Tetesi: Afisa Elimu Sekondari Moshi Manispaa amuweka lokapu Mwalimu wa idara ya Elimu Msingi kisa Mwalimu kuuliza barua ya kazi maalum haina siku maalum

Tetesi: Afisa Elimu Sekondari Moshi Manispaa amuweka lokapu Mwalimu wa idara ya Elimu Msingi kisa Mwalimu kuuliza barua ya kazi maalum haina siku maalum

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Katika hali isiyo ya kawaida, mwalimu wa shule ya msingi Moshi Manispaa amewekwa lokapu kituo kikuu cha polisi Moshi na afisaelimu sekondari Moshi Manispaa, bila mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Moshi Manispaa kujua mwalimu aliko kwa muda wa siku mbili.

Kwa maelezo ya mwalimu huyo, alipangiwa kusimamia mitihani ys kidato cha pili shule ya sekondari iliyopo moshi Manispaa, baada ya kupangiwa kituo cha kaxi maalum , mwalimu huyu aliriporti kwenye kituo cha kazi maalum , ila mwalimu aliuliza kwanini barua aliyopewa haionyeshi atafanya kazi hiyo maalum kwa muda gani na malipo ni kiasi gani?

Baada ya mwalimu kuuliza swali hilo, alikwenda kukamatwa saa moja kamili tar 31.10.2022 na kupelekwa kituo cha polisi moshi mjini na kuwekwa ndani kwa kosa la kusababisha mgomo na afisaelimu sekondari kwa kushirikiana na afisaelimu msingi.

Mwalimu huyo kwa maelezo yake , afya yake sio nzuri na kulingana na maelezo yake pia anaonyedha ni mjane na alinyanyaswa sana na mwajiri wake alivyopigiwa simu alionyesha kutokujua kilichotokea .
Kwa hali ilivyo kwa sasa,
maafisaelimu wa sekondari na msingi wanawanyanyasa walimu wa kike kiasi kwamba wengi wanajilaumu kuajiriwa moshi manispaa kwmateso wanayopata.

Kwa hali ilivyo walimu wanafanya kazi ya baraza la mtihani bila kujua malipo yao kufuatana na miongozo ya baraza la mitihani kuhusu malipo ya kazi maalum.

Kuna kila dalili walimu wa kike wananyanyaswa kijinsia na uongozi wa elimu manispaa kwa kuwachukulia wao kazi wanapangiwa kazi yao ni kuzifanya bila malipo au kwa ujira mdogo.

Tunaomba mwalimu huyo awekewe ulinzi kwani mabosi wake wamemtishua maisha na ukixingatia kuwa ni mjane hana wa kumtetea.

Kila siku ameamriwa kuripoti kituo cha polisi Moshi bila kujali anatakiwa akafundishe watoto wala bila kujali nauli anspata wapi ya kwenda na kurudi kituo cha polisi.

Ombi, tunaomba iundwe tume ya kuchunguza kilichotokea na mjane ambaye ni mwalimu awekewe ulinzi ikiwa ni pamoja na mabosi waliohusika kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi .

Pili walio mabosi wa walimu ( elimu msingi)wamekaa kwenye vituo vya kazi kwa miaka 15 na zaidi hivyo kufanya kazi kwa mazoea na kutesa walimu wa kike tunaomba wahamishwe ili wakahudumu maeneo mengine angalsu walimu wapate nafuu ya kikazi na kimaisha..

Hali ya kikazi kwa walimu Moshi Majispaa sio rafiki kupitia kwa maafisaelimu wa msingi na Sekondari, walimu wengine wameamua kukimbia na kupotelea kusikojulikana .

Walimu wengine wa kike wamekuwa wakipata mateso hadi mimba walizonazo zinatoka kwa mateso na mikasa wanayopewa na mabosi wao.
 
