kupata sifa ya kuandaa michuano hii.
 
TANZANIA, KENYA NA UGANDA MWENYEJI AFCON 2027

Nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zimepata dhamana ya kuandaa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027).

Akiongea mara baada ya kutangazwa matokeo hayo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe, Waziri wa Utamaduni, Sanaa Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema mpambano ulikuwa mkubwa na hatimaye EA Pamoja Bid ndiyo iliyopewa dhamana ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

"Tunawashukuru viongozi wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Dkt. William Ruto wa Kenya na Yoweri Museveni wa Uganda kwa utayari wao na kuunga mkono jambo hili kwa pamoja, hii imekuwa alama muhimu kwetu kuwa nchi zetu zipo tayari kuwa mwenyeji wa AFCON 2027" amesema Dkt. Ndumbaro.

Mashindano hayo kufanyika nchi za Afrika Mashariki ni dhamana kubwa kwa kuwa ni mara ya kwanza mashindano hayo kufanyika katika nchi hizo tangu mashindano hayo kuanzishwa miaka 66 iliyopita ikiwa ni mwaka 1957.

Mawaziri wa Michezo wa nchi hizo, Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania, Mhe. Ababu Namwamba, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Kenya na Mhe. Peter Ogwang, Waziri wa Nchi Elimu na Michezo, Uganda wamekuwa mstari wa mbele Cairo nchini Misri kufanikisha suala hilo.

Nchi ambazo zilikuwa kwenye kinyang'anyiro hicho ni Tanzania, Kenya na Uganda kwa kauli ya EA Pamoja Bid, Algeria, Benin na Nigeria, Botswana pamoja na Senegal.

F7A9snGWQAAcKbf.jpg
F7A9s0QXIAAJSJx.jpg
F7A9tC8XwAABcYJ.jpg
F7A9tSbW0AEiXEA.jpg
WhatsApp Image 2023-09-27 at 20.01.28.jpeg
 
Ndiyo nchi za mwanzo kuunda jumuiya ya Afrika mashariki. Rwanda, burundi, sudan kusini zijisikie vizuri tu kwa senior eac members kupata kuwa wenyeji wa afcon 2027.
 
Back
Top Bottom