pilipili kichaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 18,406
- 14,643
Kwao nahisi wana asili ya uendawazimu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utofauti ni mkubwa asiliomia 85%,wala asijidanganye sisi tume yetu ni ya kutetea marais na chama tawala.Akiongea na kituo kimoja cha redio hapa nchini, mkurugenzi msaidizi wa elimu ya mpiga kura kuhusu tathimini yake ya uchaguzi uliomalizika hivi karibuni nchini Kenya, amesema hakuna tofauti kubwa ya namna tume ya uchaguzi ya Kenya inavyotekeleza hilo jukumu na tume yetu.
Inaonekana huyu afisa ana jinsi yake ya kutafsiri mfanano.
Amani au unyonge???Sema unyonge wa Watanzania unatokana na Tume hii tuliyonayo.Hakuna tofauti kubwa kimsingi kwa sababu hizi nchi mbili tofauti kila nchi inaangalia namna nzuri ya kufanya mambo yake hivyo si lazima tufanane kila kitu hata kama kuna maboresho yanatakiwa kufanyika kwa Tume yetu ya uchaguzi ni sawa lakini sio kutaka tufanane kila kitu. Hata hao kenya nao wana changamoto vilvile ndio maana Odinga alienda mahakamani kulalamika kuwa ameibiwa kura ingekua mfumo wao ni mzuri kiasi hicho usingesikia malalamiko yoyote.
Rejea hata uchaguzi wa Marekani ambao ndio wanajiita mapapa wa demokrasia Trump nae alilalamika sana kuwa ameibiwa kura kwa hiyo tusitake copy and paste toka kenya hata Ruto wakati anatoa hotuba yake juzi alisema atazidi kuimarisha Tume yao maana yake ni kuwa anaona kuwa ina mapungufu. Hali ya amani na utulivu tulio nao sasa haivi ni matokeo ya kazi iliyofanywa na hii hii Tume kwa hiyo tusiwe wanyonge kiasi hicho ila tushauri namna bora ya kuboresha utendaji wa Tume yetu.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.1.Tanzania tume ya uchaguzi huundwa kwa matakwa ya rais(mwenyekiti wa CCM).
2.Tanzania vyombo vya dola vinaiongoza tume ya uchaguzi.
3.Tanzania,wakurugenzi ndio wasimamizi wakuu wa uchaguzi majimboni.
4Tanzania inaongozwa na chama kilichopigania uhuru.
Ongezeeni na nyie tofauti za kiuchaguzi kati ya Tanzania na Kenya.
Je wewe kuna mahakama yoyote inayokubali kesi ya uchaguzi wa Rais??have you ever witnessed this? au unasikia tu vijiweni? vetting ni vetting na ndio utaratibu unaotumiwa kila mahali
Nikukumbushe tu kuwa hata hao kenya baada ya mahakama ya upeo kutoa uamuzi hakuna mahakama nyingine tena yenye uwezo wa kuhoji na ndipo alipoishia Odinga. Kama wana uhuru wa kiasi hicho si wangeruhusu mlalamikaji kukata rufaa baada ya mahakama ya upeo? Watz sijui nani katuloga kiasi kwamba kila tunachokifanya wenyewe tunakiona hakifai. Ndio maana mara zote nasema suala la msingi ni kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kuboresha ya kwetu lakini sio kuabudu vya watu ambavyo hata wenyewe hawavitaki leo wafuasi wa Odinga wote wanalia na uhuru wa Tume yao halafu sisi huku ndio tuko busy kuililia hiyo nadhani hata wao wanatuona mazwazwa wa kiwango cha lami.
Hata alipoishia odinga kwetu inawezekana?have you ever witnessed this? au unasikia tu vijiweni? vetting ni vetting na ndio utaratibu unaotumiwa kila mahali
Nikukumbushe tu kuwa hata hao kenya baada ya mahakama ya upeo kutoa uamuzi hakuna mahakama nyingine tena yenye uwezo wa kuhoji na ndipo alipoishia Odinga. Kama wana uhuru wa kiasi hicho si wangeruhusu mlalamikaji kukata rufaa baada ya mahakama ya upeo? Watz sijui nani katuloga kiasi kwamba kila tunachokifanya wenyewe tunakiona hakifai. Ndio maana mara zote nasema suala la msingi ni kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kuboresha ya kwetu lakini sio kuabudu vya watu ambavyo hata wenyewe hawavitaki leo wafuasi wa Odinga wote wanalia na uhuru wa Tume yao halafu sisi huku ndio tuko busy kuililia hiyo nadhani hata wao wanatuona mazwazwa wa kiwango cha lami.
Kuifananisha IEBC na Tume yetu ya uchaguzi, ni sawasawa na kusema jua na Dunia, vina umbali ambao mwenda kwa miguu, anaweza kwenda!
- Ni sawa na kusema hakuna tofauti Kati ya katiba ya Kenya na katiba ya Tanzania.
- Na mpaka kwenda on-air maafisa kadhaa wenzake wamemwandaa.
- Kutetea 'ugali' si mchezo, watu mpaka 'wanaungua'.
Tume ya Mahera na mwendazake.Tume za Uchaguzi zote duniani zinatekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria za uchaguzi katika nchi husika so sioni unachoshangaa ni nini maana Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania nayo inafanya vivo hivyo kama sheria zinavyoelekeza