XxxxxX
Twende Pamoja, kwa muda mrefu wapinzani wetu kisiasa wamekuwa wanasema udini na ukabila zaidi kwa swala la Ukabila wanalengwa watu kutoka mkoa wa Kilimanjaro anakotokea Mwenyekiti wetu wa Taifa. Naomba nikushirikishe na wewe upime Je kuna ukweli wowote?
Secretariat ambacho ni chombo cha kiutendaji cha kila siku yaani engine ya Chama ina wajumbe 10 mpaka sasa. Wajumbe hawa wamegawanyika katika sehemu kuu tatu
1. Wajumbe wa kuchaguliwa na Baraza Kuu. Hapa naongelea Makatibu wa Mabaraza yote matatu (Bavicha , Bawacha na Bazecha)
2. Wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na baraza kuu. Hapa nawaongelea Katibu Mkuu na Manaibu Katibu Mkuu
3. Wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Kamati Kuu. Hapa nawaongelea wakurugenzi
Kwa mantiki hiyo, wajumbe wa moja kwa moja wanaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa ni Katibu Mkuu, Naibu Bara , Naibu Zanzibar na wakurugenzi.
UKABILA
Mpaka sasa hivi Makao Makuu wapo wakurugenzi wanne kati ya hawa wakurugenzi watatu wanatoka mkoa wa Kilimanjaro majina yao ni
Reggy Munisi - Mchaga kutoka moshi (machame)
Jonathan Mndeme - Mpare kutoka same na John Mrema - mchaga kutoka vunjo. Mkurugenzi mmoja tu ndo anatoka Mkoa wa Kagera Mzee Lutembeka na ni kwa vile tu wanamtumia ku save nafasi mbili kama Katibu Mkuu wa BAZECHA TAIFA na kwa taaluma yake wanamtumia kama mkurugenzi wa FEDHA NA RASILIMALI
Twende kwenye watumishi wa kawaida Maafisa
Hapo Makao Makuu mpaka sasa wapo wakuu wa idara na maafisa 9 kati ya Hao wakuu wa idara na maafisa 5 wanatokea mkoa wa Kilimanjaro. Kwa majina ni
1. Zuhuru Nkya - Mchaga anatokea HAI
2. Karimu Muro - mtoto wa mwisho wa kumzaa wa Zuhura Nkya - Mchaga anatokea HAI
3. Lucas Mrema - Mchaga anatokea Vunjo
4. John Ngauro - Mchaga anatokea moshi
5. Aron Mashuve - mpare anatokea same
UDINI
Hivi tunavyozungumza pale makao makuu Muislamu anayefanya kazi Makao Makuu ni lazima awe anatokea Mkoa wa KILIMANJARO. Wasiotokea mkoa wa KILIMANJARO wote baada ya chama kuanza kupokea RUZUKU wameondolewa kwenye UTUMISHI
Watumishi waliopo makao makuu ambao ni waisilamu ni watatu ambao ni Karimu Muro, Zuhura Nkya, Reggy wote hawa wanatokea mkoa wa KILIMANJARO . Watumishi ambao ni Waislamu wameondolewa kwa sababu Hawatoki KILIMANJARO ni Zainab Ashraf Kutoka Tanga na Halima Lichonyo Kutoka Ruangwa Lindi. (Chunguzeni)
Kwa ujumla wake makao makuu inawatumishi kwa maana ya Secretariat na Maafisa jumla 19. Kati ya Hao 9 wote wanatoka mkoa wa Kilimanjaro, Waislamu wote wanatokea Kilimanjaro isipokuwa mmoja tu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
Hivyo, Wapinzani wetu wamekuwa wanatupiga sana kwenye hii hoja ya UDINI na UKABILA kitu ambacho kwa jicho la kiuhalisia ni Kweli, tunatakiwa kuwa smart na kuondoa ombwe la namna hii. Lazima tupate mchanganyiko kutoka pande mbalimbali kutoka mikoa yetu. Uwakilishi uwe na uwiano wa haki na usawa.
Lazima tumwambie Mapema Mwenyekiti wetu Mtarajiwa TUNDU ANTIPASI LISSU , kuwa hii Propanganda ambayo tunapigwa ya muda mrefu tuifute kwa kuja na mkakati mpya wa upatikanaji wa wakurugenzi na watumishi wa Makao Makuu wenye sura ya Kitaifa zaidi
Ikumbukwe hapa sijaongelea walinzi wala madereva
Naomba wajumbe wapiga kura tafadhali hilo tufanyie uamuzi sahihi Tuletee TUNDU LISSU ili tuje tujenge upya Chama chetu
Tusimame na LISSU 21 January.......!
Remigius Celestine
22.12.2024