Poleni Sana. Mfumo dume Bado ni ombwe katika Taifa hili. Viongozi wanaume hunyanyasa wanawake Kwa kutumia madaraka yao. Bado wanawake wanateseka. Na mbaya zaidi Kuna baadhi ya wanawake wapuuzi ambao hutumika kama daraja la kuonea wanawake wenzao. Hakika ni maumivu Kwa Taifa
 
Sio mfumo dune tu...lakini makazini kuna watu Wana roho mbaya...yaani mtu akipata madaraka anaona kama anaweza hata kugawa pumzi au uhai...wanajawa na kibri na full manyanyaso kwa wenzao ambao wapo chini Yao...jinga kabisaaa
 
Tangu lini Afisa Elimu akamiliki chombo Cha dola? Aliwezaje kumuamuru Kamanda wa Polisi wa Wilaya?
Fika kituo kikuu cha polisi moshi mjini utakuta mwalimu alifunguliwa kesi ya uongo tarehe 31.19.2022 saa mbili asubuhi na kesi imesajiliwa kwenye kumbukumbu za polisi na mwalimu kuchukuliwa maelezo, kisa mwalimu ni mjane na maafisaelimu msingi na sekondari wanataka kutumia mbinu nje ya muongozo wa baraza kuwalipa wanavyotaka ili wajichukulie jasho la walimu wasimamizi wa kaxi maalumu .
 
Kuna wanawake wana majibu ya karaha sana.

Pongezi kwa Afisa Elimu katumia busara kubwa kumuweka lockup badala ya kufanya jambo baya.

Mpaka mtu anawekwa lockup kuna mengi mengine yamejiri
 
Kuna wanawake wana majibu ya karaha sana.

Pongezi kwa Afisa Elimu katumia busara kubwa kumuweka lockup badala ya kufanya jambo baya.

Mpaka mtu anawekwa lockup kuna mengi mengine yamejiri
Walimu wajane Moshi manispaa wamekuwa wakionewa sana .
Tume iundwe ili kupata majibu ila wapishe uchunguzi na tume iwe tume huru
 
Poleni Sana. Mfumo dume Bado ni ombwe katika Taifa hili. Viongozi wanaume hunyanyasa wanawake Kwa kutumia madaraka yao. Bado wanawake wanateseka. Na mbaya zaidi Kuna baadhi ya wanawake wapuuzi ambao hutumika kama daraja la kuonea wanawake wenzao. Hakika ni maumivu Kwa Taifa
Afisa elimu sekondari manispaa ta moshi siyo mwanaume huo mfumo dume unatoka wapi ni mwanamke kama huyo aliyenyanyaswa
 
Afisa elimu sekondari manispaa ta moshi siyo mwanaume huo mfumo dume unatoka wapi ni mwanamke kama huyo aliyenyanyaswa
Siri ni kubwa, tumeshauri tume huru iundwe.
Afisaelimu sekondari ni mwanamke na anahisua kuwa mwslimu ambaye ni mjane ana uhusiano na mume wake.

Mateso kwa walimu wa kike tupo idadi kubwa na walimu wa kike kwa moshi manispaa ni zaidi ya 75% ya walimu wote.
 
Tumesimuliwa hii habari upande mmoja tu. Tungepata na upande wa Afisa Elimu ili tuweke uwiano. Katika hali ya kawaida mtu hawezi kuwekwa rumande kwa kuuliza muda wa kazi hiyo maalumu na kiwango cha malipo. Lazima kutakuwa na jambo/mambo mengine ya ziada ama ya jinai au utovu wa nidhamu yaliyosababisha aswekwe rumande. Mleta mada ameegemea upande mmoja tu.
 
Siri ni kubwa, tumeshauri tume huru iundwe.
Afisaelimu sekondari ni mwanamke na anahisua kuwa mwslimu ambaye ni mjane ana uhusiano na mume wake.

Mateso kwa walimu wa kike tupo idadi kubwa na walimu wa kike kwa moshi manispaa ni zaidi ya 75% ya walimu wote.
😅😅mambo ya Dyudyu
 
Tangu lini Afisa Elimu akamiliki chombo Cha dola? Aliwezaje kumuamuru Kamanda wa Polisi wa Wilaya?
Kipindi cha mitihani, maafisa elimu huwa wanamiliki dola, yaani ile kamati ya mitihani wilaya inao hadi vyombo vya ulinzi. Hivyo, ilikuwa ni rahisi tu, anaundiwa kesi ya kutaka kukwamisha zoezi la mitihani, anawekwa ndani
 
Kwa hiyo huyo afisa elimu secondary analo jengo ambalo anatumia kuwaweka walimu mahabusu??
 
Afisa elimu secondary kesho atampelekea mwalimu wetu mahakamani au hii series itaishia hapo mahubusu ya afisa elimu secondary
 
Shida stories kama hizi tunasikia upande mmoja, tungesikia na upande wa afisa elimu tungekuwa na vya kuchangia
 
Back
Top Bottom