Afisa wa tume: Tume yetu ya uchaguzi haina tofauti na ya Kenya

Utofauti ni mkubwa asiliomia 85%,wala asijidanganye sisi tume yetu ni ya kutetea marais na chama tawala.
 
Amani au unyonge???Sema unyonge wa Watanzania unatokana na Tume hii tuliyonayo.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
 
Je wewe kuna mahakama yoyote inayokubali kesi ya uchaguzi wa Rais??
 
Hata alipoishia odinga kwetu inawezekana?
 
  • Ni sawa na kusema hakuna tofauti Kati ya katiba ya Kenya na katiba ya Tanzania.
  • Na mpaka kwenda on-air maafisa kadhaa wenzake wamemwandaa.
  • Kutetea 'ugali' si mchezo, watu mpaka 'wanaungua'.
Kuifananisha IEBC na Tume yetu ya uchaguzi, ni sawasawa na kusema jua na Dunia, vina umbali ambao mwenda kwa miguu, anaweza kwenda!

Hivi utawezaje kuifananisha IEBC na Tume yetu ya uchaguzi, wakati unajua dhahiri kuwa IEBC, haijapitisha hata mgombea mmoja kupita bila kupingwa, wakati Tume yetu ilipitisha wagombea zaidi ya 18 kupita bila kupingwa?

Unawezaje kuifananisha IEBC na Tume yetu, wakati unajua wazi kuwa Tume yetu, iliruhusu "manjagu" kuingia na masanduku yenye kura feki vituoni?

Unawezaje kuifananisha IEBC na Tume yetu, wakati unajua wazi kuwa Tume yetu, haikuruhusu, mawakala wa vyama vya upinzani, hususani wa Chadema, wakati IEBC, iliruhusu mawakala hao, tena wakiingia na smart phones zao na kupiga picha, matokeo ya uchaguzi huo kwenye vituo vyao??
 
Tume za Uchaguzi zote duniani zinatekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria za uchaguzi katika nchi husika so sioni unachoshangaa ni nini maana Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania nayo inafanya vivo hivyo kama sheria zinavyoelekeza
 
Tume za Uchaguzi zote duniani zinatekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria za uchaguzi katika nchi husika so sioni unachoshangaa ni nini maana Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania nayo inafanya vivo hivyo kama sheria zinavyoelekeza
Tume ya Mahera na mwendazake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…