Tetesi: Afisa Elimu Sekondari Moshi Manispaa amuweka lokapu Mwalimu wa idara ya Elimu Msingi kisa Mwalimu kuuliza barua ya kazi maalum haina siku maalum

Tetesi: Afisa Elimu Sekondari Moshi Manispaa amuweka lokapu Mwalimu wa idara ya Elimu Msingi kisa Mwalimu kuuliza barua ya kazi maalum haina siku maalum

Kuna wanawake wana majibu ya karaha sana.

Pongezi kwa Afisa Elimu katumia busara kubwa kumuweka lockup badala ya kufanya jambo baya.

Mpaka mtu anawekwa lockup kuna mengi mengine yamejiri
Hivi inakuwaje mtu unamjibia mtuhumiwa na kubeba uhalisia wa muhusika? Mimi huwa sihangaiki moja kwa moja huwa najua ni muhusika mwenyewe aliyejibu, hiyo ni roho mbaya mbaya na matumizi mabaya ya madaraka, usisahau Kuna maisha baada ya uofisa elimu
 
Katika hali isiyo ya kawaida, mwalimu wa shule ya msingi Moshi Manispaa amewekwa lokapu kituo kikuu cha polisi Moshi na afisaelimu sekondari Moshi Manispaa, bila mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Moshi Manispaa kujua mwalimu aliko kwa muda wa siku mbili.

Kwa maelezo ya mwalimu huyo, alipangiwa kusimamia mitihani ys kidato cha pili shule ya sekondari iliyopo moshi Manispaa, baada ya kupangiwa kituo cha kaxi maalum , mwalimu huyu aliriporti kwenye kituo cha kazi maalum , ila mwalimu aliuliza kwanini barua aliyopewa haionyeshi atafanya kazi hiyo maalum kwa muda gani na malipo ni kiasi gani?

Baada ya mwalimu kuuliza swali hilo, alikwenda kukamatwa saa moja kamili tar 31.10.2022 na kupelekwa kituo cha polisi moshi mjini na kuwekwa ndani kwa kosa la kusababisha mgomo na afisaelimu sekondari kwa kushirikiana na afisaelimu msingi.

Mwalimu huyo kwa maelezo yake , afya yake sio nzuri na kulingana na maelezo yake pia anaonyedha ni mjane na alinyanyaswa sana na mwajiri wake alivyopigiwa simu alionyesha kutokujua kilichotokea .
Kwa hali ilivyo kwa sasa,
maafisaelimu wa sekondari na msingi wanawanyanyasa walimu wa kike kiasi kwamba wengi wanajilaumu kuajiriwa moshi manispaa kwmateso wanayopata.

Kwa hali ilivyo walimu wanafanya kazi ya baraza la mtihani bila kujua malipo yao kufuatana na miongozo ya baraza la mitihani kuhusu malipo ya kazi maalum.

Kuna kila dalili walimu wa kike wananyanyaswa kijinsia na uongozi wa elimu manispaa kwa kuwachukulia wao kazi wanapangiwa kazi yao ni kuzifanya bila malipo au kwa ujira mdogo.

Tunaomba mwalimu huyo awekewe ulinzi kwani mabosi wake wamemtishua maisha na ukixingatia kuwa ni mjane hana wa kumtetea.

Kila siku ameamriwa kuripoti kituo cha polisi Moshi bila kujali anatakiwa akafundishe watoto wala bila kujali nauli anspata wapi ya kwenda na kurudi kituo cha polisi.

Ombi, tunaomba iundwe tume ya kuchunguza kilichotokea na mjane ambaye ni mwalimu awekewe ulinzi ikiwa ni pamoja na mabosi waliohusika kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi .

Pili walio mabosi wa walimu ( elimu msingi)wamekaa kwenye vituo vya kazi kwa miaka 15 na zaidi hivyo kufanya kazi kwa mazoea na kutesa walimu wa kike tunaomba wahamishwe ili wakahudumu maeneo mengine angalsu walimu wapate nafuu ya kikazi na kimaisha..

Hali ya kikazi kwa walimu Moshi Majispaa sio rafiki kupitia kwa maafisaelimu wa msingi na Sekondari, walimu wengine wameamua kukimbia na kupotelea kusikojulikana .

Walimu wengine wa kike wamekuwa wakipata mateso hadi mimba walizonazo zinatoka kwa mateso na mikasa wanayopewa na mabosi wao.
Shule inaitwaje alipo huyo mwalimu aliyenyanyasika? Halafu unaongelea mwalimu inakuwaje unasema habari ya ujane?
 
One side of a story….

Kahimiza mgomo, ashughulikiwe.

Nchi haiwez kwenda kwa kubembelezana
 
Shida stories kama hizi tunasikia upande mmoja, tungesikia na upande wa afisa elimu tungekuwa na vya kuchangia
CV ya afisaelimu sekondari Moshi Manispaa, kidato cha nne alipata div 4.
Hata kujieleza au kutoa mada kwake ni yes au no.
Labda upatiwe nsmba yake umsikie, ni kilaza fulani
 
Tatizo mwalimu alitaka kukitia mchanga kitumbua cha Afisa Elimu. Huu ndiyo msimu wa mavuno kwa Maafisa Elimu wengi wa Sekondari na Msingi.
Hawa maafisa elimu hasa kwenye wilaya Wana shida Sana na chakushangaza tamisemi Ina maana hawayajui haya au wanataka mpaka mama Samia awapeleke semina elekezi kwa mambo kama haya juzi tu hukohuko Moshi amelipotiwa afisa elimu kutafuna wake za watu ambao ni walimu rushwa za ngono mpaka kuficha vitendo vya kulawitiana wanafunzi duh!!
 
Hivi kuna kifungu kinachomruhusu afisa elimu kumuweka mtu Lock up? Kama hakipo achukuliwe hatua na hata kuachishwa kazi. Hata kama kipo, swali alilouliza mwalimu ni haki yake. Hao ni akina "unanijua mimi ni nani?" Wakati wa JPM walitokomea, sasa wanarudi tena.
 
Walimu wajane Moshi manispaa wamekuwa wakionewa sana .
Tume iundwe ili kupata majibu ila wapishe uchunguzi na tume iwe tume huru
Hii ya eti mwalimu mjane,sasa mjane ndiyo unyanyasike,inamaana mumewe angekuwepo asingenyanyasika,in short suala lichunguzwe,neno mjane lisitumike hovyo,ukute ana majibu ya hovyohovyo.
 
Back
Top Bottom