AFCON 2027: Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji

Namtegemea na kumtumainia mwenyezi Mungu na ndio maana nimekuwa mwenye hofu ya Mungu kimatendo na kikauli,.ndio maana huoni nikiwashambulia watu humu kwa lugha za matusi au udhalilishaji wa aina yoyote ile
 
Hujajib maswal yang bali umeongelea infrastructure tu ambayo kwahiyo ipo mataifa mengi tu!! So jibu maswal yangu..
 
Ni Kishindoo ,ni shangwe,ni furaha ,ni nderemo , Ni tabasamu,ni vicheko na Raha tupu kwa Taifa la Tanzania na pongezi nyingi kwa Rais samia mama wa shoka ,chuma cha reli, shujaa wa Afrika na jasiri muongoza njia
😒😒
 
Unajifanya unajua kusifu sio bora hizo sifa ukamsifu mamako alokuzaa au upeleke hizo sifa kanisani kuliko kumpigia mbuzi gitaa ukidhani anaenjoy

huu ni upuuziii wa kiwango cha TBS
Kwani mama yangu alikuwa na nafasi ipi katika kuwezesha michuano hii ya Afrika kufanyika Nchini?
 
Wewe una pepo au jini la unafiki, kwann kusifia hadi kupitiliza? Rais Samia amewezeshaje afcon? Ni kwasababu ya ile fedha ya kununua magoli au kajenga viwanja vipya? Unaemsifia nae anakushangaa.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe una pepo au jini la unafiki, kwann kusifia hadi kupitiliza? Rais Samia amewezeshaje afcon? Ni kwasababu ya ile fedha ya kununua magoli au kajenga viwanja vipya? Unaemsifia nae anakushangaa.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
Ni serikali ya Rais samia imetoa mabilioni ya pesa kukarabati uwanja wa Benjamini mkapa,Ni serikali ya Rais samia inakwenda kujenga viwanja viwili vya kisasa Arusha na Dodoma,Ni serikali ya Rais samia kwa kutunza na kuendeleza amani nchini imepelekea kupata sifa ya kuandaa michuano hii.
 
Morocco kaaminiwa pekeake, Africa mashariki nchi3?
 
TANZANIA, KENYA NA UGANDA MWENYEJI AFCON 2027

Nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zimepata dhamana ya kuandaa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027).

Akiongea mara baada ya kutangazwa matokeo hayo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe, Waziri wa Utamaduni, Sanaa Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema mpambano ulikuwa mkubwa na hatimaye EA Pamoja Bid ndiyo iliyopewa dhamana ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

"Tunawashukuru viongozi wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Dkt. William Ruto wa Kenya na Yoweri Museveni wa Uganda kwa utayari wao na kuunga mkono jambo hili kwa pamoja, hii imekuwa alama muhimu kwetu kuwa nchi zetu zipo tayari kuwa mwenyeji wa AFCON 2027" amesema Dkt. Ndumbaro.

Mashindano hayo kufanyika nchi za Afrika Mashariki ni dhamana kubwa kwa kuwa ni mara ya kwanza mashindano hayo kufanyika katika nchi hizo tangu mashindano hayo kuanzishwa miaka 66 iliyopita ikiwa ni mwaka 1957.

Mawaziri wa Michezo wa nchi hizo, Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania, Mhe. Ababu Namwamba, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Kenya na Mhe. Peter Ogwang, Waziri wa Nchi Elimu na Michezo, Uganda wamekuwa mstari wa mbele Cairo nchini Misri kufanikisha suala hilo.

Nchi ambazo zilikuwa kwenye kinyang'anyiro hicho ni Tanzania, Kenya na Uganda kwa kauli ya EA Pamoja Bid, Algeria, Benin na Nigeria, Botswana pamoja na Senegal.

 
Ndiyo nchi za mwanzo kuunda jumuiya ya Afrika mashariki. Rwanda, burundi, sudan kusini zijisikie vizuri tu kwa senior eac members kupata kuwa wenyeji wa afcon 2027.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…