Hii nchi ina raia wajinga kupindukia.
Mfano, mdogo fuatilia kinachoendelea kwenye uchaguzi wa TLS.
Wale ni mawakili tena wasomi, lakini japo wanajua ni nini Cha kufanya, wataacha kuchagua Mwabukusi ambaye ndiyo chaguo lao na kumpitisha mtu mwingine. Ukiuliza sababu? (Jibu lake ni aibu hata kuliandika hapa).
Haya turudi madani. Wewe ni mwanasheria, mfano yule wa Yanga. Timu imefunguliwa kesi mahakamani, mwanasheria anawashauri mabosi kwamba Yanga waende mahakamani kujitetea, lakini mabosi ya timu wanamwambia aachane na Magoma.
Baadaye Magoma anashinda kesi na Uongozi wa Yanga unatakiwa uondoke madarakani.
Hapa napo utamlaumu mwanasheria upumbavu wa uongozi uliokataa kufuata ushauri wa mwanasheria?
Unaweza ukawa msomi mzuri lakini unaowashauri wakagomea ushauri wako na mambo yakaenda mrama.
By the way, hakuna Kata imewahi kujenga chuo kikuu hapa Tanzania. Kama ipo nipewe jina lake.
Huyu jamaa wa Wang'ing'ombe naye ni bogus.
Hata kama labda kungekuwa na Kata yenye chuo kikuu, kwani Kuna tatizo gani mtu akisoma chuo hicho?
Tatizo letu bongo siyo wasomi bali ni mfumo wa maisha yetu na utamaduni wetu.