Afisa Elimu Ilala, DC Ilala fuatilieni Shule maeneo ya Vituka, Watoto wanabebeshwa Matofali na Michanga kwa ajili ya Ujenzi

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Kwako Afisa Elimu Ilala,
Poleni na majukumu ya kila siku.

Kuna shule moja ambapo mtoto wa rafiki yangu amehamia mwaka huu. Kwa wanachoona watoto, inasikitisha sana sana. Ile shule inaonekana ujenzi unaendelea wa mabweni na mengineyo.

Wanachofanya shule ni kubana matumizi. Kila jioni wanawabebesha watoto matofali umbali mrefu, na wengine wanabebeshwa mchanga kwenye virobaa.

Baadhi yao wameapa kuhamia hivi karibuni, lakini alichohadithia huyu mtoto wa kiume, aisee, inasikitisha sanasana.

Kwa heshima kubwa, DC, saidieni hawa watoto. Wasome wajibu wa shule kulipa wafanyakazi wa kubeba mchanga na matofali, na sio kubebesha wanafunzi.

Mungu awasaidie na poleni sana watoto mnayokutana nayo.
 
Kawaida tu na ww mbona unakuwa boya hivi si kazi za kawaida hizo shuleni.... na wewe uliandika huu uzi ni mtu mzima mayai..
 
Achaga ujinga mjuba, kuna ubaya gani hao watoto wakishiriki kujenga shule? Tukiwa wanafunzi wa msingi darasa la tano tulishiriki kusomba matofali kwa magari ya halmashauri kila jumamosi kwa zamu shule moja moja na baadaye ilipokamilika wenzetu wengine walipangiwa hapo first intake. Muachage kulea watoto kimayaimayai na kivivu. Watoto wafundishwe kufanya kazi wangali wadogo. Kazi ni kipimo cha utu
 
Nzasa Mbagala.
 
Ni sawa ni kazi
Ila
Inakuwa Usumbufu
Wanafunzi kukosa muda mwingi wa kusoma
 
Sisi wenyewe tulibeba tena zaidi ya km.20 ukute hao wanasogeza tu....
Shule sio darasani tu i pamoja na hizo skills
 
Reactions: K11
Vituka kuna shule nyingi...nyie mnaosema watoto wabebe matafali wajinga sana hao watoto wameenda shule kusoma hawajafanyiwa vipimo vya kubeba vitu vizito ujenzi wa taifa kwani wapo JKT....

Taifa lenyewe limejaa wahuni na matapeli mnataka muwatese watoto wetu.
 
Hiyo kazi itawasaidia zaidi kuliko hiyo Elimu yakwenye karatas
Ila isiwe chanzo cha wao kukosa muda wa kusoma na vipindi vya jioni kuachwa
Na vipi kuhusu darasa la mitihani ambao wanahitaji muda mwingi kusoma?

Alichosema Shule inabana matumiz
Kwa nn waliolipwa wasihusike
Na waalimu wanajipatia faida kwa kubana matumiz
 
Ni shule ya msingi au Secondary?
 
Hao walimu sio wajinga lazima kuna ratiba sidhani kama watoto watakosa vipindi sababu yakubeba matofali
 
Kuna shule ya Seminari naifahamu wao vipaumbele vyao ni 1. Sala 2. Kazi na 3. Elimu … na hivyo vipaumbele vimepewa umuhimu kulingana na namba hizo kwa hiyo ni mwendo wa kusali na kazi darasani ni sehemu ya tatu , ukimpeleka mtoto wako hapo mtoto wako hapo ananyooka, sijui siku hizi kama hizo values bado wanaziishi
 
Duuh!! Hivi mnataka kizazi cha aina gani? Sasa mtoto wa la 7 kubeba kitofali nayo ni nongwa? Angebebeshwa kupeleka nyumban kwa mwl si ungeripoti hadi UNICEF wewe. Vingine tuwe tunatazama tu hakuna tuzo za kuripoti hadi upuuzi.
 
Perception...

Naweza nika argue kwamba hio pia ni elimu ya kufundishwa uchapaji kazi, mazoezi au hata potentially kuwaandaa ukubwani kama ikitokea issue ya kubeba tofari waweze kujifanyia...

Sasa kama tofari zinahitaji kubebwa na watu ndio wanabeba unadhani hao watu wanatoka sayari gani kama sio dunia ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…