Tetesi: Afisa Elimu Sekondari Moshi Manispaa amuweka lokapu Mwalimu wa idara ya Elimu Msingi kisa Mwalimu kuuliza barua ya kazi maalum haina siku maalum

Kuna wanawake wana majibu ya karaha sana.

Pongezi kwa Afisa Elimu katumia busara kubwa kumuweka lockup badala ya kufanya jambo baya.

Mpaka mtu anawekwa lockup kuna mengi mengine yamejiri
Hivi inakuwaje mtu unamjibia mtuhumiwa na kubeba uhalisia wa muhusika? Mimi huwa sihangaiki moja kwa moja huwa najua ni muhusika mwenyewe aliyejibu, hiyo ni roho mbaya mbaya na matumizi mabaya ya madaraka, usisahau Kuna maisha baada ya uofisa elimu
 
Shule inaitwaje alipo huyo mwalimu aliyenyanyasika? Halafu unaongelea mwalimu inakuwaje unasema habari ya ujane?
 
One side of a story….

Kahimiza mgomo, ashughulikiwe.

Nchi haiwez kwenda kwa kubembelezana
 
Shida stories kama hizi tunasikia upande mmoja, tungesikia na upande wa afisa elimu tungekuwa na vya kuchangia
CV ya afisaelimu sekondari Moshi Manispaa, kidato cha nne alipata div 4.
Hata kujieleza au kutoa mada kwake ni yes au no.
Labda upatiwe nsmba yake umsikie, ni kilaza fulani
 
Tatizo mwalimu alitaka kukitia mchanga kitumbua cha Afisa Elimu. Huu ndiyo msimu wa mavuno kwa Maafisa Elimu wengi wa Sekondari na Msingi.
Hawa maafisa elimu hasa kwenye wilaya Wana shida Sana na chakushangaza tamisemi Ina maana hawayajui haya au wanataka mpaka mama Samia awapeleke semina elekezi kwa mambo kama haya juzi tu hukohuko Moshi amelipotiwa afisa elimu kutafuna wake za watu ambao ni walimu rushwa za ngono mpaka kuficha vitendo vya kulawitiana wanafunzi duh!!
 
Hivi kuna kifungu kinachomruhusu afisa elimu kumuweka mtu Lock up? Kama hakipo achukuliwe hatua na hata kuachishwa kazi. Hata kama kipo, swali alilouliza mwalimu ni haki yake. Hao ni akina "unanijua mimi ni nani?" Wakati wa JPM walitokomea, sasa wanarudi tena.
 
Walimu wajane Moshi manispaa wamekuwa wakionewa sana .
Tume iundwe ili kupata majibu ila wapishe uchunguzi na tume iwe tume huru
Hii ya eti mwalimu mjane,sasa mjane ndiyo unyanyasike,inamaana mumewe angekuwepo asingenyanyasika,in short suala lichunguzwe,neno mjane lisitumike hovyo,ukute ana majibu ya hovyohovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…