Afisa habari wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten ajiuzulu nafasi yake

Afisa habari wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten ajiuzulu nafasi yake

Status
Not open for further replies.

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten naye ameamua kujiuzulu nafasi yake ndani ya Yanga, Ten ameandika barua kwenda kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo akidai kwamba ameamua kujiuzulu kutokana na matatizo ya afya yake.

Dismas amejiuzulu nafasi yake siku mbili baada ya Katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Mkwasa kujiuzulu.
FB_IMG_15320686522490126.jpg
 
Huyu jamaa aliniblock kwenye page yake ya Instagram kwa kumwambia aache mafumbo, alikuwa anatumia mafumbo sana utafikiri taarabu
 
Bila manji kurudi yanga ndo basi tena!

Wako wapi wale waliokuwa wanasema wanaouwezo wa kutoa pesa hata manji akiondoka???
 
Mbona.
Kabla ya Manji, Yanga ilikuwepo na ilikuwa iko vizuri tu kwenye soka.
Au wafadhiri wote walikimbia baada ya Manji kuwa Mwenyekiti wa Yanga.
Je hawataki kurudi baada ya kuondoka, au Manji aliwafukuza Klabuni.
Nakumbuka kipindi fulani Mzee Mengi alikuwa karibu na timu ya Yanga na kama sikosei alikuwa mwanachama kabisa.
Kinachoendelea Jangwani hakipendezi katika medani ya soka letu.
Japo mimi si mpenzi wa Yanga lakini kiasi fulani inaniuma haswa kwa jinsi hali ya watani zetu inavyoendelea kudorola siku hadi siku.
" E Mwenyezi Mungu Uwasaidie waondoke kwenye hali hii mapema iwezekanavyo ili tukiwafunga wasije waka singizia ukata "
 
hali ni ngumu sana huenda hata MO anatafakari sasa
 
yani wote wana jiudhuru kwa kuwa na matatizo ya kiafya... jamani hii sio kweli, afya afya afya... basi yanga wawekeze katika afya ya akili ili viongozi wao wapate kunufaika na hili suala la afya...

Bin Kleb afya, manji afya, ten afya, mkwasa afya, yule mwingine afya... aiseee itakuwa afya ya akili...
 
Wajiuzulu wote ,tufanye uchaguzi tuanze upya.
Mtapata viongozi wapya lakini wachezaji wale wale waliocheza na Gor Mahia, maana hakutakuwa na nafasi ya kufanya usajili. Sana sana hata wengine waliocheza juzi watapungua, maana kuna waliojitolea kucheza bila kuwa na mkataba
 
yani wote wana jiudhuru kwa kuwa na matatizo ya kiafya... jamani hii sio kweli, afya afya afya... basi yanga wawekeze katika afya ya akili ili viongozi wao wapate kunufaika na hili suala la afya...

Bin Kleb afya, manji afya, ten afya, mkwasa afya, yule mwingine afya... aiseee itakuwa afya ya akili...
lakini usisahau klabu ilipo huenda ni UTI, Malaria, Kichocho ama any related to location
 
Nilikuwa na wazo. Hizi washabiki na wapenzi wa Dar Young Afrika hawawezi kufikia mil 5. Kama kila mmoja akichangia sh 10,000 makusanyo yatakuwa 50 Bilioni. Hizo pesa zikiwekwa kwenye fixed deposit ya 8% kwa mwaka, ina maana timu itakuwa inapata mgao wa milliob 330 kwa mwezi.

Kwa pesa hizo sifikirii kama timu itashindwa kujiendesha.

Yanga Daima.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom